Israel ilivyoishambulia gaza hivi karibuni: Chanzo, athari na hatima yake

kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,079
2,000
Mauaji ya Israel huko Gaza yameunganisha Wapalestina

http://www.mwananchi.co.tz/-/1596774/1630960/-/view/printVersion/-/vfoju9/-/index.html

file:///D:\DOCUME~2\CANCER\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image009.jpg
MCL
Na Nizar Visram (email the author)

Posted Jumatano,Novemba28 2012 saa 12:3 PM

Kwa ufupi
HATIMAE Israel imekubali kusaini mkataba wa kuacha kuishambulia Gaza baada ya siku nane za mauaji ya wananchi wa ukanda huo wa Palestina. Hii ni baada ya Misri kuwakutanisha Israel na wapiganaji wa Hamas na Islamic Jihad.

Katika mashambulizi hayo wakazi takriban 172 wa Gaza waliuawa, wakiwemo watoto 42, wanawake 11, vikongwe 18 na wanahabari watatu.
Kitoto cha miezi kumi kilikufa. Kingine ni cha miezi 11 pia. Mwanamke mwenye mimba ya mapacha naye aliuawa. Watoto wawili wa shule waliokuwa wakicheza mpira waliuawa. Familia ya Al-Dalou yenye watu 14 ilimalizwa, ikiwa na wanawake wanne na watoto sita.

Madege ya F-16 ya Israel yaliteketeza nyumba, shule, misikiti, ofisi za wanahabari na hata uwanja wa michezo. Alimradi Gaza imechakazwa kwa mabomu. Zaidi ya Wapalestina 11,000 walilazimika kujificha katika majengo ya Umoja wa Mataifa ili kuepuka makombora ya Israel.

Baada ya Israel kukubali kuacha mashambulizi, chama tawala cha Hamas huko Gaza kilitangaza sikukuu. Maelfu ya wananchi wa Gaza walimiminika mitaani wakisheherekea ushindi huku wakipeperusha bendera za Hamas, Islamic Jihad na Fatah. Viongozi wa vyama hivyo walipanda jukwaa moja na kuhutubia umati, kitu ambacho hakijawahi kutokea
Waandamanaji waliwapongeza wapiganaji wa Hamas na Islamic Jihad kwa ushindi. Ni ushindi wa Daudi aliyemkabili Goliathi. Israel ni nchi ya tano ulimwengu kwa nguvu za kijeshi na silaha za kisasa, pamoja na atomiki. Lakini vijiroketi vya Wapalestina viliwakosesha usingizi.
Kwa mara ya kwanza roketi hizo zilifanikiwa kufika hadi Tel Aviv na Jerusalem, kitu ambacho hakijafanyika tangu mwaka 1991 wakati wa vita vya Guba ya Uajemi.Israel kwa upande wake ilitumia ndege za kivita F-16 pamoja na vifaru na manowari za kijeshi. Waliamua kufuta likizo zote za wanajeshi na wakawaita wanajeshi 30,000 wa akiba. Hata hivyo, wapiganaji wa Palestina hawakusalimu amri.

Huu ndio ushindi uliosheherekewa huko Gaza. Muuza mboga mmoja alisema “Huu ni ushindi wa wananchi wote wa Gaza bila ya kujali itikadi.”
Ni vizuri kuelewa mashambulizi haya yalianzaje na chanzo chake ni nini. Vyombo vya habari vya magharibu vimekuwa vikizungumzia haja ya Israel kujilinda kutokana na maroketi ya Hamas. Israel inazungumzwa kana kwamba ni nchi inayoshambuliwa na maroketi kutoka Gaza.

Ukweli ni kuwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu hadi Novemba 6, 2012, Wapalestina 71 waliuawa na 291 kujeruhiwa huko Gaza kutokana na mabomu ya Israel. Wakati huo hakuna raia hata mmoja wa Israel aliyekufa kutokana na maroketi ya Gaza.
Katika hali kama hii, Novemba 4, mwaka huu majeshi ya Israel yalimuua raia Gaza aliyekuwa mgonjwa wa akili.Siku nne baadaye walimuua mtoto wa miaka 13 aliyekuwa akicheza mpira.

Baya zaidi, tarehe 14 Novemba Israel ilitumia ndege ya kivita kumuua Ahmed Jabari aliyekuwa kamanda wa Hamas.

Ni muhimu kujua kuwa wakati huo Jabari alikuwa akiratibu mkataba wa amani ya kudumu baina ya Hamas na Israel. Kulikuwepo na mazungumzo baina ya Israel na Hamas kuhusu makubaliano hayo, na Jabari alikuwa katika gari akielekea kwa wenzake wa Hamas ili nao wasaini, ndipo bomu la Israel lilipommaliza yeye na msaidizi wake.
Israel walijua fika uratibu huu wa Jabari. Kwani mkataba huo uliwahi kuzungumzwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyau na mawaziri wake tisa walipokutana Novemba 5, mwaka huu. Badala ya kusubiri kusainiwa kwa waraka huo Israel iliamua kumuua mratibu wake Jabari. Matokeo yake ni haya mapigano ya siku nane.Ni sawa na mashambulizi ya Disemba 2008 wakati Wapalestina 1,400 waliuawa na Israel. Nusu yao walikuwa raia wa kawaida. Kwa upande wa pili Israel ilipoteza wanajeshi 10 na raia watatu. Halafu tunaambiwa eti Israel inajikinga.

Rais Obama anadai eti Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Wapalestina. Wanataka tusahau kuwa ni Israel ndio iliyovamia na kukalia kijeshi ardhi ya Wapalestina, huku ikiwaua na kuwatesa kila kukicha.
Ni vizuri kujua sababu ya Israel kuanzisha mashambulizi na mauaji ya Gaza ya hivi majuzi. Netanyau anakabiliwa na uchaguzi tarehe 22 Januari 2013. Hii ni sehemu ya kampeni.

Anataka aonekane kuwa ni mbabe “anayelinda” Israel, badala ya raia wake kuzungumzia matatizo ya kimsingi yanayowakabili kama vile ufisadi wa vigogo na umaskini unaozidi kuongezeka. Kwa maneno mengine, Netanyau anabuni “adui” wa nje ili watu wasahau kuzungumzia migogoro ya ndani.
Inaonekana mbinu hii ilifanikiwa, ndipo mara tu baada ya Netanyau kuanza kuishambulia Gaza wapinzani wake walisimamisha kampeni dhidi yake, na wakamuunga mkono.
Hata hivyo, ni ndoto kufikiria wananchi milioni 1.7 wa Gaza watakubali kuishi katika hali duni huku wakizingirwa na majeshi ya Israel, wakinyimwa uhuru wa kutembea, uhuru wa kufanya kazi, hata uhuru wa kupokea misaada kutoka nje. Hili ni gereza kubwa duniani.

Suluhisho pekee ni kwa Israel kujitoa kutoka maeneo ya Palestina iliyoyavamia na kuwapa Wapalestina uhuru wao wa kujitawala. Sheria ya kimataifa, uamuzi wa mahakama ya kimataifa na maazimio mengi ya Umoja wa Mataifa yanaitaka Israel ifanye hivyo.
0713-562181
Source gazeti la mwananchi 28/November/2012

TZ biashara

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
523
0
Hii vita imeifanya Israel kuonyesha kuishiwa na nguvu na kuipa moyo Hamas na vilevile imemfaidisha Iran kwa upande mwingine.Kwasababu Gaza kubanwa kote na Israel lakini imeweza kupata silaha za kufika Tel Aviv.Na kingine kinachoipa moyo Gaza ni defence ya muisiraeli haina nguvu kutokana na kutoweza kuzuia rocket kutoka Gaza.Na Iran anazidi kuichora Israel kwa kuipima nguvu na vikundi vidogo pamoja na defence aliyonayo.Ikiwa Hezbullah wameweza kupeleka drone na kuscan sehemu za kijeshi pamoja na kupita karibu na nuclia site kwa muda wa zaidi ya masaa matatu inazunguka mpaka Palestina imefika bila ya kustukia?Sasa swali linakuja je ataiweza kuipiga Hezbullah maana haina haja ya kwenda Iran kwanza.:target:
 
MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,811
2,000

It was a sight that shocked the world - the corpse of Ribhi Badawi being dragged through the streets of Gaza City Tuesday by a motorcycle as Hamas gunmen fired into the air.

Read more: Hamas victim dragged through the streets of Gaza City Tuesday by motorcycle was no collaborator, widow says - NY Daily News

fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,985
0Watu walio la aniwa na Mungu wao kazi zao ku-uwa tu watu wasio na hatia.

Afu tazama wanajeshi wa Israel wanavyo malizwa hapo, wanaume wanauwa wanajeshi sio watoto.
 
Last edited by a moderator:

kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,079
2,000
Hii vita imeifanya Israel kuonyesha kuishiwa na nguvu na kuipa moyo Hamas na vilevile imemfaidisha Iran kwa upande mwingine.Kwasababu Gaza kubanwa kote na Israel lakini imeweza kupata silaha za kufika Tel Aviv.Na kingine kinachoipa moyo Gaza ni defence ya muisiraeli haina nguvu kutokana na kutoweza kuzuia rocket kutoka Gaza.Na Iran anazidi kuichora Israel kwa kuipima nguvu na vikundi vidogo pamoja na defence aliyonayo.Ikiwa Hezbullah wameweza kupeleka drone na kuscan sehemu za kijeshi pamoja na kupita karibu na nuclia site kwa muda wa zaidi ya masaa matatu inazunguka mpaka Palestina imefika bila ya kustukia?Sasa swali linakuja je ataiweza kuipiga Hezbullah maana haina haja ya kwenda Iran kwanza.:target:

Kama alivyosema mwandishi ni kuwa Israel ni taifa la Tano kwa nguvu za kijeshi duniani, Lakini pia Gaza ni kama jela kwa sababu Israel inamiliki mipaka yote ya ardhini ya angani na ya majini, na huwa inaingia Gaza ikiwa na silaha kaili inavyopenda. Gaza ni kasehemu kadogo sana kana KM za mraba 42, Gaza hairuhusiwi kununua au kuuza chochote bila ya idhini ya Israel, na kuna wakati Israel ilizuia Gaza wasipate hata dawa. Pamoja na hayo Israel in uwezo wa kuona mpaka mita kadhaa chini ya ardhi. Lakini cha kushangaza Hamas wameweza kutengeneza mabomu na kuyarusha nchini Israel kwa miongo kadhaa. Na cha ajabu mabomu hayo kila kukicha yanaongezeka umbali. Licha ya maguvu iliyonayo Israel haiachi kutembeza bakuli la kuomba msaada wa kijeshi na kulialia huko na huko. Kama imeshindwa kuwadhibiti watu wanaotumia manati na huku wao wakiwa na kila aina ya silaha nina wasiwasi sana wakikosea wakawachokoza wairan. Israel naifananisha na Uganda ya Idd Amini ambaye alikuwa na kila aina ya silaha na misaada tele, lakini tulimshinda na silaha zetu chache tena tukiwa hatuna misaada kama yeye.
 
Hawana kitu hao nguvu zao nikuomba USA/EUROPE wawasaidie, hawawezi hata siku moja kustand vita na warabu, kumbuka vita vyote walivyo pigana walikuwa nasaidiwa na marekani na ncvhi za ulaya lakini wanajidai wao ndo wanapigana.

Ungefatilia sababu gani Anuar Saddat alisimamisha vita, ni kwa sababu JESHI LA EGPTY kila likipiga hatua linakutana na majesho ya Italy, France, Germany, UK na USA wakimsaidia Israel...ndo Saddat akaona hakuna faida bora afanye nao peace tu.

Tazama hapa Nasrallah to Israel: You lost in Gaza, so who can you defeat?

Nasrallah to Israel: You lost in Gaza, so who can you defeat? – Israel News, Ynetnews.
Hezbollah leader says Israel's goal of ‘destroying Palestinian resistance's leadership' during Operation Pillar of Defense was not achieved; compares conflict to Second Lebanon War

Wakichokoza hapa ndo walie tu->>>
 
Last edited by a moderator:

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,659
2,000
Mimi hata sielewi ushindi wa Gaza ni nini. Wakati wapalestina 71 wakireportiwa kuuawa na zaidi 200 kujeruhiwa, tunaomba takwimu za Waisrael waliouawa na kujeruhiwa ktika mapigano hayo.

Pili anayesema Israel si inchi ya Waisrael, alete hapa vielelezo vinavyoonyesha wapalestina walianza lini kukalia hilo eneo hadi wafike waseme Israel ni mvamizi.

Ninashindwa kuelewa hapa Israel angefanyaje ndipo aonekane mshindi ikiwa kukubali kwake kuacha kushambulia na kusaini makubaliano ya amani ndio kuonekana kushindwa. Mngemwona Israel mshindi kama angeendelea kuwafyeka wakazi wote wa Gaza awafute katika uso wa dunia?

Israel kabarikiwa na Mungu aliye hai. Hutaweza kumlaani wewe hata utambike miungu. God Bless Israel.
 
Mkuu vita yoyote ile inakuwa na malengo makuu. Kwa hiyo kushinda vita kunategemea na kufanikiwa kwa malengo hayo. Kuua watu wasio na uwezo wa kujilinda kama vile vichanga, vikongwe na raia sio kushinda vita. Makaburu wa SA waliua watu wengi lakini walindwa. Wakoloni waliua maumau wengi lakini walishindwa. Hitler aliua watu wengi lakini alishindwaa. mifano ipo mingi. Tanzani tulimshinda Idd Amin sio kwa kuua watu wengi bali kwa kuuondoa mfumo mzima wa utawala.
Kwa mfano mwaka 2006 Israel ilitangaza vita ya siku saba kuishambulia Lebanon ikiwa na malengo makuu matatu. 1. kukifuta kikundi cha Hisbollah, 2. Kuwakomboa Waisrael waliokuwa wametekwa na Hisbollah 3. kutoa fundisho kwa kikundi chochote au nchi yoyote yenye lengo la kuichokoza Israel. Matokeo yake Israel ilifanya mashambulizi makubwa kwa muda wa siku 33 na hakukuwa na dalili zozote za Israel kufanikiwa malengo yake.
Baada ya kuona kuona hawafanikiwi na muda wa siku 7 umepita walianza kushambulia hovyo na kuua watu hovyo kwa hasira za kushindwa malengo. Mpaka leo hisbolla ipo hai na yenye nguvu.

Vita vya juzi Israel walikuwa na malengo matatu. 1. to destroy Palestine resistance leadership 2. to destroy resistance system 3. to reinforce Israel deterence power. Katika hayo hakuna hata moja iliyofanikiwa na badala yake wameingia kwenye makubaliano na huo ndio ushindi wa Palestine.
 
G. Activist

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
482
250
Kama alivyosema mwandishi ni kuwa Israel ni taifa la Tano kwa nguvu za kijeshi duniani, Lakini pia Gaza ni kama jela kwa sababu Israel inamiliki mipaka yote ya ardhini ya angani na ya majini, na huwa inaingia Gaza ikiwa na silaha kaili inavyopenda. Gaza ni kasehemu kadogo sana kana KM za mraba 42, Gaza hairuhusiwi kununua au kuuza chochote bila ya idhini ya Israel, na kuna wakati Israel ilizuia Gaza wasipate hata dawa. Pamoja na hayo Israel in uwezo wa kuona mpaka mita kadhaa chini ya ardhi. Lakini cha kushangaza Hamas wameweza kutengeneza mabomu na kuyarusha nchini Israel kwa miongo kadhaa. Na cha ajabu mabomu hayo kila kukicha yanaongezeka umbali. Licha ya maguvu iliyonayo Israel haiachi kutembeza bakuli la kuomba msaada wa kijeshi na kulialia huko na huko. Kama imeshindwa kuwadhibiti watu wanaotumia manati na huku wao wakiwa na kila aina ya silaha nina wasiwasi sana wakikosea wakawachokoza wairan. Israel naifananisha na Uganda ya Idd Amini ambaye alikuwa na kila aina ya silaha na misaada tele, lakini tulimshinda na silaha zetu chache tena tukiwa hatuna misaada kama yeye.

Israel wanasimama wao kama wao. Ila nchi zote za Kiislamu, Urusi, Iran, pamoja na China wanamupport Mparestina. Israel alikuwa anamtegemea sana mmarekani, lakini kwa miaka hii minne iloyopita ya uongozi wa Obama hajapata msada wa kijeshi kutoka nchini humo
 
kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,079
2,000
Israel wanasimama wao kama wao. Ila nchi zote za Kiislamu, Urusi, Iran, pamoja na China wanamupport Mparestina. Israel alikuwa anamtegemea sana mmarekani, lakini kwa miaka hii minne iloyopita ya uongozi wa Obama hajapata msada wa kijeshi kutoka nchini humo

Hakuna taifa duniani linalopata msaada wa kijeshi mkubwa kutoka nchi za magharibi kamba Israel. Kwa mfano kwa mwezi wa July Obama aliahidi kutoa dolo 70 milioni kusaidia Israel. lakini kwa kukusaidia andika military aid to Israel 2012 na u google

[h=2][/h]
 
M-Joka

JF-Expert Member
Dec 13, 2007
308
0
Mkuu vita yoyote ile inakuwa na malengo makuu. Kwa hiyo kushinda vita kunategemea na kufanikiwa kwa malengo hayo. Kuua watu wasio na uwezo wa kujilinda kama vile vichanga, vikongwe na raia sio kushinda vita. Makaburu wa SA waliua watu wengi lakini walindwa. Wakoloni waliua maumau wengi lakini walishindwa. Hitler aliua watu wengi lakini alishindwaa. mifano ipo mingi. Tanzani tulimshinda Idd Amin sio kwa kuua watu wengi bali kwa kuuondoa mfumo mzima wa utawala.
Kwa mfano mwaka 2006 Israel ilitangaza vita ya siku saba kuishambulia Lebanon ikiwa na malengo makuu matatu. 1. kukifuta kikundi cha Hisbollah, 2. Kuwakomboa Waisrael waliokuwa wametekwa na Hisbollah 3. kutoa fundisho kwa kikundi chochote au nchi yoyote yenye lengo la kuichokoza Israel. Matokeo yake Israel ilifanya mashambulizi makubwa kwa muda wa siku 33 na hakukuwa na dalili zozote za Israel kufanikiwa malengo yake.
Baada ya kuona kuona hawafanikiwi na muda wa siku 7 umepita walianza kushambulia hovyo na kuua watu hovyo kwa hasira za kushindwa malengo. Mpaka leo hisbolla ipo hai na yenye nguvu.

Vita vya juzi Israel walikuwa na malengo matatu. 1. to destroy Palestine resistance leadership 2. to destroy resistance system 3. to reinforce Israel deterence power. Katika hayo hakuna hata moja iliyofanikiwa na badala yake wameingia kwenye makubaliano na huo ndio ushindi wa Palestine.

Sadaqta mkuu, ni simple na moja kwa moja. Kwa kuongozea tu ni hivi katika upande wa kimaadili (moral grounds):

Wote (wengi)waliouawa Wapalestina ni waliodhulumiwa, innocent na wanapigania right and just cause, hivyo ni mashahidi mbele ya Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Taala)na malipo yao ni pepo, wakati wote (japo ni wachache)waliouawa waZayuni wote in general ni dhulumati, na kama miongoni mwao ni wale walio viburi (Zionists sio just Israelis) basi ni guilty na there abode is in hellfire. Na hili waZayuni wanalijuwa wazi na ni miongoni mwa linalowafanya wawe so enraged kwa kukosa angalau faraja angalau ya muda mfupi tu ya kutanua hapa duniani.

Kingine ni kwamba tayari ulimwengu umeshaitayarishia Hamas njia ya kusimama katika podiums za UN. Puppett Mahmood Abbas baada ya kuwa-side-lined katika huu mkataba ambao umeipandisha status Hamas, amepewa consolation ya "whatever the status" katika UN, ambapo kuna siku uchaguzi utaitishwa tena Palestina na ambapo Hamas watainuka tena kidedea hata kuliko walivyochaguliwa kuhalali na kidemokrasia in January 2006. Je Wazayuni na waMarekani wataifanya nini hiyo status ya observer membership wa UN? Hayo ya kukurupuka na kutangaza na kuanza kutanua settlements Jeruselem wacha liwekwe kiporo kwanza mpaka wamalize kwa maana wache wawajengee waPalestina nyumba zao za hapo baadae.

Katu Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.
 
nyabhera

JF-Expert Member
Nov 25, 2011
625
1,000
akili ni mali yaani Hamas amefyatua makomboro 1500 katika miji na makazi ya watu yote yayeyushwa na Israel afu wanasherekea Ushindi mjidanganye tu Misri iahajifunza sasa ni zamu ya Iran na Zanzibar kuishamburia Israe.
ila Jordan, lebanon, Misri na Syria hawanampango Mziki wa Jews wanaujua.
Ku

waarab, palestine na Waislam huenda vitani wakauwawe sasa ushindi ni pale wanapouwawa wengi zaidi ndo maana kila vita wanashinda tangu za ma za Moody
 
Mkabera

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
267
225

[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
[/FONT]

Yo is lockedYou are usingto confuse the public but the For the benefit of doubt:
1. The Jews are not Christians and believe Jesus is illegimate.
2. The Palestians some are Muslims and some are Christians. In fact all those churches like Church of Netibity is under Custodianship of them.
3. As history evolved If Jews were to kill Chagas and Hayas you will support because you have been deceived that to go Heaven that is the way! ? What kind of distorted belief!

I think you need to preach yourself because you are wasting your time,
 
Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,398
1,225
Muisrael 1 anajithaminisha sawa na wapalestina 1000,kama unakumbuka kuna wakati israel waliachia wafungwa wa kipalestina 1000 ili wapewe muisrael 1 aliyetoka na ndio kama exchange yao,,,,,in short ilikuwa ikipambana na kikundi ni sawa na kenya ilivyoenda kupigana na alshabab,huwa ni vita ngumu kupigana na kikundi kuliko nchi,ni mfano uganda ije tanzania kupigana na uamsho,hawataweza kwa sababu watapiga raia,na askari wa jeshi la tz na wanaweza sababisha mengineMimi hata sielewi ushindi wa Gaza ni nini. Wakati wapalestina 71 wakireportiwa kuuawa na zaidi 200 kujeruhiwa, tunaomba takwimu za Waisrael waliouawa na kujeruhiwa ktika mapigano hayo.

Pili anayesema Israel si inchi ya Waisrael, alete hapa vielelezo vinavyoonyesha wapalestina walianza lini kukalia hilo eneo hadi wafike waseme Israel ni mvamizi.

Ninashindwa kuelewa hapa Israel angefanyaje ndipo aonekane mshindi ikiwa kukubali kwake kuacha kushambulia na kusaini makubaliano ya amani ndio kuonekana kushindwa. Mngemwona Israel mshindi kama angeendelea kuwafyeka wakazi wote wa Gaza awafute katika uso wa dunia?

Israel kabarikiwa na Mungu aliye hai. Hutaweza kumlaani wewe hata utambike miungu. God Bless Israel.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom