IRINGA: Serikali yapiga marufuku Waganga wa jadi kupewa leseni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amepiga marufuku kutolewa vibalina kuwasajili waganga wa jadi kutokana na ongezeko la waganga hao kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kila uchwao ikiwamo ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo ambapo huenda waganga hao wakawa chanzo.

Mkoa huo,unakadiriwa kuwa una zaidi ya waganga wa jadi 800 waliosajiliwa huku waganga wasio na vibali wakiwa zaidi ya 500 jambo ambalo limetajwa kuwa chanzo cha matukio ya uhalifu hasa ubakaji na ulawiti kwa watoto kwa kile kinachodaiwa waganga hao kupiga ramli chonganishi.

Akizungumza wakati wa kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC ), Hapi alisema sasa umefika mwisho kwa waganga kuendelea kusajiliwa mkoani iringa kwani hawezi kuwa kiongozi wa kuongoza mkoa wa waganga wapiga ramli chonganisha na kusababisha kukatisha uhai wa watoto wasio na hatia.

“Hii kada ya kada ya waganga wa kienyeji nataka kudili nayo na sasa nasitisha utoaji wa leseni kwa waganga wote mkoani Iringa tunataka hizi leseni 800 tuanze kwanza kushughulika nazo ili tujue wapi ni halali na wapi wasio halali kwani wapo watu ambao wanatumia huu mwanya kufanya vitu ambavyo sio sawa ikiwapo kupiga ramli chonganishi zinazokatisha uhai wa watu wetu “

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani hapa kuwachunguza waganga wote wale wanaofanya kazi hiyo bila ya kuwa na vibali halali kutoka serekalini ili hatua ziweze kuchukulia juu yao .

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi amewataka viongozi wa kisiasa na viongozi wa dini kushirikiana kwa pampja kukimea na kuwafichua wanaotenda maovu hayo kwani japo kuwa kuna sheria kali lakini watu wamekuwa wakiendelea kutenda maovu hayo na jamii kuwaficha .

Alisema siku za hivi karibuni vitendo vya uwaji watoto na ubakaji vimekuwa vikiongezeka hivyo ni jukumu la kila mtu wakiwemo wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele kuwalinda watoto.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso ambaye ametumia fulsa hiyo kueleza mikakati ya wizara ya maji katika kumaliza changamoto ya maji kwa wananchi na kuwaonya wahandisi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.
 
Ni vyema kufanya utafiti wa kina kwanza kabla ya kufanya maamuzi.Tatizo hapo SIO Waganga wa jadi.Tatizo ni WAGANGA WASHIRIKINA.Waganga hawa washirikina wakubwa wao ni MASHETANI.Genge hili la mashetani watupu ndio tatizo lenyewe hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom