JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,296
- 5,431
Uongozi wa Kijiji cha Igoda, Kata ya Luhunga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Kampuni ya Foxes Treck kupitia Taasisi ya Foxes Community and Wildlife Conservation (FCWC) kwa kujitolea zaidi ya Tsh milioni 100 kujenga wodi ya wazazi na zahanati.
Akizungumza kijijini hapo mara baada ya mfadhili huyo kutembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Igoda, Laines Sanga alisema kuwa Foxes Treck ambao ni wawezekezaji wazawa katika kijiji hicho wameendelea kusaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo za ujenzi wa miradi ya elimu, afya na miundo mbinu ya barabara ndani ya eneo lao.
Hivyo, alisema wao kama kijiji wanajivunia kuwa na mwekezaji huyo ndani ya eneo lao kwani pamoja na kufanya shughuli zake za uwekezaji ila amekuwa ni nguzo ya maendeleo ya kijiji hicho na vijiji vingine.
"Tunamshukuru sana mfadhili wetu Foxes Treck, kijiji chetu kilikuwa na changamoto ya uhaba wa zahanati ila ameweza kutujengea pamoja na kujenga nyumba za watumishi kwenye kituo hiki pia wana Igoda wanajivunia sana kuwa na mdau wetu wa maendeleo anayetujali wananchi," alisema Sanga.
Kwa upande wake muuguzi mkunga wa zahanati hiyo ya Igoda, Bahati Ndelwa mbali ya kushukuru kuwepo kwenye zahanati hiyo alisema imesaidia sana kupunguza vifo vya akina mama wanaokwenda kujifungua kwani tangu afike kituoni hapo hakujatokea kifo hata kimoja kutokana na huduma nzuri inayotolewa.
Hata hivyo, alisema changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi ambapo kwa sasa kuna watumishi wawili pekee, hivyo ikitokea mmoja ana tatizo inamlazimu mtumishi mmoja kufanya kazi zote.
Hivyo, aliomba serikali kusaidia kuongeza idadi ya watumishi ili kuboresha zaidi huduma.
Meneja wa FCWC, Zilipa Mgeni alisema kuwa kampuni hiyo ya Foxes Treck imeendelea kusaidia miradi mbalimbali katika kata zote tatu za Ihanu, Mdabulo na Luhunga na kuona vijiji vinavyozunguka kampuni hiyo vinasaidia miradi ya kimaendeleo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Foxes Treck, Geoff Foxes alisema kampuni yake inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake, hivyo ndiyo sababu ya kujitolea kujenga zanahati hiyo na nyumba za watumishi.
Hata hivyo, alisema ili huduma ya afya iweze kuboreshwa zaidi ni lazima wahudumu wawepo wa kutosha ambao watasaidia kufanya huduma kuwa bora vinginevyo majengo pasipo watumishi hayatasaidia kuwa na huduma bora za afya .
Aliongeza kuwa lengo la kampuni yake ni kuendelea kuiunga mkono serikali iliyopo madarakani katika kuwahudumia wananchi wanaozunguka kampuni hiyo na kampuni yake itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi pamoja na serikali katika uchangiaji wa miradi ya kimaendeleo.
Source: Matukio Daima Blog