wadau nisaidie nilikuwa na uhusiano na dada mmoja kitaa yapata miezi 5 sasa.tulipendana sana tena sana na alikuwa ananza kuchukua nafasi katika moyo wangu. ila kwa bahati mbaya mm sina kazi kwa sasa, nayeye analitambua hilo na amekuwa sehemu yakunitia moyo kuwa utapata ila pamoja nakutambua hilo amekuwa akieleza matatizo furani ambayo kwangu mimi yanakuwa juu ya uwezo kwani sina kitu mfukoni. Tumekuwa tukisaidiana pale mikono inapofikia kujikuna. Tumekuwa tukipishana wakati mwingine ila mimi nilichukulia kama sehemu ya mahusiano kwani haiwezi kuwa furaha muda wote.kuna wakati anakuwa mkali kupita maelezo na kukasilika ovyo ovyo huka akinuna na nilifikia wakati kumwambia kuwa anahasira zakipuuzi.kawa mzito kuomba msamaha hata akikosea ila imenipasa niombe msamaha hata kama yeye kakosea......ila wiki lilopita nikasema enough is enough,uvumilivu umeniishia...aliniona nadada mmoja jirani tuemeongozana naye kwenda dukani,basi kasema ninauhusiano naye,kanuna nakuniuliza maswali yasiyo natija....katika kujibizana kwenye simu hatimaye kasema endelea naye huyo mdada na mimi yeye nimuache.....namimi nikamua kumshukuru kwa kauli yake nakumtakia maisha mema kwani hata siku zanyuma tulipishana kidogo akasema tuachane mm nilimhoji mbona sababu sioni.kwa sasa nikabaini kuwa huyu kunamtu anamsumbua wacha aende namm niruidi hali yangu yaawali kwani atapatikana wakufanana nami ila naona kama anajilaumu maamuzi yake namm nimekaza uzi hata siwezi rudi kwake.