Ishu ya mafuta; baadhi ya wabunge wana hoja nyepesi sana! Sisi Watanzania siyo wajinga!

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wadau poleni kwa kazi. Nijikite kwenye mada yangu kuhusu matamko ya baadhi ya wawakilishi wetu bungeni (narudia tena ni baadhi).

Hivi karibuni, Mbunge wa Gairo, mheshimiwa Ahmed Shabiby alitoa hoja kuntu kabisa kwamba, ili kupunguza kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta nchini, muarobaini wake ni serikali iruhusu wafanyabiashara binafsi nao waagize mafuta hayo.

Wadau mbalimbali waliibuka, wengine kumpongeza wengine kumpinga Ahmed Shabiby.

Miongoni mwa waliyokwenda naye kinyume ni mheshimiwa mbunge Shangazi. Yeye amesema kuwa, serikali ikiruhusu wafanyabiashara binafsi kuingiza mafuta, itakosa 'stoku'.

Wadau wengine walisema wafanyabiashara binafsi wakiachiwa kuagiza mafuta, wataingiza mafuta mabovu, yaani yatachakachuliwa.

Wengine wamesema, wafanyabiashara binafsi wakiruhusiwa kuingiza mafuta, kutaibuka ufisadi!!

Kwa ujumla wao wametaka mafuta yaendelee kuingizwa nchini kupitia utaratibu wa bulk procurement. Serikali iagize na kuwauzia wafanyabiashara.

Lakini Shabiby alisema kuwa, bulk procurement iendelee na wafanyabiashara binafsi wawepo. Atakayeona bulk procurement inafaa, aingie huko, atakayeona kwa wafanyabiashara kunafaa sawa pia. Ili mradi serikali ipate kodi yake.

Madai ya mbunge Shangazi kuwa, serikali itakosa 'stoku' ni ya kufikirisha sana. Serikali itakosaje 'stoku' wakati na yenyewe itaendelea kuagiza?

Kuhusu kuingizwa mafuta mabovu nchini, itawezekanaje wakati sehemu ya kushushia mafuta ni moja, kwenye mita ambapo kuna vipimo vya serikali vya kuangalia ubora wa mafuta?!

Kuhusu kuibuka ufisadi, kivipi? Mamlaka ya kusimamia mafuta, Ewura ipo. Ufisadi utatokea wapi? Na kwa njia gani?

Ushauri wangu kwa waheshimiwa wabunge, akiwemo Shangazi, waungane kumuunga mkono mtoa ushauri, Shabiby ili kuangalia hali itakavyokuwa. Kukataa bila kujaribu ni kuogopa mabadiliko.

Wafanyabiashara binafsi wakiruhusiwa wanaweza kuagiza mafuta toka kokote wawezavyo. Na wanaweza wanachotaka ni kibali tu au niseme ruhusa.

Wapo watu wanadai mheshimiwa Shangazi na mheshimiwa mwenzake mmoja kutoka mkoani Kagera waliwahi kufanyakazi kwenye kampuni moja ya mafuta nchini. Kwa hiyo, hoja zao nyingi ni kutetea maslahi. Kama ni kweli, mabadiliko ni muhimu.

Watanzania wa leo siyo wajinga. Wanajua kila hoja inayotolewa inatoka kwa ajili gani. Kama ni maslahi binafsi wanajua, kama kuwatetea wao Watanzania pia wanajua.
 
Back
Top Bottom