Is this the new way of colonialism in Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is this the new way of colonialism in Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mstahiki, Feb 3, 2010.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=Y-7b9QbVJUo[/ame]
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,171
  Likes Received: 9,787
  Trophy Points: 280
  Deng Xiaoping would say this is "Open Door Policy"

  Tatizo si kwamba investors wanakuja, labda uniambie management ya investors vis a vis corruption.

  Lakini kama serikali inaweka mikataba mizuri, mbona hata wafanyakazi wa Afrika wataongeza GDP zao na ya nchi.

  Mimi sina tatizo fundamentally na investment, we actually need more of it.Tatizo langu ni management tu.
   
 3. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kiranga,

  Umeicheki video mpaka mwisho?Je umeona watu walivyofukuzwa kwenye mashamba yao?
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,171
  Likes Received: 9,787
  Trophy Points: 280
  Kuwafukuza bila dignity noma, hata under sheria za "eminent domain" ambazo kwazo serikali ina assert ownership ya ardhi, basically saying wananchi wana lease tu ardhi kutoka serikalini, na kama kuna issue inahusu national interest (serikali inataka kujenga barabara, H.E.P etc) basi sheria zifuatwe, watu wapewe ample time na compensation na mambo ya utamaduni na mazingira (kama si mazingara) yapewe umuhimu wake.

  Swali langu,

  Kama tuna ardhi kubwa sana, kwa nini serikali isiwape investors sehemu ambazo hazina watu tayari?
   
 5. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 5,014
  Likes Received: 2,537
  Trophy Points: 280
  Concord,
  Hii ndio tunaita faida ya citizen journalism na asante kwa habari hii ili ijadiliwe hapa JF.
  .
  Video clip kuanzia 3:48 mpaka 6:38 inaonyesha jinsi Wananchi wa Eneo la Namawala, Kilombero Tanzania, walivyotimuliwa na serikali yao kupisha wawekezaji wapate eneo la hectari 10,000.

  Kutokana na maguvu ya serikali yao, Wakazi imebidi wakimbie mashamba yao, shule nzuri ya watoto kwa ajili ya watoto 200 kuwa gofu, wana kijiji wamefungua kesi mahakamani hakuna mwakilishi wa serikali wala wawekezaji wanaotokea mahakamani kujibu madai ya wana kijiji!

  Huu ni ukabaila na sio uwekezaji, maana haki za wananchi hazizingatiwi, sijui kama Mh. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro anaweza kuzuka ktk maeneo haya kama ilivyokuwa ktk mafuriko huko Kilosa, kutafuta kiini cha wana kijiji kunyanyaswa?
   
 6. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 495
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Je hii ilikuwa lini?Hao waliofukuzwa waliweza kurudi majumbani kwao?
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Waige mambo ya wale wananchi wa hanang, that is the only language leaders understand
   
 8. Natty Bongoman

  Natty Bongoman JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2010
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  dammit... hii imenikera vile sirikali, badala ya kunufaisha wananchi, inawatimua majumbani na mashuleni mwao... fvcked up!

  * Huu ni ukoloni ambao unasaidiwa na serikali zetu barani... kweli, kinachoudhi sana ni vile walivosema walimaji wapya hata hawatakuwa chini ya sheria za kibiashara... yaani wataweza kuuza chakula ng'ambo na kuwanyima wenyeji wenye njaa ... huu upuuzi gani basi??? ... hata sijasikia sheria ya kulazimisha kuajiri wananchi... viongozi wetu wanakuwa ka mtoto mdogo anaeambiwa auze dhahabu kwa shilingi mia moja kwa vile hajui thamani zake... pia, kweli, wanatenda ujangiri kuwafukuza wananchi majumbani mwao bila hata ya kuwapa nyumba na sehemu mpya ya kuishi... WHY SUCH CRUELTY TO YOUR OWN PEOPLE SIRIKALI??? yaani kweli hamjui yale majumba ya matofali ni utajiri wao?????????????? mmesahau maisha ya vijijini ????????

  ** colonism ni kuwanyang'anya wenyeji bila kuwanufaisha... huu ni ukoloni kabisaaa
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo yaliyotokea kule Loliondo na kama Watanzania hatukuwa makini kuhusu kulipinga hili basi matukio kama haya yatakuwa mengi sana sehemu mbali mbali nchini. Pamoja na kuwakaribisha "wawekezaji" lakini ukaribishwaji huo ni lazima uhakikishe wenye ardhi nao wananeemeka labda kwa kuwa partners kwenye miradi hiyo kama ni kilimo, uwindaji au uchimbaji madini na pia kupata ajira, vinginevyo kutakuwa na maafa makubwa sana.
   
 10. bona

  bona JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,794
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  uwekezaji haujawai leta maendeleo popote pale duniani, nchi inaweza kuendelea pekee kama njia kuu za uchumi ziko chini ya serikali, haiti walileta wawekezaji kila idara toka miaka ya 50's, zimbabwe hadi walisifiwa na inayojiita jumuia ya kimataifa kua ni mfano wa kuigwa na nchi za africa, wako wapi sasa? taifa linalokua halina manufacturing industry na likaendelea halijawai toka labda nchi za kiafrika za sasa ivi ndio zilete uo muujiza, andalia izo tiger economies zote zina strong manufacturing industry, brazil,malyasia,singapore,korea,argentina,india etc
  wawekezaji wanaitajika ktk joint venture tu na si kuendesha completely na izo tiger economies wawekezaji wamekuja ktk form ya joint venture tu!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...