Is the Bank of Tanzania Independent?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
799
Kadhia ya Ballali inayoendelea sasa hivi ni matokeo ya aidha Gavana kukosa uhuru wa kusema NO kwa serikali kila inapohitaji mshiko ama ni uroho wa Gavana mwenyewe katika kutafuna hela hizo akisaidiana na wakuu walio serikalini.

Nimesoma michango mingi sana kwenye thread ya Ballali kujiuzulu, baadhi tumemlaumu kwamba ni fisadi na hivyo sheria ichukue mkondo wake. Wengine tumedai kwamba Ballali hakuwa na uwezo wa kusema NO kwa serikali na hivyo yeye ametumika katika ku-facilitate uchotaji wa hayo mabilioni ambayo yamepotea. Kwa hiyo hata kama angekuwa ni mtu mwingine lazima angeyatoa tu hayo mabilioni kwa kuwa huwezi kuwa na guts za kuwakatalia walio serikalini na kuna walio toa mfano wa Rutihinda na Kibona (sijui issue yao ilikuwaje) lakini inawezekana kwamba labda walisema NO kwa serikali na leo hii hatuko nao, walisha tangulia mbele ya haki.

Tangu 1992 serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki Kuu walianza mchakato wa kurekebisha sekta ya fedha na mojawapo ya hoja ilikuwa ni kuifanya Benki Kuu iwe huru katika utendaji kazi, yaani isiingiliwe na serikali. Hii inatokana na ukweli kwamba serikali ikiingilia utendaji kazi wa Benki Kuu ni rahisi kusababisha mfumko wa bei ikiwa ni pamoja na kuifanya ijikite kwenye kuinusuru serikali kila inapokuwa na nakisi katika bajeti yake. Kwa kuwa Gavana ni mteule wa Rais, si rahisi kukataa kuchota mapesa na hasa serikali inahitaji.

Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 1995 na hivi majuzi ya mwaka 2006 zote zinasisitiza kwamba lengo ni kuifanya Benki Kuu iwe huru zaidi, yaani katika utendaji wake isiingiliwe na viongozi wa kitaifa ambao wanaweza kufanya maamuzi ya kisiasa zaidi kuliko kiuchumi.

Je, hayo wanayodai kwenye sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha kwamba lengo ni kuongeza uhuru, ni maneno matupu ama watu wanatumia sheria vibaya.

Nimeota ndoto kwamba ninaweza kuteuliwa kuchukua nafasi ya Ballali, kabla sijaingia ofisi hiyo naomba ushauri wenu wa dhati kabisa kwenye haya maswali ili siku nikiingia hapo nijue namna ya kukwepana na mafia ama serikali au niwe na guts za kusema NO kwa serikali. Vinginevyo haya yaliyompata Ballali yanaweza kunikuta na nikajikuta ninaishi uhamishoni bila kupenda au nikatangulia mbele ya haki.

Moja, nini kifanyike ili kuifanya Benki Kuu ya Tanzania iwe huru zaidi na hivyo kumpa fursa Gavana wake kusema NO au kutokuingiliwa na serikali (awe ni Rais ama waziri wa fedha).

Mbili, ikifika mwaka wa uchaguzi ni mbinu ipi nzuri ya kuikwepa serikali ili wasije wakaomba hela ya kampeni. Hili huwa linatokea nchi nyingi sana kwamba mwaka wa uchaguzi hela nyingi huwa inachotwa kutoka Benki lakini kwa kutumia njia tofauti. Ni namna gani unaweza kusema NO????

Tatu, suppose Gavana akisema NO kwa serikali au mafia, je wanaweza kum-eliminate? Na kama wanaweza kum-eliminate je Gavana atumie njia gani kujilinda na hilo? Akimbie nchi kama Githongo wa Kenya ama abaki nchini? Kama akitishiwa maisha, je, atoe ripoti polisi ama wapi?

Nne, ni mabadiliko gani ya ziada yanatakiwa kufanyika kwenye sheria ya Benki Kuu na Taasisi za fedha ili kuifanya Benki Kuu iwe huru zaidi?

Nitarudi na maswali ya ziada huku nikijiandaa kukubali uteuzi ama kukataa. Hiyo itatokana na michango yenu na majibu ambayo yatanihakikishia usalama wa maisha yangu mara mkataba utakapoisha.
 
Ni marekebisho ya katiba yanatakikana,lakini je nani atakibali kubadilisha katiba ikiwa Wabunge wenyewe hawataki katiba kubadilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom