Israel: Benjamin Netanyahu afanya kikao na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi & Usalama na kuagiza Mashambulizi dhidi ya Hamas yaendelee kwa nguvu kubwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,692
Muda mfupi uliopita Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyau amehitimisha kikao muhimu na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi & Usalama.

Kikao hicho kilifanya tathmini ya mashambulizi dhidi yaliyofanywa dhidi ya Hamas & kupitia/kuidhinisha mipango mbalimbali ya mashambulizi mapya yaliyowasilishwa na Jeshi la nchi hiyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mkuu wa Majeshi ya Israel, Mkuu wa Mossad, Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa na Mkuu wa Idara ya NSA.

Kikao hicho kiliagiza kuwa Mashambulizi dhidi ya Magaidi wa Hamas yaendelee kwa nguvu kubwa hadi pale hali ya Usalama wa Raia wa Israel itakaporejea kuwa nzuri.
 
Huyu bwana Benjamin muda mrefu sana namskia kwenye utawala wa huku Israel..na mara zote anavuma akitoa kichapo hapo ukanda wa Gaza.

Blair ameondoka jamaa yupo. Ule mpango wa raman ya amani sijui uliishia wapi.
 
Ndege Mia moja ziliyeyushwa ndani ya dk 3 tu na misiri akaapa kutofanya vita na Israeli maisha yake yote, unakumbuka
Jamali Abdelnaser Mke wake alikuwa jasusi na alikuwa na asili ya kiisrael

Zile Ndege aina ya Mig za Misri ziliwahiwa zikiwa ziko uwanjani jambo lingine Waarabu huwa hawana siri wanapanga Shambulio lakini Shekheli zinatembea wanapiga simu Israel na kutoa taarifa

Mimi nakumbuka hata Eritrea iliyashinda Majeshi ya Yemen na kuvitwaa Visiwa kwenye Bahari ya Sham

Waarabu wanachoweza kwa ufasaha ni fitna
 
Huyu mbona ana roho mbaya kama ya mwendazake?
Najua hao Hamas ni wakorofi na wao wanaishambulia Israel ila binadamu tunatakiwa kuwa na emphathy.
 
Kwanini wewe usipewe makazi nchi jirani??
Ukiangalia vizuri hawa wanaojiita Wapalestina ni vizazi vya Majeshi ya Salahudin Ayubi aliyeikomboa Jerusalem kwahiyo wamejiita Wapalestina tu i
 
Back
Top Bottom