Ishara hizi zinaweza kukusaidia ktk maamuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ishara hizi zinaweza kukusaidia ktk maamuzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by CPU, Mar 11, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Habari za Ijumaa wana JF wenzangu
  Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku

  Leo nina kitu kidogo cha kusema kwa wanawake kuhusu wanaume ktk mapenzi
  Changamoto kubwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ni kupata mpenzi mwenye upendo wa kweli na dhati. Nia ya kila mmoja ni kuwa na rafiki ambaye watatumia muda mwingi kufurahia pamoja kuliko kinyume chake.

  Mapenzi ni amani, furaha na upendo na kama moja kati ya mambo hayo yanakosekana kwenye mahusiano hapo lazima lizaliwe tatizo.

  Wanawake huwa na matarajio makubwa wanapoanza mahusiano na wanaume, na inapotokea hisia na mawazo yao yameshindwa kutimia huumia sana. Ni ngumu mwanamke kusoma mawazo ya mwanaume haraka kwa vile wanaume si watu wa kuonyesha mapema matarajio ya baadaye kama walivyo wanawake. Mwanaume anahitaji muda wa kufanya maamuzi kabla ya kwenda hatua nyingine, na mwanamke pia hufanya hivyo, lakin tofauti ni matarajio ya wanawake ni ya mapema zaidi

  anawake hujisikia vibaya zaidi wanapoona mahusiano yao na wanaume yanashindwa yanashindwa kusogea hatua nyingine, na hofu kubwa ni kwamba kuchelewa huko kunaweza kukawa na hitimisho la kutengana. Wanaona wanaume ni watu dhaifu na wenye uvumilivu mdogo wa kukwepa vishawishi tka kwa wanawake. Hili ni kweli kwa asilimia kubwa ya wanaume. Na kwa sababu hiyo wanataka wanaume wachukue maamuzi ya haraka (sio kwa papara) ikiwa kama njia ya kulinda penzi.

  Hivi hapa chini ni viangalizo vitakavyokupa taswira kama kweli mwanaume ana nia ya kweli kota moyoni au hana sababu.

  Mkweli toka moyoni
  1) Atakutafuta na kuongea na wewe mara nyingi kwa kadri atakavyoweza. Hii inawezekana kwa njia ya simu, email, barua, au hata kutuma salamu za mdomo kupitia watu wengine kama marafiki, ndugu na jamaa.

  2) Atatimiza ahadi aliyokupa. Akisema atakutafuta kwa ajiri ya maongezi, kukupigia simu au ahadi nyingine yoyote atafanya hivyo kwa muda aliousema awali

  3) Ataonyesha kujali kwa mambo unayoyapenda, kwa mfano kama unapenda kwenda muziki, filamu, aina fulani ya chakula, maua, au mambo mengine unayoyapenda ataungana na wewe ktk kufurahi hata kama itatokea kati ya mambo hayo sio hobi yake

  4) Mwanaume wa aina hiyo atakuwa wazi kuonyesha hisia zake kwako, atakuwa wazi kwa kadri awezavyo, hii itakuwa ni pamoja na kukueleza jinsi gani anajisikia anapokuwa karibu na wewe

  5) Atakufunza utamaduni wa kujenga urafiki wenye dhamira ya dhati, matumaini ya muungano imara na usiokuwa na tamati kati yenu na ukweli halisi pendo toka moyoni

  Aliyekosa ukweli
  1) Mwanaume asiyekuwa na nia kwanza atakuwa mgumu kutimiza ahadi alizotoa mwenyewe kwako, atakuwa na sababu nyingi na maelezo marefu yasiyolenga kukutia moyo wala nguvu

  2) Wakati mwingine atakuwa mbali na wewe, hatopenda kuongea na wewe kwa kirefu, na akilazimika kuongea atafanya hivyo kwa muda mfupi tu na kukupa sababu kedekede kwanini hapaswi kuongea muda mrefu

  3) Anaweza kukuambia atakuja muda fulani lakin asifanye hivyo na bado asikueleze sababu za kushindwa kuja kwake kama hutosumbuka kumuuliza

  4) Atakuacha kwenye mtihani wa kutoweza kutambua wala kujua hisia zake kwako (anakupenda au hakupendi)

  5) Hatojali hisia zako za kimapenzi, si kwa kukuangalia tu bali hata kwa vitendo kama itatokea amekubali kuwa na wewe faragha

  6) Hatojali kukuuliza wala kukushauri kuhusu tatizo lolote linapotokea kwako hata kama atakuwa ameliona

  7) Atakuacha huru (si kwa maana ya kukufuatilia) bali kutojali. Hii ina maana kwamba wewe mwanamke ndiye utakayekuwa na jukumu la kumtafuta na usipofanya hivyo kwake ndio furaha.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hivi kweli kuna wanaume kama hao kwenye red???????????

  wanapatikana wapi??

  kama wapo PM to me plzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!
   
 3. Zneba

  Zneba Senior Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wapo susy ila mpka uje umpate mbona na muda wa kuwa nae pia utakuwa umekupita ila alosema yote CPU jamani kwa asilimia kubwa ni kweli kabisa mwanaume akiwa hakutahitaji hizo dalili karibu zote huwa anazionyesha.mmmh kazi
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  My dia

  If its only you who think you cant get it then challenge yourself.
  If you have the will power you will get it.
  If you don't, you know to which group you belong. Its where you want to be.
   
 5. charger

  charger JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Haswaaa umeongea CPU thanx for this useful mada
   
 6. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu cpu..... hapa naona umenieleza mimi binafsi kuwa hizi ni tabia zako hapa nakupa hongera uko fiti...ila mimi nipo hivi nafanya hivyo na kama madada watanikimbia niko hivyo na sibadiliki yaani let people call me I am a conservative man but ninachojua I am aradical man....mimi naongozwa na ''the man is nothing but of secrecy and self reliance'' ...nakutabilia kuumia kwa haya mawazo yako.
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Sasa wakati mwingine mtu unakuwa mkweli toka rohoni, then unagundua kuwa mwenzio ni Mbwiga! unaanza na wewe kupiga sanaa, nani alaumiwe?
   
 8. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  huyu ni mwanamume wa kufikirika na anapingana na ''creation of God'' kama mimi mwongo mwulize Adam yaliyompata baada ya kukubali kula tunda alilopewa na Eva.....HAYUPO.

  I was born with it and not without it.
   
 9. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,108
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  wapo wengiii tu...ila ndo wengi tume waiwaaaa hahahahaa
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Kinachonipa shida wapo wasio na mapenzi ya kweli na mwanzoni mwa mahusiano wanakuwa na tabia kama za wenye mapenzi ya kweli....baada ya muda na kuwa wampiga hatua fulani ndio hasa unaweza kuona rangi zao kuwa hawana mapenzi ya kweli....na wapo wenye wasioweza kufanya hayo ya wenye mapenzi mema kutokana na circumstances fulani fulani....its complicated....thanks for guidelines!!!!!!!!!!!!
   
 11. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  nani alaumiwe?...mwulize Samsoni wa katika biblia nini kilimpata baada ya kuweka kila jambo hadharani kwa mdada Delila...utapofuliwa macho......''man is nothing but of secrecy and self reliance''
   
 12. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwanini upate shida ya kuuliza susy wakati hata wanawake wenyewe hawawataki wanamume kama hawa....raha ya kidume kidogo uweze kutoa faraja hata za uongo kidogo......ukweli ukitawala sana ndiyo kusema wanasayasi wa saikolojia ni waongo wanaposema wanawake wanavutiwa zaidi na uongo kuliko ukweli ok basi kiu,uwazi,ijumaa na magazeti mengi ya udaku yangekosa wateja.

  I was born with it and not without it
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  ndugu umenikumbusha yvle mdau aliyekuja kuomba ushauri akiwa kitandani kwa ugonjwa wa mapenzi kisa kamdanganya binti kuwa yuko master's kumbe undergraduate.
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenichekesha sana kwenye hizo bold
  Yaani unanipa hongera niko fit halafu unanitabilia kuumia???!!!
  Sioni uoanisho wowote hapo.
  Lakin nashukuru kwa sifa zako kwangu na utabili wako :juggle:
  Sometimes pipo are going to be totally different in terms of views and experience.
  What you have experienced in your environment is different to mine.
  For me, what i have written I have a visible proof, although I accept whatever the challenge
   
 15. CPU

  CPU JF Gold Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  So God has created pipo to lie?????
   
 16. CPU

  CPU JF Gold Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa mkuu nimekuelewa uko wapi (Udaku)
  Nashukuru kaka
   
 17. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kumbuka wanawake hawapendi ukweli wa dhati lazima uongo mapenzi yananoga kweli
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Natamani nisingekua huku via mobile ili nichangie vizuri!Nwyz vyote vilivyo kwa mkweli unaweza kuvipata kwa muongo ikiwa amedhamiria kukukamata na yanamgusa muongo unaweza kukuta moja au mawili yamemdondokea mkweli!Hapo kinachohitajika ni uelewa!Always penda kujua sababu ili uone kama ina uzito au lah!Usije ukamwacha mtu mzuri kisa tu alichokuahidi hakijatimia kwa sababu moja ama nyingine!
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nachukia mawazo ya aina hii!Kumdanganya mtu una baiskeli kumbe una mkokoteni kunanogesha nini?
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Shemeji ahsanteeee!
  Ila wengine huwa sio wawazi ili kupima uelekeo wetu.
   
Loading...