Iringa: Serikali itawakamata wazazi na wanafamilia wanaoshindwa kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya vitendo vya ubakaji na ulawiti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266
Serikali Mkoani Iringa imesema itawakamata wazazi na wanafamilia wanaoshindwa kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya vitendo vya ubakaji na ulawiti walivyofanyiwa watoto.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati akizungumza na wanahabari juu ya kushamiri kwa vitendo hivyo vinavyochangiwa na wazazi kushindwa kutoa ushirikiano kesi inapofikishwa mahakamani.

“Tuna majalada mengi ambayo wazazi wamekimbia ninakusudia kutoa agizo kwa yale majalada ambayo wazazi walifika mpaka polisi wakaandika maelezo na kugoma kwenda mahakamani tutawakamata wao ili waje watuambie kwanini walikwenda hadi polisi wakaelezea tukio lilivyokuwa halafu hawataki kwenda mahakamani kutoa ushahidi”amesema Sendiga.

Sendiga amewataka waandishi wa habari mkoani humo kusaidia kutoa elimu katika jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia kwakuwa vitendo hivyo vimeshamiri mkoani humo.

“Ni jukumu la kila mwanajamii kusaidia kuelezea na kutoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kutokomeza ukatili huu,hawa tuwalee vizuri na tusiwafanyie vitendo vya kinyama”amesema



Mwananchi
 
Kwani sheria za mwenendo wa mashstaka zikoje juu ya shahidi asiyefika mahakamani baada ya kupata wito wa mahakama? Au ndiyo tuseme nchi hii bila ya matamko sheria hazitekelezeki?
 
Back
Top Bottom