Is Africa really rising? - Ali Mufuluki

Kontoro

Member
Apr 24, 2020
20
42
Miaka sita (6) iliyopita mfanyabiashara nguli wa Tanzania marehemu Ali Mufuluki katika kipindi cha TED talk show, alikuja na mada fikirishi ikiwa na title ya Afrika is really rising?


Katika hii video aliongelea mambo mengi sana kuhusiana na maendeleo ya bara letu. Mimi nitajikita katika jambo moja ambalo aligusia katika gunduzi za raslimali zinazofanyika Africa na utata wake.

Aliongelea ugunduzi wa almasi za Geita takribani miaka zaidi ya hamsini(50) iliyopita. Mwanamadini Williamson kutoka ulaya alifika Geita akakuta Wasukuma wanacheza mchezo wa bao kwa kutumia Almasi. Hii inamaanisha wenyeji walikuwa na utajiri mwingi ila hawakujua thamani yake. Alichokifanya Williumson ni kununua hilo eneo na kuomba ulinzi toka kwa chief, akaanza kuchimba almasi, akawajengea nyumba nzuri machief, akawasomesha watoto wa machief na kufanya vitu vingine vingi ili kuwalidhisha watawala wa pale. Mwishowe alikufa akiwa tajiri mkubwa Afrika.

Alichokifanya Williumson miaka 50 iliyopita, hakina tofauti na kinachofanyika katika gunduzi za raslimali kipindi hiki barani Afrika hasa hasa gunduzi za mafuta, gesi na madini. Waafrika bado hatujui thamani ya raslimali zetu, tunaingia kwenye mikataba mibovu na wawekezaji, wanatunyonya mpaka hatunufaiki na chochote.

Dunia ya sasa inaelekea katika kitu kinachoitwa 4th industrial revolution-related technologies. Hapa ndo patamu sasa. Tanzania imeibuka kinara kuwa na madini yanayo support hayo maendeleo ikiwa na zaidi ya tani 500,000 za nikeli, tani 75,000 za kopa na tani 45,000 za Kobalti. Nikeli ambayo inathamani kubwa inapatikana katika mpaka wa Tanzania na Burundi eneo liitwalo Kabanga.

Hayo madini ndiyo yanayotumika kutengeneza betri na vifaaa vitakavyotumika katika mapinduzi hayo ya teknolojia. Ukiachana na betri za simu, laptops na vifaa vingine vya kielektroniki, biashara kubwa ya hayo madini ni kutengeneza betri za magari ambapo kwa sasa makampuni makubwa ya magari duniani yakiongozwa na kampuni ya Tesla, yanatengeneza magari ya umeme na yana soko kubwa sana.

Natamani ugunduzi wa hayo madini Tanzania Usiwe na tofauti Na ugunduzi wa mafuta uarabuni, ambapo waarabu waliweza kuokoa vizazi vyao kiuchumi.

Je, ni mzarendo gani ataweza pigania hizi raslimali zetu kutoka katika mikono ya mabeberu?

Hizi raslimali mpya zimeishaondoka na viongozi wakuu wa nchi wawili na sababu kubwa ikiwa ni wao kuwa mstari wa mbele katika kutetea maslai na kulinda raslimali zetu. Mungu awapumzishe kwa Amani, Juhudi zenu za dhati kulinda raslimali za Kabanga tumeziona, tutazienzi na tutaendelea kuzipigania.

Soma hii pia: Tanzania's Late President Magufuli: 'Science Denier' or Threat to Empire? - unlimitedhangout.com
 
Back
Top Bottom