Isidingo la Gesi: Tuijue gharama ya Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dar es salaam

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,379
3,882
Tuijue gharama ya Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dar es salaam. Tukimaliza hapo, tuanze kuelewa kwanini Gesi tunaipeleka Kenya.

Gharama za mradi ni Dola za Marekani 1,225,327,000 (Bilion 1.2)Kati ya
fedha hizo Benki ya Exim ya China imechangia asilimia 95 na Serikali ya
Tanzania asilimia 5. Kiasi hicho cha fedha kinatumika kugharamia
maeneo yafuatayo:
a) Mtambo wa kusafisha gesi asilia wa Songo Songo Dola za
Marekani 151,735,000; (Usd 151.7 mln)
b) Mtambo wa Kusafisha gesi asilia wa Mnazi Bay Dola za
Marekani 197,877,000;(Usd 197.877mln)
c) Bomba la kusafirisha gesi asilia Dola za Marekani
875,715,000 (Usd 875.715 mln).

Kwa maana hiyo gesi ya Mtwara inamilikwa na Watanzania kwa 5% pekee. Tutafute mkataba huu wa mradi wa Gesi ili tujue ni nini kilisainiwa.

Ukweli huu hapa unaohusu mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara _ Dar es salaam.

👉Mitambo ya Gesi Madimba na SongoSongo
Moja ya mitambo ya kuchakata gesi nchini umejengwa eneo la Madimba mkoani Mtwara na kampuni za China Petroleum Engineers, China Chemical Engineering Secondary Construction Corporation na Worley Parson. Mtambo mwingine wa gesi ulijengwa kisiwani SongoSongo na unamilikiwa na kampuni ya SONGAS Ltd; kampuni ya ubia kati ya CDC Globeleq, Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na TDFL.

Makubaliano ya Ujenzi kati ya Tanzania na China.

Mwezi Septemba 2012, Wizara ya Fedha kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Exim ya China walitiana saini makubaliano ya mkopo wa miaka 33 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.225 kwa riba ya asilimia 2 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi linalounganisha eneo la Msimbati na Mnazi Bay mpaka Dar es Salaam. Kampuni zilizosimamia ujenzi huu ni China Petroleum Technology and Development Corporation (CPTDC) na China Petroleum Pipeline Engineering Corporation (CPPEC).

Gharama za ujenzi wa Bomba la Gesi kuja Dar es salaam ilikuwa ni uamuzi wa Wakopeshaji ambao ni Benki ya Exim ya China. Uamuzi huo ilikuwa ni kuweka Gesi katika maeneo jirani ya Bagamoyo ili kuwa karibu na mradi ambao ulikuwa ukisubiriwa kufanyiwa mapitio ya mwisho ya Uwekezaji wa Mradi wa EPZ. Harakaharaka iliyokuwepo ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi Dar es salaam haikuwa ya bahati mbaya na wala msingi wake haukuwa ni kutengeneza mkoa wa Viwanda.

Kuna mtu atasema msingi wa usafirishaji wa gesi ilikuwa kuchochea kasi ya Uwekezaji wa Viwanda katika mkoa wa Pwani. Si kweli bali ilikuwa kuiweka karibu na maeneo ya kusafirisha gesi hiyo. Kama issue ilikuwa kuchochea ujenzi wa Viwanda, kwanini isifanyike mkoa wa Mtwara, kwani Mtwara haifai kujengwa Viwanda? Je hadi Sasa takwimu za viwanda vinavyotumia Gesi ni vingapi mkoani Pwani? Hapa ndo pakuhoji.

Mradi huu ulikuwa kwa ajili ya kuuza Gesi yetu nje ili kufidia gharama za mkopo, maana yake ilikuwa ni lazima tuiuze haraka ili kufidia deni la uwekezaji wa 95% ya benki ya Exim ya China. Usishangae kwa nini tunaipeleka gesi Kenya. Gesi ya Mtwara sio ya Mtanzania, hili lieleweke kwa sasa, Gesi hii itakuwa yetu baada ya deni kuisha. Juzi Mama "amesinya" kule Kenya, automatically Gesi inapitia Bagamoyo pale kwenye ule mradi wa EPZ na hapo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo utaanza "upyaaaaa" hata kabla bomba halijafika Kenya. Keep this post.

Hebu rejea hapa;

Kupatikana kwa gesi asilia kule Mtwara kulishabikiwa na watawala wetu ikiwa ni pamoja na mataifa makubwa kama vile Marekani na China. Mpaka watu wengi hasa watanzania wa kawaida wakadhani kwamba labda sisi ni nchi pekee duniani tuliokuwa na mali ghafi hiyo muhimu kwa uchumi na maendeleo. Ki_ ukweli ni kwamba kulingana utafiti uliofanywa shirika la mafuta la Uingereza BP wa mwaka 2009 (The World Factbook Based on BP Data - 2009) ulionyesha kwamba gesi asilia ipo katika nchi 102 duniani kote na Tanzania inashika nafasi ya 83 kwa kuwa na kiasi cha gesi kinachokadiriwa kuwa ni 6,513,000,000 m³ (Mita za Ujazo 6,513,000,000)! Marekani ni ya 5 kwa kuwa na gesi kiasi cha 8,500,000,000,000 m³; China ni ya 12 kwa kuwa na gesi 3,100,000,000,000 m³; Rwanda ni ya 63 kwa kuwa na kiasi cha 56,630,000,000 m³ ambayo ni nchi jirani na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sasa tujiulize kwamba ni kwanini Wamarekani na Wachina waishabikie gesi yetu kama vile huko kwao haipo au kama vile ni sisi tu barani Afrika ndio wenye rasimali hiyo muhimu? Ni tabia ya kila mfanyibiashara anapenda kununua bidhaa kwa bei ya bure na aiuze kwa faida kubwa iwezekanavyo. Hivyo ni wazi kwamba Wamarekani na Wachina wanajua kwamba pamoja na kwamba gesi hii inapatikana katika nchi 102 duniani zikiwemo nchi 22 za Kiafrika, lakini Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo inasifika duniani kwa kusaini mikataba ya kifisadi ndiyo maana kila muwekezaji asiyependa uwazi anakimbilia hapa Tanzania.

Halafu gesi yetu siyo nyingi sana kama nchi zingine za Kiafrika kwa vile kwenye orodha ya nchi za Kiafrika 22 sisi tunashika nafasi ya 17 mbele ya Somalia, Morocco, Benin, DRC na Afrika ya Kusini.

Mawazo yangu Mlalahoi/Mganga njaa.

Tanzania inatumia pesa nyingi sana za kigeni kila mwaka kununua mafuta ambazo ni karibu 55% ya pesa zote za kigeni zinazozalishwa na Serikali. Gesi inaweza kubadilishwa ikawa mafuta ya maji (Petrol, diesel, paraffin) na nchi yenye technolojia hii duniani kote ni kampuni moja tu toka Afrika ya Kusini Sasol Company (Sasol has a technology of gas to oil); hivyo mimi nilikuwa napendekeza kwamba gesi asilia ya Mtwara ni kwanini Serikali isiingie mkataba na Sasol ili tuibadilishe gesi hiyo na kuwa mafuta ambayo yangeweza kulipunguzia taifa mzigo mkubwa wa kutumia pesa za kigeni kwa kuyanunua mafuta hayo kila mwaka?

Kampuni hii imeingia mikataba na nchi zisizopungua 20 duniani ambazo zina gesi na kampuni hii inabadilisha gesi hiyo na kuwa mafuta jambo ambalo limepunguza umasikini katika nchi hizo zikiwepo Amerika, Kazakhstan, Malaysia, Msumbiji, China na nyinginezo.
 
Ndiyo maana mzee mpaka anaondoka hapa duniani, hakuwahi kuwaletea ubabe mabeberu wa gesi. Alishajua fika mkwere alishafanya ya kwake.

Nakumbuka kipindi kile sheria ya gesi ilipitishwa kwa hati ya dharura kule bungeni. Na hata wapinzani walipohoji, waliishia tu kupuuzwa na kukejeliwa! Yako wapi sasa!!
 
^Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo inasifika duniani kwa kusaini mikataba ya kifisadi ndiyo maana kila mwekezaji asiyependa uwazi anakimbilia hapa Tanzania.^

#^Anayeweza kukubali mkataba wa hovyo kiasi hicho ni kichaa tu^ ~ ilisikika sauti ya mzalendo wa kweli.
 
Zamani nilikuwa nawaona waasi kama wehu vile ila kwa ujinga huu wa CCM kuna kila sababu ya TAnzania kuwa na vikundi vya waasi!
gesi mtwara.jpg
 
Mkuu, Mungu akubariki Kwa upendo wako huu, hapa nimekuelewa vema, Na kiukweli unahoja fikirishi na yenye mashiko

Mimi huwa najiulizaga siku zote, hivi Kwa nini watu waungwana huwa hawadumu,????

Si ajabu kuna mtu ataanza kuona haufai kuyasema haya hadharani na akaingiwa tu na roho ya kishetwani ya kuangamiza Kwa wema wako huu, Mungu akulinde
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom