Israel: Visa vya corona vyafikia zaidi ya 10,800, vifo zaidi ya 100; Uhaba wa vifaa vya kupimia watawala

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
Taifa teule la Israel laendeleza mapambano dhidi ya corona huku likiwa limerikodi visa zaidi ya 10,800 na vifo 103.

Hata hivyo maabara za nchi hiyo zimekumbwa na uhaba wa vifaa vya kupimia corona, na hivyo kupunguza upimaji wa watu wenye kuonesha dalali za ugonjwa huo. Mamlaka yatarajia kuanza kutengeneza vifaa vyake vya kupimia kwa material zinazopatikana nchini humo.

Pia Israel imeamua kupiga magoti kwa Uturuki, ikiomba msaada wa vifaa tiba vya kupambana na corona licha ya mahusiano mabaya yaliyopo baina ya nchi hizo mbili kutokana na manyanyaso ya Israel kwa wapalestina. Pamoja na mahusiano hayo mabovu, na pia Uturuki kuwa imeombwa msada wa aina hiyo na nchi nyinginezo takriban 100, Uturuki imeamua kuisaidia Israel.

Baadhi ya miji nchini Israel ipo kwenye lockdown/watu kuzuiliwa kuzagaa zagaa nje. Uvaaji wa mask umesisitizwa ili kupunguza maambukizi.
============



Screenshot_2020-04-12-16-57-03-1.png

Screenshot_2020-04-12-16-57-37-1-1.png


Screenshot_2020-04-12-17-26-11-1-1.png

Screenshot_2020-04-12-17-26-17-1.png
 
Hawa wapuuzi sinilisikia wamegundua dawa imekuaje tena mbna taifa teule linatuangusha hivi asee

Sema hawa mabwege kwakuficha idadi tu hawajambo

Sent using My COVID-19
 
Alaaaaa kumbe sasa nao wameanza kujua lockdowns maana yake
Wapalastine wako lockdown miaka
Acha wawasaidie ili wajitambue kuwa hakuna mbabe duniani


Sent from my iPhone using Tapatalk
aseee umeongea jambo ambalo linasikitisha sana ukanda waghaza toka mwaka 2007 wako lockdown PHALESTINE Yenyewe ndio Toka Mwaka 1948 iko lockdown wao waache waionje kidogo tu wauone utamu wake

Sent using My COVID-19
 
aseee umeongea jambo ambalo linasikitisha sana ukanda waghaza toka mwaka 2007 wako lockdown PHALESTINE Yenyewe ndio Toka Mwaka 1948 iko lockdown wao waache waionje kidogo tu wauone utamu wake

Sent using My COVID-19

Mungu mkubwa
Wao walikuwa wanawapiga kila kukicha na kuchukua ardhi yao kibabe
Lakini leo yamewakuta
What goes around comes around
Sasa acha waisome namba na wao
Mpaka yapite Haya heshima itarudi
Kweli Corona kiboko
Wanajeshi wao wawe na kazi ya kuzika sasa badala ya kupiga


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom