Ishara za kupokwa nchi ya TZ na mafisadi ni Dhahiri

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
278
Ninaongea kwa Masikitiko makubwa kama mtanzania mwenye matumaini ya kuona siku moja Mungu anatuinulia kiongozi mwenye kusimamia kwa dhati maslahi ya watanzania maskini ambao ndio wengi.

Ishara zinaanza kuonyesha kwamba Ngwe ya mwisho ya JK itatawaliwa na genge la Majeruhi wa tuhuma za ufisadi wa , Richmond, Meremeta,EPA na Rada ambao watajitahidi kurusha karata yao ya mwisho kwa lengo la kujisafisha.

Usafi wanaoutafuta watu hawa ni wa kuwapatia qualification ya kuwania nafasi kubwa serikalini kama urais na uwaziri mkuu.

Swali ninalouliza ni kwamba wanatafuta vyeo hivi kwa maslahi ya nani?. Nina waonea huruma watanzania wenzangu ambao wamekuwa wagumu kuelimika kwenye suala la kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Mabadiliko ambayo ili yatokee lazima tuamue kuacha mazoea ya kukichagua chama ambacho lengo lake si la kuwaletea watanzania maendeleo bali kujineemesha kwa kodi za maskini wa nchi hii.

Watanzania walio wengi wamekuwa ADDICTED kwa CCM na kama ilivyo ngumu kwa core drinkers and smokers kuacha hivi vitu ndivyo na kwa wengi ilivyo ngumu kuacha kuchagua CCM. Kama ilivyo kwa sigara na pombe CCM imekuwa ikiwapa rizimu watu wengi kiasi kwamba wanalewa na U-CCM. Nasema wanalewa kwa sababu wengi wao akiwemo mama yangu ukiwauliza kwa nini unakipigia kura CCM anatoa majibu kwa njia ya swali" Kwani CCM imekukosea nini jamani?" au hiki chama ndicho kilichotufikisha hapa.

Ishara tunazoziona za akina Chenge kutaka kwa nguvu kugombea Uspika na hapo hapo KUSAFISHWA NA TAKUKURU ni dalili kwamba tuendako kama nchi ni kubaya zaidi kuliko tulikotoka.

Hii itafuatiliwa kwa karibu na mzee wa Monduli naye kujisafisha na hatimaye kupata hati safi itakayo mpa sifa ya kugombe urais 2015.

Ishara hizi zinaonyesha kwamba bado mafisadi wanatumia nguvu ya fedha walizopata kifisadi kutaka kuendeleza wimbi la kuwapora watanzania maliasili zao kwa manufaa binafsi.

NINATOA WITO KWA VIONGOZI AMBAO TAYARI WAMESHAPATA KASHFA MBALI MBALI WASIJARIBU KURUDI KWA LAZIMA KUONGOZA WATANZANIA AMBAO UMASKINI WAO KWA KIASI KIKUBWA UMETOKANA NA MAAMUZI YALIYOFANYWA SI KWA MASLAHI YA WACHACHE.

Mlivyoipora hii nchi vinatosha na kwa bahati mbaya mmepoteza sifa ya kuwa viongozi wa umma. Tunahitaji watu waaminifu, committed, na wachapa kazi ambao wana dhamiri ya dhati ya kuwainua watanzania kwa kutumia vema rasilimali za nchi yetu.

Tunataka viongozi watakaowasikiliza wananchi na siyo watakaojitengenezea miradi kwa ajili ya watoto wao na fndugu zao.

Watanzania tutumie uwezo wote tuliopewa na Mungu tukatae kuwaruhusu watu kama hawa kutuongoza.

CCM wekeni maslahi ya watanzania mbele ili kuokoa nchi na wezi,na waporaji ambao wamevaa vazi la Chama lakini ndani ni Mbwa mwitu wakali. Kama mtawalelea hawa dubu ipo siku watakosa chakula na wataanza kuwatafuna ndani ya Chama. Mungu atawadai kutokana na Mateso na vilio vya maskini wa Tanzania ambao umaskini wao unaongezeka kutokana na wizi na uporaji wa maliasili zao.

Mateso na vilio vya watanzania vitakuwa laana kwa watoto na vizazi vyenu. tafadhali kaeni pembeni iachieni nchi iongozwe na watu waadilifu.

Mnawatwisha watanzania mizigo mizito na mnakataa siyo tu kuwanasua bali mnawazuia kujinasua kwa kuwaibia kura zao.

Tuwasaidie watanzania kwa kujiweka pembeni tukubali tumeshindwa na tuwaachie wenye dhamira njema na nchi yetu waendelee

HIma Hima Tanzania
Mungu Ibariki
Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom