Ishi misingi yako na elewa tabia zako kupata mwenza sahihi.

padlock

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
328
496
Wengi wamekuwa wakihangaika kupata mtu sahihi ktk maisha yake wengine kudiriki kukesha kuomba na kufunga kupata mtu sahihi wakitegemea mtu huyo atakuja tu ktk maono kama zilizvyo njozi zingine za kiroho.

Ukweli mchungu ni kuwa upendo haushushwi kutoka mbiguni bali hujengwa kupitia sisi wenyewe wanadamu. Upendo huwa kwa mtu unayempenda na hubadilika kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Ukiishi kwa kutambua misingi yako ni ipi ktk maisha yako huwezi taabika upata mwenza sahihi wa maisha na zaidi ukielewa tabia zako ni zipi huwezi kupata shida wapi pa kuweka moyo wako.

Watu wengine wamekuwa wakifoji mahusiano, wengi zaidi wamekwenda mbali na kulazimisha mazingira ya upendo yawepo baina yake na mtu ampendaye ilihali sio pea yake, sio msingi wake na sio wa tabia zake. Kitu hiki kimeleta mwendelezo wa migogoro mingi sana ktk maisha ya ndoa na mahusiano kiujumla.

Msingi mkuu wa upendo ni uhuru wa kuamua, kuelewa na kupenda, upendo haulazimshwi, upendo hauombwi wala upendo hauamuliwi kuwa mpende huyu usimpende yule bali huja huru, huamua huru na huwa tendo lililo Automatically kutoka kwa mtu.

Unaweza ukajiuliza kwanini fulani alikuwa ananiona sana lakini sasa hivi ndio ananipenda sana, je kwanini isiwe tangu zamani? La hasha si kwa sababu ya vitu unavyofanya sasa bali ni kutoka kwenye "EMOTIONAL LOVE MAP ILIYO KTK FIKRA ZAKE" ndizo zimepelekea yeye kuwa na upendo kwako kwa sasa. Unaweza kuwa unayoyafanya sasa ni sawa na ya Zamani tu ila hayakugusa hisia zake kwa muda huo though yaezekana yalikuwa mazuri tu na wakati unayafanya hukufanya kwa nia yakutaka akupende (hukulazimsha mazingira).

kwa hiyo ukiishi ktk misingi yako, na kuelewa tabia zako huwezi sononeka au hangaika kupata mwenza sahihi wa maisha yako, kila nyota ina nyota yake pacha, wadada wengi walokole (MTANISAMEHE) huwa na dhahania kuwa kupitia maombi watapata wenza sahihi wa maisha yao, La hasha bali omba kwa mambo mengine si la kupata mwenza. Jukumu La mwenyezi Mungu ni kukusaidia pale unaposhindwa si kukuamulia pale unapoweza kuamua.

Embu jiulize kwa akili ya kawaida tu kuwa una akili, una vigezo vyako tiyari ktk kumpenda mtu na una tabia zako pia ambazo unaelewa kuwa mie nkiwa na wa dezaini hii hatuwezi kuendana, Je kwanin Mwenyezi Mungu aingilie katikati y vigezo vyako wakati tayari ulishajiamulia tangu mwanzo ktk fikra zako????

Hakuna mume anayeshushwa kutoka mbinguni au mke kutoka mbinguni wote unawapata na kuwaacha hapahapa duniani, so ni vema ukielekeza nguvu na nia ya kujitambua zaidi ktk kuelewa misngi na Tabia zako ili upate kuchagua mtu sahihi wa maisha yako ( hasa yule ambaye unaweza kuvumilia mapungufu yake yanayoendana na yako pia).
 
Back
Top Bottom