Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,510
- 28,416
Serikali ya Tanzania imesema kwa sasa iko kwenye mazungumzo na serikali ya Israel kuona ni namna gani Israel itaipatia Tanzania teknolojia mpya ya ndege zisizo na rubani "drones" ili kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa za wanyama.
Waziri wa Maliasili na Utalii Professor Jumanne Maghembe amesema mazungumzo yanakwenda vizuri na kwa sasa wanaangalia ni namna gani teknolojia hio itaweza kutumika katika mazingira ya kwetu.
Teknolojia hio itaweza kuwagundua majangili mara tu wanapoingia hifadhini kabla hata hawajaanza kuwaua wanyama hususani tembo kwa kutumia ndege ndogo ambazo hazina rubani.
Haya yamekuja baada ya Israel kukubali kufungua Ubalozi wake Dar es Salaam na hapo jana kuzindua kituo cha kushughulikia VISA ya kwenda Israel jijini Dar es Salaam.
Source: The Guardian.