GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 390
- 392
Wana JF najua wengi mnaweza kushangazwa na topic hii, lakini sina lengo la kukufuru hapa bali tujadili kama great thinkers. Nimeangalia na kutathmini maisha yetu ya kila siku. Jiulize kuhusu huu umaskini jinsi unavyokithiri kila kukicha huku wachache wenye pesa wakiendelea kula bata. Ukichunguza wengi wenye pesa hawakuipata kiuhalali, viongozi wadhalimu wanaendelea kushika madaraka huku viongozi wa dini wakiwapaka mafuta na kutusihi kuwa wavumilivu wa kisiasa. Hivi Mungu haoni udhalimu huu? Je tuliumbwa ili baadhi tuwe maskini na wengine wawe matajiri peke yao? Nini mpango wa Mungu katika mwili wa viumbe wake? Je ni nani wana nafasi kubwa ya kwenda mbinguni kati ya tajiri na maskini? Kama ni tajiri mbona wengi wao ni wadhalimu? kama ni maskini mbona wengi wao ndo wakosaji wakubwa? Katika maisha yetu ya kila siku tumtafute Mungu kwanza ili tuwe na maisha mazuri au tutafute maisha mazuri ili tumjue Mungu? Maisha hayana budi kuendelea ila umaskini ni kikwazo kikubwa sana. Nawasilisha wadau.