Is Bakari Kitwana a Tanzanian?

AmaniGK

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,153
380
Members hasa kwenye masuala ya Enternteinment nina swali?
Hivi Bakari Kitwana aliyeandika "Why white Kids Love Hip Hop" ni wa kwetu?

Kama kuna mwenye details zake animwagie
 
Bakari Kitwana si Mtanzania. Ni matunda ya "Civil Rights Movement" za miaka ya 60 na 70. Jamaa zetu wenye mwelekeo wa siasa kali kama vile "Black Pathers" waliamua kuchukua majina ya Kiafrika na kuasili Kiswahili kama lugha yao, kwa kuwa majina ya Kizungu na Kiingereza kwao ilikuwa ni vya kitumwa. Wengi walichukua majina ya Kiafrika na wakajifunza Kiswahili. Watu kama kina Dr. Maulana Karenga, Amir Baraka, Jamaldeen Tacuma, Assata Shakur (mama´ke Tupac Shakur R.I.P), Sundiata Acoli, Kamau Sadiki (a.k.a Fred W. X. Hilton), Dhoruba Bin Wahad, Mumia Abu Jamal, n.k. walibadili majina

Angalia:

http://en.wikipedia.org/wiki/Kwanzaa

http://www.officialkwanzaawebsite.org/index.shtml


Wako,
Mosi-O-Tunya
 
Ushamsikia Dk. Haki Madhubuti (formely Don L. Lee)? Naye ndiyo hao waliokataa majina ya kitumwa.

Halafu utacheza sisi Waafrika wenyewe ndiyo tunajipa majina ya kizungu, lol.
 
Ushamsikia Dk. Haki Madhubuti (formely Don L. Lee)? Naye ndiyo hao waliokataa majina ya kitumwa.

Halafu utacheza sisi Waafrika wenyewe ndiyo tunajipa majina ya kizungu, lol.

Usipokua na jina la kidhungu hupati interview lol. Wengine majina yetu inabidi ukifika kati upumzike, unywe maji halafu uendelee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom