Isome barua hii ya kushangaza, kuhuzunisha huenda ni ya kwako uliidondosha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Isome barua hii ya kushangaza, kuhuzunisha huenda ni ya kwako uliidondosha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bampami, Mar 16, 2012.

 1. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280

  A SAD LOVE LETTER

  Najua hautamani kusikia lolote kutoka kwangu kwa kuwa sina thamani tena kwako, thamani niliyokuwanayo kabla hujanipatia ujauzito mara mbili zote ukanisihi nitoe. Kwa sababu ninakupenda nilifanya yote unayotaka. Ulipodai kuwa ukitumia kondom hujisikii raha sikuogopa kuibeba mimba ya tatu nilikuambia fanya unavyotaka.
  Nilifanya haya nikiamini kuwa nalinda penzi langu kwako!!!
  Naumia sana leo unaponiita mkimi Malaya!!! Mjinga tena mshamba!! Hakika hujakosea maana nilikuwa Malaya katika chumba chako, chumba ulichonifanya utakavyo tena kila siku, huku jukumu la kukisafisha ukiniachia mimi, kweli nilikuwa mjinga sana kwa kukulilia hata pale ulipokuwa umenikosea waziwazi na nilikuwa mshamba kwa kuwa ni wewe uliyenifundisha kufanya mapenzi kwa kutumia kila kiungo cha mwili wangu.
  Babaa si unajua nilianza uhusiano na wewe maziwa yangu yakiwa wima, mbona leo wanifukuza ukidai kuwa hunitaki kwa kuwa nina maziwa makubwa tena yamelala. Hukumbuki ni wewe uliyeyafanya hivi???
  Unaniita mimi mchafu sasa unasahau kuwa ni wewe u mchafu zaidi yangu, au unasahau jinsi ulivyokuwa mchafu kupitiliza, uchafu wako ulitokana tamaa zako za kimwili tamaa zilizokufanya ulitake penzi langu hata nilipokuwa katika siku zangu!!!!! Hukuwa ukiuona uchafu huu ati leo waniita mchafu!!!
  Wewe una usafi gani???
  Babaa!!! Nakuandikia haya japo utayapuuzia lakini unaujua ukweli kuwa nilikupenda na wala sio kimakosa. Nilifanya yote uliyoyataka lakini hunilipi thamani yangu tena leo hii.
  Unazuga kuwa u wa mjini sana!!! Unasahau kuwa ulikuwa unakosa hata pesa ya nauli nikawa nakupatia akiba yangu ya pesa za pedi nilizokuwa nimepewa na mama. Niliacha kulipa ada yangu nikakupatia pesa umnunulie mama yako dawa alipokuwa anaumwa, sijali sana hata kama ulinidanganya lakini nilifanya kwa mapenzi yangu kutoka moyoni.
  Hivyo visichana vimekudanganyishia hayo mavazi yao kama viko uchi vile, macho yao ya wiziwizi yamekukamata unanisahau unasema ulipitiwa yaani ulinipenda bahati mbaya. Ulinipenda bahati mbaya???? Wakati ulikuwa unanililia, hivi kumbe machozi yako yalikuwa ya kunilaghai nashukuru umefanikiwa.
  Lakini naomba nikwambie kitu kimoja babaangu, ulipoamua kujiingiza katika uhusiano na visichana vyako hivyo nilivumilia lakini siku nilipokufumania na yule rafiki yangu Jane mkifanya ngono makaburini niliumia sana, ni siku hiyo niliamua kujibu maombi ya yule rafiki yako Benard, siku hiyo nililala kwake, nilizini naye kwa hiari kwa lengo la kulipiza kisasi.
  Kisasi kile hakikuyatuliza maumivu yangu, bado ulikuwa una nafaqsi katika moyo wangu!!! Penzi lako halikuwa na mrithi baada ya siku mbili nilipata hamu ya kuwa na wewe nikaja kwako. Tukafanya mapenzi bila hata kukukumbushia juu ya uchafu ulionifanyia.
  Nadhani lilikuwa kosa kubwa, kama ninavyokuabdikia wewe barua hii usiyoipenda na mimi Benard aliniandikia na yeye aliandikiwa na Jane akadhani ni utani kumbe ni kweli tupu. Jane amethirika, amemwambukiza Bernard, Bernad kaniambukiza mimi halafu MIMI na JANE tumekuambukiza wewe.
  Sikupenda iwe hivyo lakini na wewe sikulaumu!!!
  Asante kwa kuisoma barua yangu, sina uhakika na maamuzi utakayochukua.   
 2. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Asee, ingawa imekaa kishigongo shigongo, but nimeipenda.
  By the way sina rafiki anayeitwa Bernard mwenye msichana aitwaye Jane, kwa hiyo barua siyo yangu..!
   
 3. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  :sleepy:
   
 4. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  ndo imefika kwako hivyo
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Ngoja nikamlete muhusika , yupo humu humu jf .
   
 6. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anza kwa kutwambia kuwa wewe sio Bernad lol. .
  Binafsi mi sio Jane! wala sio 'mimi' mtoa story!
  Sina rafiki /ndugu mwenye jina la Bernard nor Jane!
   
 7. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Story nzuri yenye funzo kwa sisi wanaume kuwa tusiwanyanyase wanawake pale tunapoanza kuona matiti yamelala na pia tusiwaite majina mabaya kama vile malaya.
   
 8. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,855
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Dah! Ww ni Shigongo kwa kweli!
   
 9. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kama umepata somo nami pia nimepata somo.
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Siamini katika kifo, naamini katika maisha.
  Silipizi hasira kwa kuua mwingine, hasa napojua nimebeba kifo.

  Mungu aepushie mbali hasira za namna hii.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  K u d da'ada de k
  nimeishiwa maneno !
  Mziki mnene !
   
 12. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  Hongera k kwa kulitambua hili
   
 13. m

  mtukwao2 Senior Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa ila kuna baadhi ya wanawake wanapenda kuitwa majina kama hayo hasa wakiwa kazini japo sijui hasa sababu yake ni nn! VERY TOUCHING TORY
   
 14. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah dunia hadaa na walimwengu ni shujaa
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Du! Ata kidogo hiyo si yangu, si unajuwa naongeza wa pili keshokutwa kuepuka hayo!
   
 16. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Falsafa yangu naamini kuwa Mapenzi yameleta matatizo mengi katika dunia hii. Laiti kusingekuwa na mapenzi ulimwenguni tungeishi kwa amani, upendo na furaha...
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  jamani Bampani mambo yetu ya faragha mbona umekuja kunianika hapa? Hili la HIV usijali we twenzetu tukachukue ushauri nasaha kisha twanze tiba,tutakuwa ok.
   
 18. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kuna kitu kilikuwa kinaniambia haka kabarua kanamshabihi wa nyumbani.Ha..ha..ha Pole kwa hii dhahama.
   
 19. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  No no no bishanga tufe wote
   
 20. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,859
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  Umenena
   
Loading...