Is there something wrong with us, Tanzanians????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is there something wrong with us, Tanzanians?????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumba-Wanga, May 26, 2011.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wa JF! Nimekuwa najiuliza watanzania tuna nini? What do we miss that our countries have. Just look at Rwanda and Uganda. they have fought civil wars, but look at their economies! We are proud of been Island of peace.

  Ni kitu gani tunachokitanya vizuri? Angalia maisha ya watu! Umaskini ni rampant despite ahadi hewa za maisha bora kwa watu. Agalia elimu yetu, ndio hata huwezi kusema lolote, ni masikitiko matupu! Shule za kata zimekuwa disaster (sitaki kuongelea yale ua UDOM).

  Watanzania! Angalia Richmond, Songa gas! unaweza kuamini kuwa kuna watu wana guts za kumwaga maji ya Mtera, kutengeneza mgao ili ku justify ununuzi wa mitambo ya Dowans! ikifika hapo nachoka kabisa! Mgao unapowabana watanzania, tunaambiwa ni kosa la wanasheria wa serikali/TANESCO kutafsiri vifungu vya sheria ndio chanzo cha machungu ya watanzania!!!

  Hapo bado EPA, Kagoda na mengine! mbaya zaidi ni kuwafunga watu wadogo kwenye EPA wakati vigogo wapo, kwa kweli, people are not interested in these day light robbery, wamechoka! Kila kitu ni kiini macho!

  Tunajifunza nini kwenye chaguzi zilizopita? wananchoiwamekwenda kulinda kura, wanajua kuwa haka yao itapokwa. Juzi juzi watu wamevamia mgodi wa North Mara, wakijua kabisa kuwa polisi wana live bullets! Are we still blind? Swala na issue sio kwenda kule kulinda maiti zisizikwe, bali kuangalia swala hili kwa undani zaidi! Picha nzima inatuambia nini? watanzania wamechoka kuona mali zao zinaporwa, in day light!

  Kwa miaka mingi wakenya wamekuwa wanatumia mlima Kilimanjaro kwa faida yao! What are we doing? nothing, just clapping maisha bora kwa kila mtanzania, wao wanakusanya pesa na uchumi wao unakuwa! Sisi tumekalia siasa!

  Angalia kwa babu wa Loliondo! More than 75% of the visitors are Kenyans, na mbaya zaidi wanaingia nchini kwetu watakavyo! wale waliowahi kwenda kenya wanakuliana na mimi kuwa kama babu angekuwa nchini kwao, sidhani kama sisi tungeweza kujazana kwako kiasi hicho! Polisi wao wangetunyanyasa sana!

  Mpira! Hata huo tunashindwa? DRC wanafunga tikmu yetu ya taifa, wakati wao nchi yao ina vita, sisi ni wazee wa amani! Hata organization ya football in a peaceful country is not possible!

  Look at the altitude of Tanzanians! watu hatupendi kufanya kazi, tunapenda njia za mikato, mission town and the like! Siku hizi ni sifa kuibia serikali, kujenga majumba na mengine. wazee wa zamani waliofanya kazi kwa uadilifu wako wapi? angalia yaliyompata Mh Shelukindo, mtu aliyewahi kupewa tuzo la ufanyakazi wa uliotukuka! Yaliyompata na mizengwe yote, yako wazi!

  wakulima! Nao wamejifunza jinsi ya kuishi kwenye hii system. nao wamekuwa waongo, ukizubaa tu umeuziwa mazao pungufu kuliko unayolipia! wao

  Itokee bahati mbaya upate ajali huko njiani! Utaziona hasira za watanzania watakavyokushughulikia! Utawalaumu? wao hawana mgao na maisha yao yamesimama, kila kitu bai juu (sukari, petrol sabuni na mengine)

  Jamani tunakwenda wapi? tunawafundisha nini watoto wetu?
   
 2. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Labda tunahitaji civil war na sisi!...
   
 3. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  yan kwa kwel inauma sana yan umeongea kwa hasira na ukwel mpaka hata mm umenipandisha hasira hivi ni kwanini iwe tanzania tuu hivi kwanini jaman ni kwel tunasonga mbele kwa namna hii? Au kunalingine mana ninashindwa kuelewa? Kwan hatujifunzi kupitia wenzetu? Mana ninashndwa kuelewa tatzo lipo wap tanzania mana kama wasomi wapo lakn chaajabu wasomi ndio wezi kuliko wasiokuwa wamesoma yan nchi hii haina mzarendo wazalendo wote wameshajifia. Hapa kunawez na propaganda za hapa na pale yan uwongo mtupu. Heee.. MUNGU IBALIKI TANZANIA IBADILIKE NA UWABADILISHE WATU WAKE AMEN. Kunamwanafalisafa aliwah kusema ukiwachukuwa wamerekan ukawaleta tanzania na watanzania wakaenda malekan alafu ukawaacha ukarud baada ya miaka mitano utakuta wamarekan waliokuja tanzania wameijenga tanzania na watanzania walio kuwepo malekan wameibomoa marekan akauliza unajua kwann? Hebu tafakari mwanajf thnker juu ya hili tanzania kunakwenda wap?
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tunamiss viongozi wenye nia ya dhati tulionao wamejaa magamba ya chuki na tamaa
   
 5. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Tuna laana kwa sababu ya kutoitambua ISRAEL na kushirikiana nao. Believe me or not, juzi juzi waziri foreign affairs akaongeza chumvi kwenye kidonda kuwa TZ itahakikisha inaiunga mkono palestina ipate uhuru wake, na akailaani ISRAEL kwa nguvu zake zote kwa niaba au kama msemaji wa TZ; hiyo ni kuzidi kujichimbia shimoni. Wageni watakuja watakula na kusaza mbele ya macho yetu, tutauliwa na polisi wetu wenyewe kwa ajili ya kuwalinda wageni na tusipobadilika, miaka nenda rudi tutaendelea kupiga mark time kwa kwenda nyuma! Wageni watazidi kuja na kupora mali yetu yote, si twiga, pundamilia, ndege nk kila kitu kinaonja joto ya jiwe kwa sababu hiyo; wataendelea kutoroshwa na kuvunwa kama wao na hakuna litakalofanyika. Miundo mbinu yote ni kituko. Nadhani umesikia aliyekuwa MD wa ATCL amestaafu hakuna hata ndege inayofanya kazi. Tutaendelea kudidimia hivi hivi mpaka tutakapogeuka nyuzi 180 na kubadili misimamo yetu. Nadhani TZ is a sick man of East Africa, kweli si kweli? Sudan itapata uhuru na itatupita! Mungu atuhurumie! :pound:
   
 6. g

  gugu Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  We a just a bunch of people with no real back borne. We a cowards. One instance. Leo nimesoma issue moja kuhusu wanaigeria wenye makesi ya uhalifu wameachiwa kuongoza mabenki na wanatumia mabavu kuwanyanyasa ndugu zetu watanzania lakini cha kushangaza baada ya mda kidoogo iliondolewa kiaina. Hii inaacha maswali mengi sanaya kujiuliza je uzalendo tunao au ni maneno tu maji yakishinda shingo ni survival of the fittest
   
Loading...