Is it that the world is not fair or God does not exist.

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
277
250
Wana JF najua wengi mnaweza kushangazwa na topic hii, lakini sina lengo la kukufuru hapa bali tujadili kama great thinkers. Nimeangalia na kutathmini maisha yetu ya kila siku. Jiulize kuhusu huu umaskini jinsi unavyokithiri kila kukicha huku wachache wenye pesa wakiendelea kula bata. Ukichunguza wengi wenye pesa hawakuipata kiuhalali, viongozi wadhalimu wanaendelea kushika madaraka huku viongozi wa dini wakiwapaka mafuta na kutusihi kuwa wavumilivu wa kisiasa. Hivi Mungu haoni udhalimu huu? Je tuliumbwa ili baadhi tuwe maskini na wengine wawe matajiri peke yao? Nini mpango wa Mungu katika mwili wa viumbe wake? Je ni nani wana nafasi kubwa ya kwenda mbinguni kati ya tajiri na maskini? Kama ni tajiri mbona wengi wao ni wadhalimu? kama ni maskini mbona wengi wao ndo wakosaji wakubwa? Katika maisha yetu ya kila siku tumtafute Mungu kwanza ili tuwe na maisha mazuri au tutafute maisha mazuri ili tumjue Mungu? Maisha hayana budi kuendelea ila umaskini ni kikwazo kikubwa sana. Nawasilisha wadau.
 
Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,308
2,000
kama sijakosea kuna maandiko yanasema "ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza mbele yangu na kuziacha njia zao mbaya, nami nitasikia kutoka mbinguni na kuiponya nchi yao" mwenye huo mstari anaweza kunisahihisha
 
Abdulhalim

JF-Expert Member
Jul 20, 2007
16,725
2,000
Ukiona haki ipo mbele yako, itwae. Ukianza kujiuliza habari za Mungu, sijui nini utaishia kuchanganyikiwa tu.
 
Kaka Sam

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
540
0
kama sijakosea kuna maandiko yanasema "ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza mbele yangu na kuziacha njia zao mbaya, nami nitasikia kutoka mbinguni na kuiponya nchi yao" mwenye huo mstari anaweza kunisahihisha

Huo mstari uko sahihi preta kama sikosei jana ulienda church...!

Mungu ni wa wote na hana upendeleo na kila jambo linalotokea chini ya jua lina makusudi maalum mbele za Mungu, yaani ili utukufu wake udhihirike mbele yetu na wasio mwamini wamwamini...! japo kuna wabishi....!

Neno la Mungu linasema ni rahisi NGAMIA kupenya katika tundu la sindano kuliko TAJIRI kuingia katika ufalme wa mbinguni... hii ni kweli watu wengi ambao wamejitosheleza kwa kila namna ya dunia hawaoni haja ya KUJINYENYEKESHA mbele za Mungu, huku niliko watu hawaendi church its only wazee na vijana wachache walio jitoa... na wengine ni culture kwao kwenda church... wengine hawajui nini maana ya PRAYER/MAOMBI...

YESU atarudi pale ambapo kila sikio litaskia neno la Mungu ili kusiwepo na awae yeyote atakaesema mimi sikuskia habari zake....

Mwenye sikio na asikie na mwenye macho aone.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,494
2,000
I say god does not exist, and that is why the world is not fair. It is inconceivable that there exists a just, all powerful god who made a world that is inherently unjust, with the law of the jungle ruling practically all over nature.

Ndiyo maana wajanja wakasema "God helps those who help themselves". Hii ni aina ya kidiplomasia tu ya kusema "look after yourself, god does not exist".

Mungu mwenye upendo na nguvu zote angekuwepo angewezaje kuwapelekea maskini WaHaiti majanga baada ya majanga? Mara matetemeko ya ardhi, mara cholera ?
 
Mkuu japo ckuungi mkono ktk kutokuwepo kwa Mungu ila nakubaliana na wewe hasa ktk suala la matatizo. Wakatoliki wanatufundisha kuwa mwili ni hekalu na kristo ni kichwa chake, lakini kwa nini hekalu hili limeumbiwa magonjwa yasiyo na idadi? Na mahekalu yaliyo mengi ni maskini hivyo yanapigwa na kila aina ya ugonjwa. Maskini wanahangaika juani kutafuta maisha ila hakuna wanachoambulia. Tunahitaji kumjua Mungu zaidi ya hapa ili kuijua ile kweli vinginevyo tupo katika kiza kinene.
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,966
2,000
"Hakika nawaambia, ni vigumu kwa tajiri kuuona ufalme wa mbinguni kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano"
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,494
2,000
Mkuu japo ckuungi mkono ktk kutokuwepo kwa Mungu ila nakubaliana na wewe hasa ktk suala la matatizo. Wakatoliki wanatufundisha kuwa mwili ni hekalu na kristo ni kichwa chake, lakini kwa nini hekalu hili limeumbiwa magonjwa yasiyo na idadi? Na mahekalu yaliyo mengi ni maskini hivyo yanapigwa na kila aina ya ugonjwa. Maskini wanahangaika juani kutafuta maisha ila hakuna wanachoambulia. Tunahitaji kumjua Mungu zaidi ya hapa ili kuijua ile kweli vinginevyo tupo katika kiza kinene.

Swali hapa, kama mungu ana uwezo wote, maana yake alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na magonjwa.

Kama mungu ana upendo wa juu kabisa usio kifani, angetupenda kiasi cha kutaka tusiwe na magonjwa.

Kwa sababu tuna ulimwengu wenye magonjwa, either mungu alitaka kuumba ulimwengu usio na magonjwa, akashindwa. Au pengine mungu aliweza kuumba ulimwengu usio na magonjwa, hakutaka tu.

Kama unaamini mungu ana uwezo na upendo usio kifani, la kwanza hapo juu lina tatizo kwa sababu linatuambia mungu hana uwezo wote.

La pili lina tatizo kwa sababu linatuambia mungu hana upendo usio kifani.

All in all, mungu mwenye uwezo wote na upendo usio kifani ni wa kufikirika tu.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,819
0
Huwezi kutaka complete free will kisha ukataka mungu aingilie shughuli zako
 
Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
1,250
kama sijakosea kuna maandiko yanasema "ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza mbele yangu na kuziacha njia zao mbaya, nami nitasikia kutoka mbinguni na kuiponya nchi yao" mwenye huo mstari anaweza kunisahihisha

duh, preta uko deep!!!!!!!!!!!!!!!!......... ubarikiwe na bwana..................
 
Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
1,250
I say god does not exist, and that is why the world is not fair. It is inconceivable that there exists a just, all powerful god who made a world that is inherently unjust, with the law of the jungle ruling practically all over nature.

Ndiyo maana wajanja wakasema "God helps those who help themselves". Hii ni aina ya kidiplomasia tu ya kusema "look after yourself, god does not exist".

Mungu mwenye upendo na nguvu zote angekuwepo angewezaje kuwapelekea maskini WaHaiti majanga baada ya majanga? Mara matetemeko ya ardhi, mara cholera ?

Now that is the definition of unfair.

Swali hapa, kama mungu ana uwezo wote, maana yake alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na magonjwa.

Kama mungu ana upendo wa juu kabisa usio kifani, angetupenda kiasi cha kutaka tusiwe na magonjwa.

Kwa sababu tuna ulimwengu wenye magonjwa, either mungu alitaka kuumba ulimwengu usio na magonjwa, akashindwa. Au pengine mungu aliweza kuumba ulimwengu usio na magonjwa, hakutaka tu.

Kama unaamini mungu ana uwezo na upendo usio kifani, la kwanza hapo juu lina tatizo kwa sababu linatuambia mungu hana uwezo wote.

La pili lina tatizo kwa sababu linatuambia mungu hana upendo usio kifani.

All in all, mungu mwenye uwezo wote na upendo usio kifani ni wa kufikirika tu.

Yeah, kama kafanya makusudi kuingia mbinguni kuwe kugumu namna hiyo kwa tajiri huoni kwamba hayuko fair ?

hii topic itamfanya kiranga atoboe keyboard yake kwa kubofya manake anapenda sana kuiabudu na kuitukuza miungu wake yaani wanafalsafa.......... so maswali na analysisi zooote yeye hana hata neno moja hapo amablao ni wazo lake.......... yooote, alisoma sijui kwa philosofa gani.... hao ndio miungu yake.............

God does realy exist.........only great minds appreciate.............. simple minds find it unconceivable!!!!!!!!!!!!. kaazi kwelikweli................
 
Sasa wewe ndiye umeleta analysis ?

Na wewe unayesema mimi sina kipya chako kipya ni kipi? Kusema mungu ana exist bila kutetea hoja ndiyo kitu kipya?

Maswali ya juu hapo ni ya msingi na hayajapata majibu.

Tuna maovu kwa sababu mungu hakuweza kuumba ulimwengu usio maovu au aliweza ila hakutaka tu ?
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,592
2,000
Kiranga, you want God to always abrogate the law of cause and effect e.g. by giving maisha bora kwa kila Mtanzania in the midst of Ufisadi?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,494
2,000
Kiranga, you God to always abrogate the law of cause and effect e.g. by giving maisha bora kwa kila Mtanzania in the midst of Ufisadi?

Hii sentensi inahitaji mabadiliko, haijakaa sawa kisarufi.Haieleweki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom