Ishara ya Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed''

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,519
6,511
Jina la Hollywood lilibadilishwa na kuwa Hollyweed
_93205197_hollyweed.jpg


Raia wa Los Angeles ambao ndio majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood' waliamka mwaka mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'.
Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45.
Wapiga kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8 Novemba.
Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo.
Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.
Chanzo: BBC Swahili
 
Tatizo wamepigwa cover sana naona wamechukia.

HOLLYWOOD.

bollywood
Nollywood
Swahiliwood.

Wakaona isiwe taabu.nasubiri kuona swahiliweed.
 
Herufi zina urefu wa futi 45?
bango hilo lina ukuba wa gani?

halafu, wavuta bangi kweli hawaaminiki, yaani wameona walibadilishe ili iliwapendelee!
 
Back
Top Bottom