Ishi ndoto yako

Geneous99

Member
Aug 31, 2019
16
24
Toka miaka ya tisini na pengine miaka ya ya sitini mpaka themanini, ahadi zilikuwa nyingi sana, ndoto kwa vijana zikawa nyingi Sana, watu wakawa na matarajio makubwa, na pengine wakatamani wayaishi matarajio hayo na ndoto zao.

Walitamani maisha mazuri, maisha ya amani, lakini sio amani tu, amani yenye utulivu na furaha ndani ya mioyo yao. Walihitaji barabara nzuri, wakahitaji maji safi na salama, umeme kila kijiji, shule na vyuo vyenye mazingira mazuri ya kujifunzia, chakula na makazi na pengine maisha bora yenye sera nzuri za elimu, ajira serikalini na viwandani, hakika walikuwa na matarajio makubwa.

Hawakuyaishi hayo, barabara zikawa mbovu zaidi, njaa ikazidi, ajira zikapoteana siku zikasogea na ndoto hazikutimia. Mwalimu akaona ni vyema, vyama vingi kipindi hicho, vikiwa haviko kwenye mioyo yawatanzania, akavianzisha. Miaka iliposogea, chama kimoja kikazidi kutawala, ahadi za miaka ile zikazidi jirudia, lakini bado ndoto na matarajio hayakutimia.

Pengine ni kwa sababu ya ubovu wa katiba iliyokuwa imejichokea na mifumo mibaya nchi iliyokuwa imejiwekea. Sasa watu wanahitaji katiba na mifumo thabiti ya kiutawala, yenye tume huru ya uchaguzi, yenye mifumo thabiti na imara ya kudhibiti matumizi mabaya ya nguvu za dola, uimara wa makakama, na kujitegemea kwa kila muhimiri wa serikali.

Katika jamii moja yenye utawala mbovu, siku ya uchaguzi ikawadia, kampeni, vyama vikajipigia, kwa miaka hamsini chama tawala kilijitawalia, mjukuu akamwambia Bibi, twende tukapige kura, Bibi akamwambia, miaka hamsini yote niliyopiga kura bado maisha ni yaleyale, umesoma mpaka chuo kikuu na ajira haujapata, chakula bado cha shida, ona sasa hata maji ya kunywa hamna, nimeenda hospital nimepewa panado tu, siwezi kupiga kura mie.

Mjukuu akamsisitiza, kuwa sasa ni muda umewadia, ajira nitajipatia, maji yatajitiririkia, mahospitalini dawa zitajimwagikia, ni muda wa kubadilisha mfumo. Mjukuu akawachukua mama na Bibi yake , kwenye uchaguzi wakaelekea. Msitari wakajipangia, walikuwa wa mwisho kupiga kura mida ya jioni kabisa, Kwenye sanduku la kupigia kura, kura yao wakaitumbukiza.

Baada ya matokeo kutangazwa, chama tawala kikajishindwa, huku machozi yakiwatiririka kea furaha, chama pinzani kikashika dola. Ukawa mwanzo wa mabadiliko, thamani ya kura moja ya bibi ikaleta tumaini jipya. Barabara zikajengwa, maji safi na salama yakapatikana, maisha bora yakaanza, ajira zikamwagika.

Watu wote wakafaidika, wakaanza kushi ndoto na matarajio yao, usiidharau kura yako moja kwani inaweza kubadilisha matukio. Usiache kupiga kura, kura yako ndio italeta mabadiliko katika jamii yako, Kama wakemia wanavyosema, even a single drop can change the result.
 
Toka miaka ya tisini na pengine miaka ya ya sitini mpaka themanini, ahadi zilikuwa nyingi Sana, ndoto kwa vijana zikawa nyingi Sana, watu wakawa na matarajio makubwa, na pengine wakatamani wayaishi matarajio hayo na ndoto zao. Walitamani maisha mazuri, maisha ya amani, lakini sio amani tu, amani yenye utulivu na furaha ndani ya mioyo yao.

Walihitaji barabara nzuri, wakahitaji maji safi na salama, umeme kila kijiji, shule na vyuo vyenye mazingira mazuri ya kujifunzia, chakula na makazi na pengine maisha bora yenye sera nzuri za elimu, ajira Serikalini na viwandani, hakika walikuwa na matarajio makubwa.

Hawakuyaishi hayo, barabara zikawa mbovu zaidi, njaa ikazidi, ajira zikapoteana siku zikasogea na ndoto hazikutimia. Mwalimu akaona ni vyema, vyama vingi kipindi hicho, vikiwa haviko kwenye moyo wa watanzania, akavianzisha.

Miaka iliposogea, chama kimoja kikazidi kutawala, ahadi za miaka ile zikazidi jirudia, lakini bado ndoto na matarajio hayakutimia. Pengine ni kwa sababu ya ubovu wa katiba iliyokuwa imejichokea na mifumo mibaya nchi iliyokuwa imejiwekea.

Sasa watu wanahitaji katiba na mifumo thabiti ya kiutawala, yenye tume huru ya uchaguzi, yenye mifumo thabiti na imara ya kudhibiti matumizi mabaya ya nguvu za dola, uimara wa makakama, na kujitegemea kwa kila muhimiri wa Serikali.

Katika jamii moja yenye utawala mbovu, siku ya uchaguzi ikawadia, kampeni, vyama vikajipigia, kwa miaka hamsini chama tawala kilijitawalia, mjukuu akamwambia Bibi, twende tukapige kura, Bibi akamwambia, miaka hamsini yote niliyopiga kura bado maisha ni yaleyale, siwezi kupiga kura mie.

Mjukuu akamsisitiza, kuwa sasa ni muda umewadia, wa kubadilisha mfumo, mjukuu akawachukua mama na Bibi yake , kwenye uchaguzi wakaelekea.

Kwenye sanduku la kupigia kura, kura yao wakaitumbukiza. Baada ya matokeo kutangazwa, chama tawala kikajishindwia, chama pinzani kikashika dola.

Ukawa mwanzo wa mabadiliko, thamani ya kura moja ya bibi ikaleta tumaini jipya. Barabara zikajengwa, maji safi na salama yakapatikana, maisha bora yakaanza, ajira zikamwagika.

Watu wote wakafaidika, wakaanza kushi ndoto na matarajio yao, usiidharau kura yako moja kwani inaweza kubadilisha matukio.
 
Back
Top Bottom