Is President Kagame behind General Imran Kombe's assasination?

Kilichompata imran kombe kitampata Apson pia,time will tell.Kagame mnampa uwezo mkubwa ambao hana,naona hata yeye wakati mungine anawashangaa!
 
Na kila siku iendayo kwa Mungu huwa ninaomba atujaalie Makagame japo wawili tu,mmoja aende Somalia na wa pili aje Tanzania ili kumaliza porojo za mitaani na kurudisha watu katika utekelezaji wa majukumu ya ujenzi wa nchi na kuondoa uzembe usio na maana
Kagame uliekua unaombea aje Tanzania ndio tayari kaja, au bado unamuomba Mungu?
 
Nasikia hata vifo vya kina Sokoine, Kolimba na Nyerere, Kagame alihusika sana, huyu mtu ni hatari sana inabidi serikali imwangalie kwa karibu na ikibidi kufanya mipango ya kumwondoa pale, kale kanchi kadogo sana tukiamua kukachukua ni siku moja tuu.
That monents kagame was nothing na alikuwa bado kijana mdogo. Najua watanzania sisi wajinha to maxmum tunasema tu vitu haya hatuvijui, unakita mtu mshipa umemtoka pima.anasimulia.
 
Kagame uliekua unaombea aje Tanzania ndio tayari kaja, au bado unamuomba Mungu?
Umeikurupua wapi hii post madam? Yaani nikikueleza ninavyoshukuru hutoamini. Na hata nikikueleza yaliyonikuta wakati ninamkampeinia mwaka 2015 hutoamini vilevile. Ila kikubwa ni kuwa nimeshukuru na kufurahi mno kwa kumpata Kagame wetu.
 
Tatizo letu tunajua sana kuongea,utekelezaji ni sifuri.Hainiingii akilini kuwa Kagame alihusika na mauaji ya Kombe hata kama habari hiyo itakuwa imetoka CIA.Iliwezekana vipi kwa yeye kupenyeza majasusi wake mpaka wakapanga njama na kutekeleza mauaji hayo bila ya sisi wenyewe kugundua njama hizo.Na kama aliweza kutekeleza yote hayo bila ya watu wetu wa usalama kugundua basi kuna haja tena ya haraka kuunda upya mfumo wetu wa usalama wa Taifa ili tuepukane na mabaya yanayoweza kuja kujitokeza nchini mwetu zaidi ya suala la kifo cha Imran.Kwa mtazamo wangu ninaona kuwa haya yote yanatokana na maadui wa Kagame ambao bado wako katika zama zao za uhutu na utusi na wameshindwa kumkabili huyu jamaa na hivyo kutafuta njia mbadala ya kumchonganisha na jirani zake ili wasaidiwe katika kumkabili na hivyo kumuondoa madarakani ili kuendeleza sera zao za kibaguzi.Ni nani ambaye hajui na haoni kasi ya maendeleo iliyopo nchini Rwanda kwa sasa hivi?Mwacheni ajenge nchi yake sababu kwa hali ilipokuwa imefikia nchini Rwanda kama si kwa yeye kujitokeza ninaamini kabisa hali ingekuwa mbaya zaidi ya yale tuliyoshuhudia.Na kila siku iendayo kwa Mungu huwa ninaomba atujaalie Makagame japo wawili tu,mmoja aende Somalia na wa pili aje Tanzania ili kumaliza porojo za mitaani na kurudisha watu katika utekelezaji wa majukumu ya ujenzi wa nchi na kuondoa uzembe usio na maana unaorudisha nyuma maendeleo kwa kisingizio cha demokrasia(Tanzania) na huyu sio wa ukoo wangu(Somalia)Mchawi wetu tunaye wenyewe,tusijaribu kufuata mambo ya nchi jirani kuficha matatizo yetu.I stand to be challenged.
Maombi yako yamejibiwa mkuu
 
Asee hii ni post yangu mkuu? Asante sana mkuu kwa kunirudishia post hii na maombi niliyotoa..Binafsi alipopatikana huyu Kagame wetu hata upinzani niliuona hauna faida..
Huyu jamaa ameuvaa upinzani haswa na kuamua kwenda maili nyingi zaid ya PK. Tuombe Mungu dhamira yake ya dhati juu ya taifa hili itimie.
 
Ukimalizana na Kagame rudi huku muulize Kikwete yuko wapi Daudi Mwangosi???

Yuko wapi Ally Zona aliyechomwa na kitu Kikali pale round about ya Msanvu - Morogoro??

Yuko wapi yule Mama Mjamzito aliyepigwa risasi na polisi wa Mtwara wakati hakuwepo kwenye maandamano ya kudai gesi??
Huyo siku hizi ni malaika bana ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kagame anajua anachokifanya, usidhani TISS haina watu wenye akili, tatizo ni namna inavyowa-utilise, afisa wa usalama haendi na wakati, nchi hii inavichwa sema kubweteka kwa taasisi kutokana na kufanya kazi kwa mazoea:A S embarassed:

Wanasiasa ndio wanayo iharibu Tiss, Tukiweza kutofautisha TISS na CCM basi TISS itakuwa bora kuliko wakati wote
 
Back
Top Bottom