Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,324
- 67
Siri ya polisi yafichuka
2007-11-29 10:33:01
Na Lucy Lyatuu
Sakata la askari polisi walioua na kuwajeruhi raia jijini Dar es Salaam, limeingia sura mpya baada ya mmoja wa aliyejeruhiwa katika tukio hilo, kupinga waziwazi taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana.
Katika tukio hilo lililotokea juzi, mtu mmoja, aliuawa na polisi kwa kupigwa risasi na wengine wawili ambao ni ndugu, kujeruhiwa mmoja wao kuvunjwa mguu wake wa kushoto.
Raia aliyeuawa katika tukio hilo lililotokea eneo la Kiwalani, Minazi Mirefu, jijini Dar es Salaam ni Thomas Mwingira (23) na majeruhi ni Consolata Mwingira (40).
Bi. Consolata alipigwa risasi na kuvunjika mguu wake wa kushoto.
Mwingine ni ndugu yake, Joyce Mwingira (15) mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Yombo Bwawani ambaye pia alijeruhiwa katika mguu wake wa kulia.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana aliwataja askari waliohusika katika tukio hilo ni F 7808 PC William, F 5870 PC Rashid na F 7868 PC Marks ambao wote walitiwa mbaroni.
Kamanda Tibaigana alisema askari hao wakiwa katika doria ya kawaida eneo hilo, walikuta kundi la vijana likicheza kamari na walipotaka kuwakamata, walianza kuwarushia polisi mawe.
Alisema katika hali hiyo, polisi hao walilazimika kufyatua risasi 18 hewani ambapo moja ilimpata marehemu Mwingira na nyingine kuwajeruhi Consolata na Joyce.
Hata hivyo, akisimulia mkasa mzima kuhusiana na sakata hilo, dada wa marehemu Bi. Consolata ambaye amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), alisema maelezo yaliyotolewa na Kamanda Tibaigana kwa vyombo vya habari, yalificha ukweli halisi wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa majeruhi huyo, kisa cha polisi hao kufanya mauaji hayo, kinaonekana kilikuwa ni cha kulipiza kisasi kwa marehemu na waliojeruhiwa.
Akielezea kwa kina suala hilo akiwa kitandani wodi namba 21 MOI, Bi. Mwingira (40) alisema, kwanza yeye hakutoka ndani na kwenda kumng?ata askari katika sehemu yake ya nyonga na hivyo kumfanya ampige risasi.
Alidai kuwa, chanzo cha mgogoro huo, ni baada ya askari wawili kufika eneo hilo kwa lengo la kulipiza kisasi kutokana na hasira iliyojengeka kati yao wakidai kuwa, marehemu aliwahi kupigana na polisi.
"Ni tukio lililotokea kama miezi miwili ama mitatu iliyopita, ambapo walifika askari wawili katika eneo hilo na kudai kuwa, marehemu na wenzake wawili, ni wavuta bangi", alisema.
Aliongeza kuwa, kauli hiyo ilipingwa na watuhumiwa hao na baadaye walianza kurushiana makonde na hatimaye askari hao kuondoka eneo hilo.
Bi. Consolata alisema, baada ya tukio hilo, ndipo juzi askari wawili mmoja akiwa amevaa kiraia na mwingine sare, walipokwenda eneo hilo la tukio.
Alisema baada ya kufika hapo, yule askari aliyekuwa amevaa kiraia, alimnyoonyeshea mdogo wake (marehemu) kidole kuwa, ndiye yeye aliyempiga askari.
?Walimkuta mdogo wangu amekaa juu ya karo la choo, ndipo aliponyooshewa kidole kuwa, ndiye aliyepigana na askari, ndipo walipomkamata na kuanza kumpiga,? alisema Bi. Consolata.
Aliongeza kuwa, baba wa marehemu aliposikia vurugu hizo, alitoka ndani na kuwasihi polisi hao kuwa, kama ni mtuhumiwa, ni vyema wamkamate na kumpeleka kituoni badala ya kumpiga.
Aidha, alisema wakati hayo yakiendelea nje, yeye (Consolata) alikuwa ndani, na ndipo alipotoka na kukuta askari hao wakimpiga mdogo wake makofi na kuchana nguo zake.
Alisema, aliwauliza polisi hao kiini cha kufanya hivyo lakini badala ya kujibiwa, naye alipigwa kofi na mmoja wa askari hao huku akimpasha kwamba, anatetea ujinga na kuendelea kufyatua risasi juu.
Alisema hatua hiyo ilimfanya mdogo wake aingiwe na woga na kutaka kuondoka eneo hilo.
Hata hivyo, alisema wakati akimkimbilia kwenda kumuokoa, ndipo askari huyo alipompiga risasi mbili katika mguu wake wa kushoto.
?Wakati nikiugulia maumivu pale chini, ndipo mmoja wa askari alipita pembeni yangu akimfuata mdogo wangu, nami nikamng?ata mguu na sio nyonga,? alisema Bi. Consolata.
Kwa mujibu wa Kamanda Tibaigana, alisema askari hao walitumia bunduki mbili za aina ya Sub Machine Gun (SMG).
Alisema kutokana na tukio hilo, askari hao kwa sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku kukiwa na timu ya watu sita iliyoundwa kuchunguza juu ya tukio hilo ili sheria zaidi iweze kuchukuliwa.
Alisema timu hiyo imeanza kazi rasmi jana na kwamba imetakiwa kukamilisha uchunguzi wake na kutoa majibu ifikapo Desemba 7, mwaka huu.
Timu hiyo inaundwa na watu sita, watatu kati yao ni maofisa wa polisi, wawili kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na mmoja kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
SOURCE: Nipashe