Iringa: Wanafunzi 400 wa Shule ya Msingi hatarini kuhara kutokana na changamoto ya choo kukosa maji

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Wanafunzi zaidi ya 400 wa shule ya msingi Ifwagi, iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wapo hatarini kuugua magonjwa ya kuhara kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya vyoo, hali inayowalazimu baadhi yao kujisaidia ovyo vichakani.

1625725685548.png


Mkuu wa Mkoa wa Iringa atoa majibu, soma hapa chini:
- RC Queen Sendiga ampa wiki mbili DED wa Mufindi kupeleka maji vyoo vya shule ya Msingi Ifwagi
 
Mkuu wa mkoa yupo
Mkuu wa wilaya yupo
Mkurugenzi yupo
Katibu tawala yupo
Afisa elimu yupo
Mbunge yupo
Wazazi mpo
Jitahidini hamjashindwa kujenga hivyo vyoo
 
Halafu eti hela zinaenda kujenga sanamu ya mtu! Nyingine zinatumika kununulia Benzi la Rais Mstaafu, nyingine zinaenda kuwajengea Marais hao hao Wastaafu mahekalu ya kuishi!!

Yaani mtu amehudumu katika nafasi ya ubunge, uwaziri na baadae Urais kwa miaka lukuki, analipwa mafao ya 80% kila mwezi, halafu bado ananunuliwa gari, anajengewa nyumba ya kifahari na bado haitoshi, anajengewa mpaka sanamu!

Hakika Tanzania inahitaji Katiba Mpya haraka iwezekanavyo! Kuna mambo yanaleta sana maudhi.
 
Back
Top Bottom