3D.
JF-Expert Member
- Sep 7, 2010
- 1,018
- 282
Usiwe na jazba Kiranga
SI unit ni Standard Measuremnt Unit.
hayo mambo ya troy pounds na avoirdupois pounds unayoyasema unaweza kuyafafanua kimahesabu? unaweza kufanya conversion zake. Umewai kufanya calcculation ya physics kwenye uzito wa punds?
Ndio maana kukawepo kuna kitu kinaitwa SI unit inayokubalika kimataifa. Ukisema umbali wa kutoka eneo A to B ni yards 600 hiyo siyo SI unit inayokubalika labda kwa hao waingereza
So tell us when u critically challenge others people's ideas, comments and views who died and made u chef?
Hata uki google kitu usichukue kizima kizima kama kilivyo.
Nakubaliana nawe. Hata hivyo nashangaa kidogo kuwa suala hili linaleta mjadala wakati naona liko wazi tu. Anyway, SI unit hupima Heaviness in terms of mass or weight. Kilo 100 za kitu chochote ni sawa kwa uzito na kilo 100 za kitu kingine chochote, full stop. Weight ni namna uzito unavyopimika tegemeana na uvutano (gravitation) uliopo kwenye eneo husika. Weight hupimwa kwa kipimo kiitwacho Newton (N). Hata hivyo kimazungumzo (Si kisayansi) mtu akiuliza what is the weight of this sugar unaweza kujibu 2 kg japo kg ni kwa ajili ya mass, hayo ni mazungumzo tu na inakubalika kukosea hivyo. Sasa, mass ya 2 kg katika eneo fulani lenye uvutano wa 10 m/seq square (tuite tu 10) ni = uvutano x mass = 20 N. Mass hiyo hiyo katika uvutano wa 5 weight yake ni = 2 x 5 = 10 N.
Uvutano unabadilikaje? Maeneo hutofautiana uvutano. Dunia si umbo kama mpira, maana yake kutoka magharibi kwenda mashariki ni parefu kuliko kutoka kaskazini kwenda kusini. Hivyo, ukikaa katika ncha ya kusini na kaskazini unakuwa uko karibu zaidi na kitovu cha dunia (centre of the earth) unakoanzia uvutano kuliko kama ungekuwa pembeni ya dunia yaani maeneo ya ikweta. Hii ina maana kitu hichohicho kimoja kinakuwa na weight kubwa katika north na south pole (ambako kinavutwa sana) kuliko katika ikweta japo mass ni ile ile (mass haizidishwi na gravity) kwa sababu mvutano unapungua maeneo hayo.
Mwezi unavuta (mvutano) kitu kidogo/kidogokidogo hivyo weight ya kitu hichohicho duniani ni kubwa kuliko mwezini na ndo maana ukiliachia yai liangukie jiwe mwezini linaweza lisivunjike kwa sababu linatua polepole lakini duniani likely litavunjika kwa sababu gravitation ya dunia ni kubwa mara sita (navyokumbuka) kuliko ya mwezi. Mvutano wa sayari ya Jupiter ni mkubwa sana kuliko dunia (sijui ni kwa kiasi gani) sija-google. Ukianguka toka mezani duniani hadi sakafuni utachubuka, kwenye jupiter utavunjika mbavu kwa kuwa utaanguka kwa kasi kubwa kweli sababu ya ukubwa wa gravity.
Kuna sehemu angani hakuna uvutano, hivyo ukiachiwa eneo hilo unaweza ukaelea siku zoote na utakufa kwa njaa, baridi na kukosa hewa ya oksijeni na si kwa kuanguka.
Ah, haya nadhani nimeeleweka.