Isingekuwa Ubunge, Halima na wenzake 18 waliofutwa uanachama CHADEMA wangehamia CCM leo Aprili 30, 2021

Watasamehewa na watagombea tena ubunge ndani ya CDM.
Siasa zetu ni hizihizi na watu ni walewale.
Muda utaongea tu.
Kama wangekuwa na akili, walitakiwa waachane na ubunge wa CHACHANDU wakaombe msamaha Chadema. Wangeweza rudishwa tena kwa tiketi cha Chadema.
 
Pamoja na kuwa Ndugai kawahakikishia kuwa atawalinda lkn ukiwaangalia machoni hawana amani kabisa mioyoni mwao, kwa vile ni vigumu kwao kurudi Chadema wanatamani aidha waache ubunge wawe raia wa kawaida au wajiunge CCM.

Tatizo kubwa linalowasumbua vichwani ni kupoteza ubunge wao, kungekuwa na kanuni kwamba unaweza kuhama chama lkn ukabaki na ubunge wako siku nyingi wangeshahamia CCM na leo wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wa dharura wangepokewa CCM pamoja na Nyalandu.
Mateso wanayo yapata ni heri ukahukumiwa jela miezi sita
 
Lissu yupi? Hvi Lissu angehamia CCM unadhani asingekua waziri wa sheria kma kina Silinde au Waitara? Ndio aje kusettle kwa ajili ya viti maalum?

Mkuu watu wame sacrifice vitu vingi kubaki upinzani.... Hasara alizopewa Mbowe hta Sugu mpaka hoteli manusura ivunjwe ndio sembuse wajitoe ufahamu kisa kiti cha ubunge?

Tatizo lenu mnadhani CHADEMA ni kama ACT au NCCR...... Kma wangeendekeza njaa hiki chama kingeshakufa toka 2013
Umenikumbusha maneno ya nyoodo ya Wasira eti cdm ingekufa kabla ya mwaka 2014.

Sasa hivi kaisha yeye kisiasa .
 
Hao Covid hata kama sio wote basi baadhi yao naamini kuna watakao kimbilia CCM. Samia alisema kuna wengine wanafuata baada ya Nyalandu.
Hao covid inatakiwa washitakiwe kwa kufisadi fedha za umma.
Wanalipwa mshahara wasiyo stahiki.
 
Mnawaza Siasa wenzenu wanawaza Maisha.
Mafanikio ya Kimaisha.
Hiyo ndiyo tabia ya wasaliti hata Yuda kipindi anamsaliti yesu kristu alikuwa anawaza vipande vya fedha.

Wakati wenzake walikuwa wanawaza kupata uokovu.
 
Kinyume chake mkuu, Mama ni muumini wa siasa shirikishi za kistaarabu na jana katamka hilo.Salama yao hao covd19 ni kuomba radhi na kumtupia lawama hayati kuwarubuni, kisha maisha yanasonga nyumbani CDM.
Pamoja na kuomba radhi lkn siamini kama wana cdm wapo tayari kuwasamehe hao mbwamwitu
 
Sisi tulishamaliza kazi,yeyote atakayekuwa na nia ya kuihujumu Chadema hatadumu. Hatuandikii mate.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom