Ismail Jussa amtukana Sitta, Nyerere na wa Tz Bara!

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2][/h]


Na Charles Mwankenja



12th July 2011



[FONT=ArialMT, sans-serif]Chama cha Wananchi (CUF) kimezidi kuelekeza makombora kwa viongozi wandamizi serikalini wanaopinga kuwepo kwa serikali tatu katika sura ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ijumaa iliyopita, wakati anajibu hoja za Wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais mjini Dodoma, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema kufufua serikali ya Tanganyika ni sawa na kutengeneza mpinzani wa Zanzibar.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sitta ambaye alikuwa Kaimu Kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni, pia alisema Muungano wa serikali mbili una manufaa zaidi kwa upande wa Zanzibar, ambao unabebwa kutokana na uwezo wake mdogo wa kuchangia gharama za huduma, kama vile za umeme na uanachama katika Muungano.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Bububu, mjini hapa, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, alisema kupingwa kwa Muungano wenye sura ya serikali tatu kutonatokana na hofu ya muda mrefu ya Tanzania Bara kupoteza fursa ya kunufaika, kiuchumi kupitia mgongo wa Zanzibar.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jussa alisema Muungano wenye sura mbili unainufaisha zaidi Tanzania Bara kutokana na mfuko wa serikali ya Muungano ambao uendeshaji wake unakosa uwiano katika suala la mgawanyo wa fedha kati ya pande hizo mbili za Muungano.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Vifungu vinavyoongoza matumizi ya fedha kutokana na mfumo huo, vinapaswa kueleza kiasi gani ni kwa ajili ya Tanganyika na kipi kinaenda Zanzibar… matumizi ya mfuko hayana maslahi kwa Zanzibar,” alisema Jussa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Zanzibar haiwezi kufurahia sura ya Muungano wa serikali mbili kwa sababu inanyonywa na Tanzania Bara na ndio maana viongozi, kama Waziri Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hawataki serikali tatu.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Ukiwa na serikali mbili, mapato yote ya serikali ya Muungano yanabaki Tanzania Bara, zikiwa tatu yatakwenda kwa serikali ya Muungano, ya Tanganyika na ya Zanzibar kwa uwiano unaoeleweka,” alisema Jussa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema maelezo ya Waziri Sitta dhidi ya Zanzibar ndani ya Bunge la Muungano ya kutumia vitu na huduma za umeme kwa wananchi wa pande hizi mbili, ni ishara ya nia mbaya ya Tanzania bara kwa Zanzibar.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Sitta asitulaghai kwamba chini ya muundo wa serikali tatu, Tanganyika ingechoka kuibeba Zanzibar na Muungano ungevunjika, Zanzibar hatupewi bure umeme, tunanunua, sawa na Kenya na Uganda wanavyouziana huduma hiyo,” alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema ujenzi wa miundombinu ya umeme unaotumika visiwani kutoka Ras Kilomoni uligharamiwa na serikali ya Zanzibar. “Badala ya kutusimangwa, Zanzibar tulipaswa kulipwa faida kwa kuwekeza katika umeme huo.”[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kauli yake Bungeni Dodoma, Waziri Sitta pia alisema Muungano wa serikali mbili ulipata baraka zote za Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume na kwamba katika hatua fulani, Rais huyo wa kwanza wa Zanzibar aliwahi hata kupendekeza kuundwa kwa serikali moja.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Juu ya mchakato Katiba mpya, Jussa alisema Serikali ya Mapinduzi yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, imesimama imara kuhakikisha muswada wa mapitio ya Katiba mpya unapelekwa bungeni ukiwa umelinda maslahi yote ya wananchi wa Zanzibar yaliyomo katika Muungano.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 

Attachments

  • Sita(4).jpg
    Sita(4).jpg
    14.5 KB · Views: 134
Ni CCM tu ndiyo inayoulinda muungano usiyokuwa na tija,kwa kuwa CCM siku zake zinahesabika basi na muungano pia siku zake zinahesabika.Wanzabari ni watu wanaoamini maendeleo watayapata kwa njia ya misaada,na ndiyo maana wanajitahidi wajitenge ili wapatate misaada ya kutosha ikiwemo michele kutoka Oman na nyama kutoka saud Arabia.Lakini nachojua ni kuwa hakuna nchi iliyoendelea au itakayoendelea kwa kutegemea misaada,lazima watu wafanye kazi kwa juhudi na ndipo maendeleo yatapatikana.Hivyo basi,sioni haja ya kuendelea kuungana nawatu wenye fikra kama hizi!!
 
Huenda anachosema Jusa Radhu kuhusu umeme kina ukweli, maana pamoja na Mgao huu wa giza wa masaa 18 huku bara, kule Zanzibar umeme huwa unakatika kwa muda wa Lisaa limoja tu. ( Yaani ukikatika saa nne asubuhi unarudi siku hiyo hiyo saa tanon asubuhi) Nimeshuhudia mwenyewe.

Viongozi wa Chama Marehemu Mtarajiwa ndio waliotuuza kwa hawa Wajinga. Halafu sisi huku tunajiona Wajaanjaa!! Kumbe mbele ya Wapemba, Sisi ni Wachumba tu.
 
Ni CCM tu ndiyo inayoulinda muungano usiyokuwa na tija,kwa kuwa CCM siku zake zinahesabika basi na muungano pia siku zake zinahesabika.Wanzabari ni watu wanaoamini maendeleo watayapata kwa njia ya misaada,na ndiyo maana wanajitahidi wajitenge ili wapatate misaada ya kutosha ikiwemo michele kutoka Oman na nyama kutoka saud Arabia.Lakini nachojua ni kuwa hakuna nchi iliyoendelea au itakayoendelea kwa kutegemea misaada,lazima watu wafanye kazi kwa juhudi na ndipo maendeleo yatapatikana.Hivyo basi,sioni haja ya kuendelea kuungana nawatu wenye fikra kama hizi!!
kwani comoro na kwenyewe kuna Muungano, mbona bado na penyewe naona life lao halipo juu kihivyo! Sawa sawa na Zanzibar wanavyotaka kutuaminisha kwamba muungano ukivunjika basi Zanzibar inaweza ikawa kama Dubai!
 
Jussa nae ni mwanasheria anajua vyema anachozungumza.lakini Lugha anayotumia si ya kiungwana hata kidogo,anakosa heshima na anachochea uasi!Inapaswa aongozwe na kujua jinsi ya kuheshimu watu

.Masuala ya Uongozi hakuyaanza yeye,anapaswa kuwa diplomat kidogo.Hizi Jazba na ubabe hautosaidia kitu!.........Ndio maana inafika wakati watanganyika wanaona hakuna sababu ya kung'ang'ania Muungano ni vyema sasa kwenda solo.

Haya masuala ya kutukanana "Nani kambeba nani siyo ya kistaarabu hata kidogo"!
 
Jussa nae ni mwanasheria anajua vyema anachozungumza.lakini Lugha anayotumia si ya kiungwana hata kidogo,anakosa heshima na anachochea uasi!Inapaswa aongozwe na kujua jinsi ya kuheshimu watu.Masuala ya Uongozi hakuyaanza yeye,anapaswa kuwa diplomat kidogo.Hizi Jazba na ubabe hautosaidia kitu!.........Ndio maana inafika wakati watanganyika wanaona hakuna sababu ya kung'ang'ania Muungano ni vyema sasa kwenda solo.Haya masuala ya kutukanana "Nani kambeba nani siyo ya kistaarabu hata kidogo"!


Hata kama mtu amesoma kwa kiwango cha Ph.D lakini akikubali kujulikana bei yake hapo anakuwa ni sawa na bure, shule inakuwa haijamkomboa.

Ili kuepukana na haya mashambulizi, dhihaka, malalamiko na shutuma za kila siku ni wakati muafaka sasa tuvunje muungano ili kila nchi iendelee na hamsini zake.

Hawa wala urojo kila siku ni kebehi na dharau kwa watanganyika wakati sisi ndio tunawapa platform ya unafuu wa maisha.
 
Back
Top Bottom