Israel: Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aomba kinga ya bunge dhidi ya mashitaka ya ufisadi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
1577951360581.png
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameamua kutafuta kinga ya bunge dhidi ya mashitaka ya ufisadi yanayomkabili.

Hatua hiyo huenda ikachelewesha kesi dhidi yake hadi uchaguzi utakapofanywa upya mwezi Machi.

Mwezi Novemba, Waziri Mkuu alishitakiwa na mwanasheria mkuu kwa kutoa hongo, kufanya udanganyifu na kuwavunja imani raia waliomchagua kuhusiana na kesi tatu tofauti.

Bw. Netanyahu, ambaye amekana makosa, atahitaji ungwaji mkono wa zaidi ya nusu ya wabunge kupewa kinga hiyo.

Kwanini anaomba kinga ya bunge?
Netanyahu ambaye ni kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo alidaiwa kukubali kuchukua zawadi kutoka kwa wafanyabiashara matajiri na kutoa hongo ili kuweza kuwa katika vyombo vya habari mara kwa mara.

Alitoa ombi hilo la kinga ya bunge kupitia hotuba ilipeperushwa kwenye televisheni saa nne kabla ya muda wa mwisho wa kutoa ombi hilo kumalizika.

Alisema "Nafanya hivi kwa mujibu wa sheria... kwa lengo la kuendelea kuwahudumia na mistakabali wa siku zijazo ya Israel".

Mwezi Machi, atakabiliwa na uchaguzi wa tatu wa kitaifa katika kipindi cha kwaka mmoja.

Kesi haiwezi kuanza ombi la kinga litakapowasilishwa katika bunge la Israeli, ambalo lilitakuwa limevunjwa kabla ya uchaguzi huenda likatoa uamuzi kuhusu ombi hilo kabla ya hapo.

Chini ya sheria ya Israeli, wanachama wa Knesset hawapewi kinga ya moja kwa moja dhidi ya mashitaka lakini wanaweza kuomba kinga wakati hali ikiwalazimu kufanya hivyo.

Waziri Mkuu wa Israel aliye madarakani anatakiwa kujiuzulu atakapo shitakiwa.

Chaguzi zilizopita zilizofanywa mwezi Aprili na Septemba mwa 2019 kiliifanya chama cha Bw. Netanyahu cha mrengo wa kulia cha Likud kujipata katika njia panda dhidi ya chama Blue na White hali iliyoifanya kushindwa kuunda serikali.

Changamoto za kisheria zinazomkabili Bw. Netanyahu zimekuwa kizingiti katika majadiliano. Amekuwa akisisitiza kuwa mashtaka hayo ni jaribio la mapinduzi dhidi yake.

''Sitakubali uongo kushamiri'', alisema katika hotuba ya kupinga kesi hiyo.

Mashtaka yanayomkabili
Mwanasheria mkuu Mandelblit alisema mwezi Februari kwamba alilenga kumshtaki bwana Netanyahu kutokana na kesi tatu tofauti zinazojulikana kama kesi 1000, kesi 2000 na kesi 4000 kabla ya kesi hiyo kusikilizwa mwezi uliopita.


  • Kesi ya 1000: Netanyahu ameshtakiwa na ulaghai na kuwavunja imani raia. Anadaiwa kupokea zawadi ya thamani ya juu ikiwemo mvinyo na sigara, kwa lengo la kumsaidia tajiri mmoja rafikiye. Bwana Netanyahu anasema kwamba alipokea vitu hivyo kama zawadi ya kirafiki na kwamba hakumfanyia hisani yoyote rafiki huyo. Rafiki huyo pia amekana kufanya makosa yoyote.

  • Kesi 2,000: Bwana Netanyahu anakabiliwa na mashtaka ya ulaghai na uvunjaji wa imani. Anadaiwa kukubaliana na mchapishaji wa gazeti moja kuweka sheria za kudhoofisha gazeti pinzani kwa lengo la kuangaziwa mara kwa mara na gazeti hilo. Mchapishaji huyo ameshtakiwa na mashtaka ya kutoa hongo . Sawa na waziri huyo mchapishaji wa gazeti hilo amekana kufanya makosa yoyote. Wote wawili wamesema kuwa hawakuwa na lengo la kukuza maswala waliozungumzia katika mkutano wao na kwamba hakuna sheria kama hiyo iliopitishwa.

  • Kesi 4,000: Haya ndio madai makali kwa sababu Bwana Netanyahu ameshtakiwa na tuhuma za kutoa hongo pamoja na ulaghai na uvunjaji wa imani za wengi. Imedaiwa kwamba alipitisha maamuzi ambayo yalikuwa yakipendelea kampuni moja ya mawasiliano kwa lengo la kuangaziwa mara kwa mara na vyombo vya habari , ikiwa ni miongoni mwa makubaliano na mwanahisa mkuu wa kampuni hiyo. Waziri Mkuu amesisitiza kwamba wataalam waliunga mkono uamuzi huo na kwamba hakulipwa chochote. Mwanahisa huyo ambaye pia naye amefunguliwa mashtaka ya hongo amekana madai hayo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Israel one of the most democratic nations in the world. Yakifichuliwa maovu ya wengine ambayo yanalindwa vilivyo kwa mikono ya chuma mbona hadi malango ya kuzimu yataachia yenyewe?
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jana ameliomba bunge la nchi hiyo kumpatia kinga, wiki kadhaa baada ya kiongozi huyo aliye kwenye shinikizo kushatakiwa kwa makosa kadhaa ya rushwa.

Netanyahu anayekabiliwa na kiwingu cha mashataka ya rushwa na mbinyo kutoka chama cha upinzani cha mrengo wa wastani amewaambia waandihi habari mjini Jerusalem kuwa kinga hiyo itamwezesha kuendelea kuitumikia Israel.

Ombi la kupatiwa kinga linatarajiwa kuchelewesha kwa miezi kadhaa kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili kwa sababau wabunge hawawezi kulipigia kura hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Machi.

Netanyahu alishatakiwa na mwanasheria mkuu wa serikali Novemba iliyopita kwa makosa matatu tofauti yanayojumuisha rushwa, udanganyifu na kupoteza uaminifu.Kiongozi huyo wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud mara kadhaa amekana kuwa na makosa kwenye kesi hiyo.

Benjamin Netanjahu Ministerpräsident von Israel (dpa)
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jana ameliomba bunge la nchi hiyo kumpatia kinga, wiki kadhaa baada ya kiongozi huyo aliye kwenye shinikizo kushatakiwa kwa makosa kadhaa ya rushwa.

Netanyahu anayekabiliwa na kiwingu cha mashataka ya rushwa na mbinyo kutoka chama cha upinzani cha mrengo wa wastani amewaambia waandihi habari mjini Jerusalem kuwa kinga hiyo itamwezesha kuendelea kuitumikia Israel.

Ombi la kupatiwa kinga linatarajiwa kuchelewesha kwa miezi kadhaa kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili kwa sababau wabunge hawawezi kulipigia kura hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Machi.

Netanyahu alishatakiwa na mwanasheria mkuu wa serikali Novemba iliyopita kwa makosa matatu tofauti yanayojumuisha rushwa, udanganyifu na kupoteza uaminifu.Kiongozi huyo wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud mara kadhaa amekana kuwa na makosa kwenye kesi hiyo.

Benjamin Netanjahu Ministerpräsident von Israel (dpa)
Naomba kuuliza hivi huyu waziri hana wakuu wake kama raisi nan. K
 
Huku kwetu pamoja na kwamba IQ inawalakini tukiuliza maswala ya kodi zetu watu wanaanza kugeuka mbogo kwenye ofisi zilizojengwa na kodi zetu!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom