Ismail Jussa amtukana Sitta, Nyerere na wa Tz Bara!

Bwana Jussa, hapa hapana! Hakukuwa na lazima ya kumwita Samuel Sitta mjinga ili ufikishe ujumbe wako. Mwisho wa siku, unakuwa mjinga wewe
 
Suluhisho la matatizo ya Muungano ni kuwa na Nchi moja yenye mifuno miwili ya utawala (One country, two systems). Hii ni model ya China, Hong Kong na Macau. Tuwe na nchi moja tu lakini Zanzibar iwe in Special Administrative region, iwe na full autonomy kwa mambo yote isipokuwa Ulinzi (Jeshi) na Mambo ya nje. Waendeshe uchumi wao wenyewe, wawe na Benki kuu yao, immigration yao kila kitu kwa kadri wanavyotaka. Labda hii itawasaidoa kuacha kulalamika lalamika.
Kwahiyo gharama za ulinzi nani atazibeba? kama watachangia watachangia nusu au kwa ratio gani?
 
huwa namuona ni mtu mwenye busara lakini kwa hili aamelikoroga, Jusa ni mpuuzi, hawezi kuwatukana namna hii, ila kwa sababu serikali yetu inavyoendeshwa, angekuwa Lema saizi ungeskia yupo segerea. Pinda kamsikia Jusa au coz ni ccm B
Ulikosea kama ulidhani jusa ana busara. Tafuta kumbukumbu zote zinazomhusu jusa hutapata mahali ametumia busara, huyu ni mpayukaji namba moja wa CUF na kama kuna sehemu wanahitaji mtu wa kupayuka basi hapo cuf watampeleka Jussa na si mwingine. Kwa nchi serious huyo asingepata hata uongozi wa tawi la chama wala ubalozi wa nyumba tano.
 
Suluhisho la matatizo ya Muungano ni kuwa na Nchi moja yenye mifuno miwili ya utawala (One country, two systems). Hii ni model ya China, Hong Kong na Macau. Tuwe na nchi moja tu lakini Zanzibar iwe in Special Administrative region, iwe na full autonomy kwa mambo yote isipokuwa Ulinzi (Jeshi) na Mambo ya nje. Waendeshe uchumi wao wenyewe, wawe na Benki kuu yao, immigration yao kila kitu kwa kadri wanavyotaka. Labda hii itawasaidoa kuacha kulalamika lalamika.
Hata mfumo huo hawataukubali. Maalim Seif, Jussa na Wazanzibar wengi tu wanataka NCHI yao. Mipaka wameichora upya juzi kwenye KATIBA yao. Sijasikia tu wakidai tarehe ya UHURU wa Zanzibar mwaka 1963.
 
Bungeni Lissu alitukanwa na kukashifiwa na wabunge wa Bara na Zanzibar kisa kazungumzia aina ya muungano tunayoitaka. Sasa ukweli unaanza kujithihirisha.
 
Kama
ni hivi,, na Uvunjike (Muungano)... Hatuwezi kuzarauliwa kiasi hiki,, tena mpaka na walowezi!! (Wahindi)!!.... Kisa anazungumza kiswahili!! Enough is enough!!.. What are we benefiting from Zanzibar????
 
Hotuba ya Jussa ni taarabu iliyokosa midundo! Hoja ya dakika tano anatumia zaidi ya nusu saa kupotezea wajinga wenzake muda kwa kuwaweka juani. Anamsifu Karume (wa kwanza) kuwa mzalendo wakati aliwanyima baraza la uwakilishi hadi Nyerere alipolazimisha.

Anasema sasa waunde chombo chao kuchimba mafuta lakini alikuwa wapi kuunda chombo cha kuyatafuta hayo mafuta na je anajua TPDC ilitumia gharama kiasi gani kufanya utafiti?

Anasema waligharamia umeme unaotumika Tanganyika ndio maana wanatumia umeme bure, hii ingekuwa hivyo kila mtu angegharamia kujiunganishia umeme na kisha kutumia bure tu. Au hajui wote huwa tunalipia connection charges na kisha tunalipa bili? Kwa nini alitaka Zanzibar wapelekewe umeme dezo? Kwa kifupi Jussa ni kiazi mviringo tu!
 
Jussa alitakiwa amjibu Sita kwa hoja na wala si kwa matusi kama alivyofanya!!! Jussa kajishushia hadhi sana kisiasa. Kama kweli eneo linalodhaniwa kuwa na mafuta lipo kati ya Tanga na Pemba*(kama alivyotamka Jussa mwenyewe), basi asitegemee mteremko katika suala hili hata kama mafuta yataondolewa katika mambo ya muungano au hata muungano ukifa!!!
MTAZAME HAPO KWENYE VIDEO INAYOPATIKANA KWENYE LINK HAPO CHINI,SIO SIRI AMENIKERA SANA HUYU MHINDI!SAM SIX SI NI SAWA NA BABA YAKE?HAKUKUWA NAHAJA YA KUMTUKANA MZEE HUYO KISA KATOFAUTIANA NAE MAWAZO,HIZI NDIO SIASA ZA MAJI TAKA SASA...

Rashid Video: ISMAIL JUSA ANAMJIBU SAMWEL SITA
 
Hahahahaaa!! Sipati picha Jussa akiingia bungeni! Ana mengi ya kuongea..... Uyu jamaa kama hamujui anajua mambo mengi kushinda uyo Sitta, Amesomeshwa na amesukwa na CUF vizuri tu! Uyu Sitta nae kama hajasoma, Zanzibar inanufaika na umeme kwani mnatupa bure uo umeme? Akh hana hoja kabisa Sitta,,,,, kijasho kilimtoka alivokuja Zanzibar kuskiza maoni naona hajarudi tena mana alikosewa kupigwa!
 
Suluhisho la matatizo ya Muungano ni kuwa na Nchi moja yenye mifuno miwili ya utawala (One country, two systems). Hii ni model ya China, Hong Kong na Macau. Tuwe na nchi moja tu lakini Zanzibar iwe in Special Administrative region, iwe na full autonomy kwa mambo yote isipokuwa Ulinzi (Jeshi) na Mambo ya nje. Waendeshe uchumi wao wenyewe, wawe na Benki kuu yao, immigration yao kila kitu kwa kadri wanavyotaka. Labda hii itawasaidoa kuacha kulalamika lalamika.
Basically, huu unalingana sana na mfumo ambao tunautumia sasa hivi kuendesha Muungano ingawa katika miaka ya hivi karibuni Zanzibatr imekuwa ikijitalia madaraka zaidi kwa kisingizio kwua bara iliongeza articles of union kinyemela
 
TUKUTUKU Znz haitegemei misaada ushaoneshwa vyanzo vya hela vinapatikana wapi, Zanzibar palikua na biashara kubwa sana kuliko Tanganyika. Wafanya biashara waenda kuchukua mchele india na kwengine kufanya biashara tena msaada wa mchele wa kazi gani wakati raia uwezo wanao?
Na Zanzibar yaweza kuwa Dubai ya pili duniani kwanini isiwe? Kilichoinua Dubai ni freeport, na Zanzibar kuna mpango wa kutengeza freeport apo chacha, biashara itazidi kukuwa!!!!
Bagaile mmejiona km ni wachumba tu? Urojo na udwebedo wetu si kwenye Akili,,,, mwala Sembe lkn mambo mdg yanawashinda!!
Alosema jussa ni ukweli, Zanzibar inajitegemea kila kitu! Na saiv kuna majenereta mapya yapo zanzibar, mkizima uku tunawasha wa kwetu, na badooooo, tutafua wa kwetu wenyewe karibuni, uu wa Tanesco ni upuuzi tu ja wizi,,,,
 
Vile vile Maalim ana siri nyingi za muungano na anamuachia mikoba uyo Jussa aje atumbue jipu,,,,, Nyerere alikoma kwa Maalim mpk kaamua kumtia kifungoni,,,,
 
Kichwa cha bahari juu nilitaka kisomeke kama hivi ' Mh. Samwel Sitta utachukuwa hatua gani baada ya kutukanwa kule Zanzibar?'

Mh Samwel Sitta kwanza pole kwa shughuli za Taifa. Watanzania wengi wanakujua hasa kutokana na mchango wako bungeni wakati ulipokuwa Spika wa bunge.

Ulipopata nafasi ya kusimamia shughuli za serikali bunge kwa kukaimu nafasi ya waziri mkuu ulijibu hoja mbali mbali moja ikiwa ya Muungano. Nadhani ulikuwa unafanya hivyo kama kiongozi wa serikali(waziri mkuu) kujibu hoja zinazoelekezwa serikalini kwa kutoa maoni ya serikali. Sasa wengi tumeshangazwa na kauli za matusi zilizotolewa na kiongozi wa CUF(Isimail Jussa) kule Zanzibar dhidi yako.

Tunaomba kusikia kutoka kwako, ni hatua gani utachukua? ama umekubali kuwa wewe ni mjinga na mpumbavu kama ulivyosema Jussa kitu ambacho sisi wananchi wengi hatuamini hivyo. Hatuamini hivyo kwa sababu tunakujua kutokana na uwezo wako na mchango mkubwa wa utumishi katika nafasi mbali mbali za uongozi serikalini na mashirika yake tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere hadi sasa.
 
hivi mtu aliyezima mjadala wa richmond bungeni anastahili kuitwa mpumbavu?iam just asking
 
Hata mfumo huo hawataukubali. Maalim Seif, Jussa na Wazanzibar wengi tu wanataka NCHI yao. Mipaka wameichora upya juzi kwenye KATIBA yao. Sijasikia tu wakidai tarehe ya UHURU wa Zanzibar mwaka 1963.

Mkuu kwenye video hukusikia Jussa akisema Zanzibar ilipopata uhuru ilikuwa na wataalam karibu wote ukilinganisha na Tanganyika ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Mzungu - Mwingereza! Hajasema wakati wa Mapinduzi amesema wakati wa uhuru! anajua anachokifanya haikuwa bahati mbaya!
 
Jussa alitakiwa amjibu Sita kwa hoja na wala si kwa matusi kama alivyofanya!!! Jussa kajishushia hadhi sana kisiasa. Kama kweli eneo linalodhaniwa kuwa na mafuta lipo kati ya Tanga na Pemba*(kama alivyotamka Jussa mwenyewe), basi asitegemee mteremko katika suala hili hata kama mafuta yataondolewa katika mambo ya muungano au hata muungano ukifa!!!

Mkuu wangu mafuta yenyewe huko mpakani yapo kweli? Mafuta yapo Mtwara Mkuu huko Pemba the project is not economically and environmentally viable!
 
Mkuu kwenye video hukusikia Jussa akisema Zanzibar ilipopata uhuru ilikuwa na wataalam karibu wote ukilinganisha na Tanganyika ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Mzungu - Mwingereza! Hajasema wakati wa Mapinduzi amesema wakati wa uhuru! anajua anachokifanya haikuwa bahati mbaya!
Wazanzibar wa MAPINDUZI DAIMA wamemalizika nini! Najua wanaumia kwa ndani kuiona SMZ yao imehamia PEMBA.
 
Makao makuu ya muungano yapo Dar na bungeni kule Dom. Wazanzibari fanyeni hima fungasheni muondoke! Mnasubiri nini? Mnalia jicho moja na jingine likicheka. wanafiki wakubwa
 
hivi mtu aliyezima mjadala wa richmond bungeni anastahili kuitwa mpumbavu?iam just asking

Na mimi niulize, hivi context ya Jussa kumwita Sitta "mpumbavu" ilikuwa mjadala wa Richmond?

Tukiamua kuchunguza ni lini fulani aliwahi kufanya jambo la kipumbavu katika maisha yake kama hoja ya yeye kuwa mpumbavu kwa wakati uliopo au jambo tofauti linalozungumziwa kwa wakati uliopo basi hakuna asiye mpumbavu asilani! Kwa mtazamo huo kila mtu ni mpumbavu.
 
Back
Top Bottom