Is allah a muslim god??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is allah a muslim god???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abunwasi, Dec 24, 2009.

 1. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Recently there has been a lot of talk about Allah being a muslim God to the extend that some members going below the belt [insultive].
  My firm belief is that JF offers us with opportunity to discuss/debate issues logically[no jazba] In view of this i would like to educate all non muslims what ALLAH really means
  Actually the word Allah is the perfect descripton of Oness of GOD for both Jews Christians and Muslim.
  The word Allah was used by early christian arabs and jewish arabs well before Islam.
  In arabic bible on page 1 of Genesis in the Old Testament the word Allah is mentioned 17 times.
  Actually Allah comes from the word Elaha.
  For a muslim the best definition of Allah is “The one and only. The eternal, the absolute. He begets not, nor is He begotten And there is none like Him”.
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  I think you didn't expect him to be called MUNGU in the arabic environment.

  When it comes to JAZBA....... it is very obvious......who are the most JAZBIAS..tehe...teheee
   
 3. maringeni

  maringeni JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2017
  Joined: Oct 8, 2013
  Messages: 2,838
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Allah alitokea wapi?

  Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale.

  Je, jambo hilo ni kweli?

  Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

  Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?

  Asili Ya Allah
  Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.
  Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.
  Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.
  Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.
  Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.
  Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).
  Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:
  'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."
  Yaani.
  Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.
  Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo, al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’. Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’
  Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walik uwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.
  Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwa Allah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.
  Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.
  Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?
  Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.
  Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?
  Tunasoma hivi:
  Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
  Yaani:
  Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.
  Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
  Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
  Kwa mfano:
  Yoshua – Yahwe ni wokovu;
  Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
  Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
  Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
  Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
  Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
  Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.
  Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).
  Tunaambiwa kwamba:
  An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).
  Maana yake:
  Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Qura aish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.
  Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).
  Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake,….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).
  Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).
  Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).
  Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5)..............................................Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.
  Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.
  Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba. Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:
  "The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."
  Yaani.Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."
  Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.
  Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?
  Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.
  Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:
  "Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up.
  "Yaani:
  Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
  Swali ni kuwa:
  Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.
  Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?
  Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).
  Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!Hitimisho
  Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu?
  Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze? Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe? Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota? Ni nini asili ya vitu hivyo?

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 4. f

  finyango JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2017
  Joined: Aug 11, 2016
  Messages: 1,673
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Ile miezi siku hizi haipo

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 5. itara

  itara JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2017
  Joined: Aug 10, 2013
  Messages: 1,881
  Likes Received: 932
  Trophy Points: 280
  mbona kwenye quran kuna pingwa kuabdiwa kisichukua Allah,pia ambaye hakuzaaa wala hakuzaliwa na asiye na mfano kitu chochote..(qur 112:1-4)

  mkuu hebu jaribu kupitia vitabu vya waislam vinavyohusu 'tauhidi'.au jaribu kupitia site za kiislam online ili ujiridhishe nafsi yako huenda unahitaji kupata kuelimika..huenda ukawa umeongolewa..na pia ufanye kiutafiti kuwa ni kwanini basi waislamu wana lugha moja duniani ya kuabdia, wana aina moja ya kuabudu, wana uelekeo mmoja wakufanya ibada, wana mavazi ya namna moja na utamaduni mmoja..

  kuhusu totem au mwezi na nyota hilo halikuwa kipindi cha muhammad hata kina emil durkheim na wenzao wanayajua hayo, labda hao wana symbolic wanajua ni kwanini.
  ni hivyo tu.
   
 6. T

  Tabby JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,881
  Likes Received: 5,477
  Trophy Points: 280
  No he isn't. He even never proclaimed to be and neither his assistant mohamed did.
   
 7. T

  Tabby JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,881
  Likes Received: 5,477
  Trophy Points: 280
  Ni mfalme yupi aliyetaka watu wake wasiusifu ufalme wake na wamsifu mwingine? Wewe uko hapa, jaribu sikumoja kumponda sizonje halafu umsifie mwingine uone kama hujajikuta usipopajua.

  Miungu na mizimu yote hulazimisha watu waliochini ya himaya yake kuiamini na kuiabudu tena kwa lazima. Bila kuwa na Mungu, shetani analazimisha hata kwa mateso ili watu wamwabudu yeye. Iweje mohaemdi mwasisi wa qurani asilazimishe watu kumwabudu mungu wake na zi mwingine? Ila haahla si Mungu na hajawahi kusema yeye ni Mungu, na hata mohamed amesema "hakuna Mungu", ila kuna alaah tu na kwa maana hiyo, alitaka watu waone mwisho allha wasiende zaidi kujua kuna Mungu.
   
 8. The Businessman

  The Businessman JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 6,997
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Tumsifu Yesu Kristo
   
 9. ArD67

  ArD67 JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 14, 2016
  Messages: 2,450
  Likes Received: 1,668
  Trophy Points: 280
  Ni moja ya thread nzuri ktk maswala ya imani hii, Mkuu Maringeni, umetoa hoja za msingi ktk ubora wake kabisa. Apaswaye kuzipinga aje na hoja kinzani na hizo si vya kuambiwa au kukaririshwa na wenye matakwa yao.

  Lakini Mkuu, Maringeni, wewe umeegemea pia ktk wanavyotufundisha na kutuaminisha tu, tutoke nje ya mabox ya vitabu hivyo kidogo... Haswa ktk swala la upagani na imani juu ya hilo. Mungu na miungu, ulimwenguni kote ktk jamii zote wanaamini ktk Mungu mmoja, the creator. Miungu ni yote yenye nguvu kupita nguvu za kibinadamu zenye asili toka ASILI kuu, God the Creator. Mfano wa jamii zenye Mungu na miungu yake ni wahindi, waislamu na Wakristu wa hata leo.

  Ukifatilia imani ya miungu kama nilivyonyambulisha hapo juu, huwa na nguvu ktk utendaji fulani wa kipekee kwake tu, mfano mungu wa mvua, kizazi, uponyaji, mavuno nk. Ktk Ukristu hii miungu hujulikana kama ni Malaika, eg Gabriel, Rafael nk Jibril, Izrail nk na ktk ubudha pia wako na yuko the Creator pia.

  Nionavyo mimi, kipimo sahihi cha Mungu yupi ndiye sahihi zaidi kuabudiwa ni kuangalia sifa kuu ya Mungu Muumbaji Mkuu, Mungu ni UPENDO, Mungu wa kweli atafungamanishwa na UPENDO wa ajabu, ulio thabiti. Ndio maana karibia dunia yote, Golden rules zao zinajikita ktk kuutangaza ukweli wa Mungu, UPENDO. Ubuntu, Ukristu na hata Ubudha pia. Vinginevyo, Hongera Mkuu kwa elimu uliyotupatia itakayo tusaidia kuikaribia Kweli.

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 10. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Uzi kama huu upo hapa naona mtu kaukopy kaja na andiko leefuu wakati lipo katika uzi uliopo ndani JamiiForums #mods unganisheni huu uzi.

  Mobile Traveller
   
Loading...