Israel/palestina conflict: Waarabu hujuwana kwa vilemba

m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,484
372
Kama ulikuwaunafuatilia vurugu za kisiasa katika Ghuba la Uajemi mwezi uliopita, yaanikuanzia uvamizi wa Ubalozi wa Israel kule Misri na ombi la Mr. Abbu Mazzeen (Mr.abbas)kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu kutambuliwa kwa Taifa la Palestina, ni vigumu kuamini kwamba masaa machache yaliyopita, zoezi la kubadlishana wafungwa kati ya Serikali ya Israel na Hamas, You heard me, HAMAS!!! limeanza kwa shangwe nanderemo.

Gilad Schalit ndio star wa zoezi hilo, na muda mfupi ujao, baada ya kuwa kifungoni kwa karibia miaka 5, atakabidhiwa kwa wazazi wake: Schalit anabadilishwa kwa wafungwa 1027 wa Kipalestina. What an asymmetricalexchange

Bila shaka katika zoezi hili kuna looser na winner.

Winner wa kwanza nadhani ni Natanyahu (Bibi)kwa kuweza kutimiza ahadi yake ya kumrudisha nyumbani salama salimini SergentSchalit. Hamas kwa upande wao, wameweza kuonyesha kwamba strategy zaoza kupambana na Israel ni bora zaidi kuliko zile za FATAH chini ya Mahd' Abbas.

Kwamba at least wameweza kufanyikisha kuachiliwa kwa wafungwa wengi, na ambao wamekuwa kifungono huko Israeli kwa zaidi ya miaka 15 kulinganisha na Mr.Abbas.


Misri, nao wameweza kujionyesha kwamba bado wana ushawishimkubwa katika ukanda huo wenye matatizo kwa kuweza kufanyikisha majadiliano kati ya Israel na Hamas na usimamizi wa zoezi hili muhimu la kubadilishana wafungwa.

Looser: Nadhani wa kwanza ni Mahmood Abbas.Ingawa amejaribu kufuata njia ya mjadala kuhusu utatuzi wa mgogoro waIsrael/Palestina, lakini ameshindwa kupata chochote kutoka Mr. Bibi, ambae yupotayari kuipa Hamas ushindi wa kisiasa kuliko Mr. Abbas.

Na hii kwa bahati mbaya, inaweza kuchangia ongezeko la utekaji nyara wa askari wa Israel kwa manufaa ya baadae.

Nadhani suala la msingi kwenye migogro ya Bara hili la Ghubaya Uajemi, labda kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, ni kwamba, hakuna kitukinachotokea kwa bahati hata siku moja.

Kila events huwa zinaambatana na calculations za hali ya juu na ambazo wakati mwingine hazihusiani na imani zaoza kidini (kama tunavyofikiria), bali zinazingatia political gains ( just imagine Israel na Hamas kwenye meza moja ya majadiliano).

Natumaini wadau wa jukwaa hili, na ambao huwa wanashambuliana kwa jazba, haswa kwenye topics zinazohusu Middle East Conflicts wataelewa jinsi siasa za bara hilo zinavyoendeshwa na kwa manufaa ya nani.


NB: TUSISAHAU ILEMETHALI YA KISWAHILI ISEMAYO, "UKIWAONA NDUGU 2 WANAPIGANA, BASI CHUKUWA JEMBE UKALIME."
 
m_kishuri

Wapalestiuna walivyo wanaweza wakawa wamefanya siri wawapokee watu wao wazima na kumtoa mwisraili marehemu kama ilivyokuwa yule mwanajeshi wa mika kama 3 au 4 hivi iliyopita waisraili hawakujua kuwa hamasi wameshamuua mjeshi na kubadilishana na wafungwa kwa maiti.
 
Last edited by a moderator:
Naona ktk hili Wapelastina na Arab ndiyo wameshinda zaidi. Kwa sababu, kama unakumbuka speech ya Obama kwamba Zion State itakuwa isolate zaidi kama haitoweza kutatua matatizo na jirani zake haswa ktk kipindi hichi cha Arab Spring.

Obama alipotoa hii speech alilaumiwa sana na Wayahudi kwa kuwatosa haswa pale Netanyahu alipoanza kubishana na Obama. Lakini hapa tunaona mshindi mwingine ni Obama; kwa sababu maneno aliyoyasema ni ya kweli.

Zion State imegundua kwamba Arab Spring imeleta chuki zaidi kwao, haswa pale walipoona Egypt walipofanya maandamano ya kupinga mauaji ya Wanajeshi wao, also pia mateso ya Wapelestina. Uhasama mwingine waliuona pale walipoona Turkey inazidi kuwa na siasa kali dhidi ya Israel.

Zion State wamegundua maneno ya Obama; kwamba wameanza kuwa Isolate in Mid East.

Hii yote waliyofanya kuhusu kubadilisha mwanajeshi ni Strategic plan ya kurudisha uhusiano mzuri na jirani zake na Arab States kama vile Egypt, Turkey, nk.

Goal yao si mwanajeshi kurudishwa; bali ni Urafiki na Arab States.

Natanyahu kagundua kwamba sera zake za ubabe zimepitwa na wakati. Kaamua kumsikiliza Obama.
 
Lakin hauoni kama ni tusi kwa waarabu hilo,yani mwanajesh mmoja kwa wafungwa zaidi ya 1000?
 
Back
Top Bottom