Is this a serial killing?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Wote wanahusika na usalama wa watanzania kwa namna moja au nyingine.

Noel Paul Jenga (33)=>kaijipiga risasi moja kichwani , akiwa chumba cha kutunzia silaha cha TANZANIA POLICE ACADEMY, Dares salaam.
"Katika taarifa hiyo iliyoandikwa saa 12.45 asubuhi, Konstebo Noel Jenga, alisema kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa hiyari yake bila ya kulazimishwa na mtu yoyote na ameomba asisumbuliwe mtu yeyote kutokana na tukio hilo. Kabla ya kutimiza kusudio lake, marehemu aliwapigia simu baadhi ya ndugu zake kuwaaga, akazima simu, akaweka mtutu wa bunduki mdomoni kisha akajifyatulia risasi." SACP Alice Mapunda

WP Suzanna (22) => kajipiga risasi nne upande wa kushoto kifuani, akiwa nimahabusu katika kituo cha Tarime,"PC SUZANA alijiua baada ya kuamuriwa kurudi kituo cha kazi kufuatia kupotea kwa msafara wa Rais." Kaimu Msemaji wa jeshi la Polisi, ADVERA SENSO.

Mashauri (24)=> kajipiga risasi mbili chini ya kidevu, akiwa eneo la Ikulu ya Mkoa wa iringa (Gangilonga), kisa "wivu wa mapenzi baina yake na askari mwenzake" Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla

Mzee Mnyeti (32)=> kajipiga risasi nyumbani kwake kijitonyama. "Ni kweli mwili wake ulikutwa saa 8:45 ukiwa chumbani mwake, baada ya watu kubomoa mlango," Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga

Hivi vifo vinanipa maswali mengi sana.
1. Kwanini vijana(angalia umri) hawa wafe?
2. Ni kwanini wafe sasa katika mwaka wa uchaguzi katika kipindi kisichozidi miezi mitatu?
3. Kwanini maelezo yanayotolewa baada ya vifo vyao hayaonyeshi kuwa wanajiua ila ni kama kuna mauaji yanafanywa lakini ukweli wataka kufichwa?
4. Nini matokeo ya uchunguzi wa Tume alizounda IGP Saidi Mwema?
5. Kama ni serial killing, nani anaendesha mauaji haya?
 
kuna kitu hapa, subiri,

Ni kweli! Nami nafikiri kuna kitu. Lakini,ninapoendelea kusubiri, hivi unafahamu ama umesikia kwanini zile ripoti za Tume zilizoundwa na IGP hazijatoka hadi leo?
 
Ni Frustation za maisha,mapenzi etc...

Hivi ukiwa na msongo wa maisha unaweza kujipiga risasi mbili chini ya kidevu ukiwa na lengo la kujiua? Ama risasi nne ukiwa na lengo hilohilo lakujiua?

Kwanini msongo huu uwakute wanausalama hawa katika umri huo?

Kwanini isiwe eatu wa kituo kimoja cha kazi au mkoa mmoja, mbona kuna-mtawanyiko wa namna fulani? Ni nini mahusiano ya vijana hawa? ama ni taarifa gani in-common wanayoijua/wasiyoijua?
 
It is a good post, lakini kamwe hatvapata majibu ya maswali haya
 
Mkuu MNYAMAHODZO umenena niliyokuwa nafikiria all the way. maana inaonesha kuna dots zinafuatana kwa vifo hivi. Halafu kama kawaida wale walio responsible wanatoa maelezo mepesi kana kwamba aliyekufa ni inzi au mbu. Naamini kunawezekana kukawa na mauaji mengine yaliyofichwa ambayo yanahitajika maelezo ya kina pia.
Hii inaonesha kuna muunganiko wa mauaji haya na anayeyafanya ni mtaalam/ wataalam na yanalindwa na mfumo.
Au tuseme vifo hivi vimepangwa na vina sababu zake kwa manufaa ya taifa???

Natamani ningekuwa licenced sniffer ningechimbachimba hizi kadhia ili kupata majibu kwa manufaa ya umma.
 
Wote wanahusika na usalama wa watanzania kwa namna moja au nyingine.

WP Suzanna (22) => kajipiga risasi nne upande wa kushoto kifuani,

Mashauri (24)=> kajipiga risasi mbili chini ya kidevu,

Je Mtu anaweza kujipiga risasi zaidi ya mmoja? Automatic rifle inaweza kufanya hivyo?
 
je mtu anaweza kujipiga risasi zaidi ya mmoja? Automatic rifle inaweza kufanya hivyo?

jiulize mkuu hapo kuan ka wasiwasi kwa mbali labda watalam wa maswala ya bunduki watufafanulie
 
Serial killers ni wale wanaoua watu wengi kwa vipindi tafauti.

Mfano katika kipindi cha mwezi mmoja au miaka kadhaa huwa anaua watu ambao hawana hatia. Inawezekana ni wanawake wa umri fulani, au watu wa jamii fulani (wamarekani weusi, waafrika, mashoga na kadhalika),

Kujipiga risasi mwenyewe ni 'comitting suicide'. Na inakuwaje mtu kujipiga risasi nne, ile ya kwanza tu inamuua au inamfanya awe paralysed.
 
Je Mtu anaweza kujipiga risasi zaidi ya mmoja? Automatic rifle inaweza kufanya hivyo?

inaweza,
. Hii ni kutoka chanzo cha habari cha kuaminika.
Kama haumini unaweza kujaribu.
Utata mwingine unaweza kuchunguzwa simple kama vile... Je wote walimaliza depo pamoja, yaani walikuwa kozi pamoja? Au walishafanya kazi katika kituo kimoja hapo kabla au je wali wahi kufanya kazi kwa nyakati tofauti lakini kituo kimoja??
Ukipata maswali ya majibu hayo ni mwanzo mzuri...
 
Excellent approach for behavioral analysis, big up!
 
inaweza,
. Hii ni kutoka chanzo cha habari cha kuaminika.
Kama haumini unaweza kujaribu.
Utata mwingine unaweza kuchunguzwa simple kama vile... Je wote walimaliza depo pamoja, yaani walikuwa kozi pamoja? Au walishafanya kazi katika kituo kimoja hapo kabla au je wali wahi kufanya kazi kwa nyakati tofauti lakini kituo kimoja??
Ukipata maswali ya majibu hayo ni mwanzo mzuri...
Ni nyongeza tu,
Je vijana wanamfahamu (nao pia kujulikana) na mtu fulani "muhimu"?
Je wanaripoti jambo flan kwa "common point"?
Is registration of phone numbers revealed their mission?
 
WP Suzanna (22) => kajipiga risasi nne upande wa kushoto kifuani, akiwa nimahabusu katika kituo cha Tarime,"PC SUZANA alijiua baada ya kuamuriwa kurudi kituo cha kazi kufuatia kupotea kwa msafara wa Rais." Kaimu Msemaji wa jeshi la Polisi, ADVERA SENSO.

Mashauri (24)=> kajipiga risasi mbili chini ya kidevu, akiwa eneo la Ikulu ya Mkoa wa iringa (Gangilonga), kisa "wivu wa mapenzi baina yake na askari mwenzake" Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla

Mzee Mnyeti (32)=> kajipiga risasi nyumbani kwake kijitonyama. "Ni kweli mwili wake ulikutwa saa 8:45 ukiwa chumbani mwake, baada ya watu kubomoa mlango," Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga

Hivi mtu anajipigaje risasi 4? hii inawezekanaje?
This explanation is not sufficient. There is no way you can shoot yourself 4 times in the chest, unless someone was doing the killing.
 
Hivi ukiwa na msongo wa maisha unaweza kujipiga risasi mbili chini ya kidevu ukiwa na lengo la kujiua? Ama risasi nne ukiwa na lengo hilohilo lakujiua?

Kwanini msongo huu uwakute wanausalama hawa katika umri huo?

Kwanini isiwe eatu wa kituo kimoja cha kazi au mkoa mmoja, mbona kuna-mtawanyiko wa namna fulani? Ni nini mahusiano ya vijana hawa? ama ni taarifa gani in-common wanayoijua/wasiyoijua?

Kwa aina ya bunduki wanazotumia askari wetu ikiwemo SMG, kujiua kwa kujipiga risasi nne sijui inawezekanaje. Halafu maeneo ambayo mtu anajipiga unajiuliza alitumia AK 47 kwamba zilitoka kwa mbonyezo mmoja wa 'triger'!!! maana AK 47 hatuzitumii kwenye majeshi yetu.

Risasi inayoweza kuonekana ni kujiua ni moja tu. zaidi ya hapo ni utata!!!!!
 
Wote wanahusika na usalama wa watanzania kwa namna moja au nyingine.

Noel Paul Jenga (33)=>kaijipiga risasi moja kichwani , akiwa chumba cha kutunzia silaha cha TANZANIA POLICE ACADEMY, Dares salaam.
"Katika taarifa hiyo iliyoandikwa saa 12.45 asubuhi, Konstebo Noel Jenga, alisema kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa hiyari yake bila ya kulazimishwa na mtu yoyote na ameomba asisumbuliwe mtu yeyote kutokana na tukio hilo. Kabla ya kutimiza kusudio lake, marehemu aliwapigia simu baadhi ya ndugu zake kuwaaga, akazima simu, akaweka mtutu wa bunduki mdomoni kisha akajifyatulia risasi." SACP Alice Mapunda

WP Suzanna (22) => kajipiga risasi nne upande wa kushoto kifuani, akiwa nimahabusu katika kituo cha Tarime,"PC SUZANA alijiua baada ya kuamuriwa kurudi kituo cha kazi kufuatia kupotea kwa msafara wa Rais." Kaimu Msemaji wa jeshi la Polisi, ADVERA SENSO.

Mashauri (24)=> kajipiga risasi mbili chini ya kidevu, akiwa eneo la Ikulu ya Mkoa wa iringa (Gangilonga), kisa "wivu wa mapenzi baina yake na askari mwenzake" Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla

Mzee Mnyeti (32)=> kajipiga risasi nyumbani kwake kijitonyama. “Ni kweli mwili wake ulikutwa saa 8:45 ukiwa chumbani mwake, baada ya watu kubomoa mlango,” Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga

Hivi vifo vinanipa maswali mengi sana.
1. Kwanini vijana(angalia umri) hawa wafe?
2. Ni kwanini wafe sasa katika mwaka wa uchaguzi katika kipindi kisichozidi miezi mitatu?
3. Kwanini maelezo yanayotolewa baada ya vifo vyao hayaonyeshi kuwa wanajiua ila ni kama kuna mauaji yanafanywa lakini ukweli wataka kufichwa?
4. Nini matokeo ya uchunguzi wa Tume alizounda IGP Saidi Mwema?
5. Kama ni serial killing, nani anaendesha mauaji haya?

What if I told told you today that I killed all those people, and I'm still free to kill at will?
 
Ni kweli! Nami nafikiri kuna kitu. Lakini,ninapoendelea kusubiri, hivi unafahamu ama umesikia kwanini zile ripoti za Tume zilizoundwa na IGP hazijatoka hadi leo?

nimekusoma toka juzi unavyochangia na ulivyoanzisha hii mada, ila nahic kua una jua mengi kuliko unayoandika, kwa nini usitoe tu moja kwa moja tukapata picha, kwa mfano ilol suala la kwa nini ripoti za IGP hazijatoka!
 
Mtu kujipiga risasi 4 inawezekana. Kumbuka ukijipiga risasi sio kwamba unakufa muda huo huo. Hata ikitokea ukakatwa kichwa ghafla, kuna maneno utakuwa unazungumza kwa dakika kadhaa. Kujipiga risasi nne inawezekana kabisa.
 
Mmmh!!.....Sawwa.:disapointed::sad:
 
Back
Top Bottom