Israel ilivyowaduwaza wanajeshi wa Idd Amin katika Operation Entebbe 1976

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Ilikuwa mwaka 1976- 27- june ndege ya Ufaransa A300 Airbus iliyokuwa ikitokea Israel ikapitia ugiriki Athens ilitekwa na magaidi wa Kipalestina na Ujerumani, ikiwa na abiria 254 wengi wakiwa ni waisrael,

Ndege hiyo ilibadirishwa mwelekeo na kupelekwa nchini Uganda uwanja wa ndege wa Entebbe, na Amin akaweka walinzi wa kuilinda,
Palestina walikuwa na lengo kushinikiza Israel iachie wafungwa raia wa Palestina, waliwahoji abiria wote na kuwaachia wasio wa Israel,

Baada ya habari kuwafikia Israel waliomba baraza la usalama la usafiri wa anga usijisumbue kuingilia suala ilo bali watamaliza wenyewe,

Walifanya uchunguzi ndani ya masaa 12 japo muda ulikuwa mfupi wakagundua
1. Uwanja na muundo wa uwamja wa Entebbe ulivyo,
2. Gari la Idd Amini muundo wake, ulivyo na aina yake,
3. Wakagundua umbali wa kutoka uwanja ulipo mpaka makao ya jeshi yalipo,
4. Wakataka kujua mateka walipotunzwa,

Baada ya kugundua hayo walifanya yafuatayo
Wakatafta gari kama la Idd amin na rangi ilivyo na plate number ya kufoji,
Wakatafta ndege tatu za kivita,
Wakaandaa wanajeshi kadhaa na makomandoo 35 wakiwa na mavazi ya wanajeshi ya uganda ,

Wakaanza safari mpaka Entebbe usiku wa manane , ndege ya kwanza ilitangulia iliyokuwa na magari natatu ya kufanana na convoy ya Amin,
Ndege zao za kivita ilibidi ziende juu meter 30 kuzuia detection, maana ikienda juu ya hapo itakuwa detect,

Ndege nyingine zilichelewa kufika,
Baada ya kufika magari matatu yakatoka kwenye ndege na kupita V.I.P japo gari la kwanza lilishtukiwa ambapo ilibidi wajeshi wa Israel watumie silent pistol kuwanyamazisha,

Wakapita vema na njian kwingine hawakupata tatizo maana ilikuwa ni kama masafara wa Rais ,

Baada ya kufika hapo vita ilipiganwa dakika 53 tu na kuwakomboa mateka

Walikufa wanajeshi 139 wa Uganda
Kwa upande wa Israel alikufa mwanajeshi mmoja na Muhim
Jonathan Netanyahu kaka wa waziri mkuu wa sasana Benjamin Netanyahu

Operation ikaisha , wakapandisha mateka na kurudi Tel Aviv ,
Kumbe kuna mama mmoja alisahaulika wa Israel, kwenye chumba maalumu cha hospital, kwa hasira Idd Amin alimuua kwa kumchinja na kuondoa moyo wake,
VIDEO FUPI KWA WASIO NA BANDO LA KUTOSHA



VIDEO / FULL DOCUMENTARY KWA MWENYE BANDO



Britannica
 
Mara nyingi huwez kuwa kiongozi wa Israel bila kupitia ujeshi, tena siyo kama wa Tanzania wa makotopola, ujeshi wenyewe
Hahah! Eti Makotopola....

Vipi baada ya zoezi la uokoaji kukamilika Uganda hawakuchukuliwa hatua zozote baada na wao kua wamehusika katika hilo zoezi?
 
Hahah! Eti Makotopola....

Vipi baada ya zoezi la uokoaji kukamilika Uganda hawakuchukuliwa hatua zozote baada na wao kua wamehusika katika hilo zoezi?
Yaan walipanga kiintelijent zaid, ni dakika 53 tu na kuondoka, wala wajeshi wa nje ya Entebbe hawakujua, hata Amin hakujua maana ilikuwa usiku hakujua kama kuna operation kama hiyo, aliamka asubuhi anakuta cinema, hebu angalia video

 
Yaan walipanga kiintelijent zaid, ni dakika 53 tu na kuondoka, wala wajeshi wa nje ya Entebbe hawakujua, hata Amin hakujua maana ilikuwa usiku hakujua kama kuna operation kama hiyo, aliamka asubuhi anakuta cinema, hebu angalia video

Ubarikiwe mkuu
 
Hahah! Eti Makotopola....

Vipi baada ya zoezi la uokoaji kukamilika Uganda hawakuchukuliwa hatua zozote baada na wao kua wamehusika katika hilo zoezi?
Uhanda sikujua hapo maana zoezi zima ilikuwa engineered na Palestina, Libya maana ndege ilipita benghazi kuongeza mafuta, alafu na uganda
 
Nauliza tu,israel bila uislam itakuwa na uadui na ukistro,
Maana kwenye vitabu ni wayahudi tu ndio hawakumuamini yesu.na matukio yote wao walipingana nao.
 
Pia ujue yafuatayo maiti ya yule bibi aliyeuwawa hospital ilikuja kupatikana mifupa yake kwenye mashamba ya miwa miaka miwili hivi baadae

Pia waziri mkuu wa sasa wa Israel ni komando wa kikosi cha sayaret maytikal
Alihusika kwenye uokozi wa mateka kwenye tukio jingine LA utekaji wa ndege ya sabena ambapo waziri mkuu mwingine ehud Barack aliongoza operation ile kwa mafanikio


Pia ujue karibu makomandoo wengi walioshiriki ile operation thunderbolt wengi walikuwa majenerali wa jeshi baadae yani rav aluf au prime ministers na wakuu wa vitengo mbalimbali mfano

Ehud olmet
Ehud barak
Benjamin netanyahu

Hawa wote walikuwa mawaziri wakuu baadae lakini wote walishiriki operation hatari sana ya thunderbolt ikumbukwe ehud olmet ndie aliyepiga picha za mwanzo kwa ndege ya kibinafsi uwanja wa entebe na kuzituma Israel kwaajili ya maandalizi ya operation

Israel sio ya kimchezo mchezo viongozi wao wote wanatokea majeshini tena baada ya kuprove mafanikio thabit

MTU kama ehud barak nadhani historia yake ya medani ya kimapigano ya kikosi cha komando cha sayaret matikal haijavunjwa mpaka wa Leo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom