IRINGA: Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi(TSN), Abdul Nondo akutwa na kesi ya kujibu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Mahakama ya Hakimu Mkazi imesema Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi(TSN), Abdul Nondo ana kesi ya kujibu katika shauri linalomkabili

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Liad Chamshama amesema Mahakama imemuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu katika maelezo yake aliyoyatoa kwa Afisa wa Polisi, hivyo anatakiwa kuthibisha ukweli wa maelezo hayo

Aidha, Nondo ataanza kujitetea mahakamani hapo Septemba 18 mwaka huu

Katika kesi hiyo Abdul Nondo anashitakiwa kwa makosa mawili ikiwemo la kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakimu gani?
 
NONDO AKUTWA NA KESI YA KUJIBU, MAHAKAMA YATAKA APELEKE MASHAHIDI WA KUJITETEA

August 27, 2018 Fatma Ally

Mahakama ya Mkoa wa Iringa Leo imetoa uamuzi juu ya kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo kuwa mshitakiwa huyo,ana kesi ya kujibu na hivyo anatakiwa kupeleka mashahidi kwa ajili ya kujitetea.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Liad Chamshana amesema kuwa Nondo amekutwa na hatia kutokana na maelezo yake aliyotoa polisi kuwa alitekwa .

Awali Nondo, alifikishwa mahakamani hapo akiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambapo,shtaka la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa eneo la Ubungo Dar es Salaam na John Dar Mpya: NONDO AKUTWA NA KESI YA KUJIBU , MAHAKAMA YATAKA ALETE MASHAHIDI WA KUJITETEA

Mahakama ya Mkoa wa Iringa Leo imetoa uamuzi juu ya kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo kuwa mshitakiwa huyo,ana kesi ya kujibu na hivyo anatakiwa kupeleka mashahidi kwa ajili ya kujitetea.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Liad Chamshana amesema kuwa Nondo amekutwa na hatia kutokana na maelezo yake aliyotoa polisi kuwa alitekwa .

Awali Nondo, alifikishwa mahakamani hapo akiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambapo,shtaka la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa eneo la Ubungo Dar es Salaam na kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.

Katika shtaka la pili, wakili huyo amesema Nondo ametoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana kutoka Dar es Salaam na kupelekwa kiwanda cha Pareto Mafinga.

Katika kesi hiyo Nondo anatetewa na mawakili wawili wakiongozwa na Jebra kambole chini ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC)
 
Hakuna kesi hapo, hakuna ushahidi wowote kuwa ni Abdu Nondo aliyetuma meseji ya kutekwa mitandaoni!

Wanamsumbua tu kwa sababu ya kutetea haki ya Akwilina!
 
Halafu watu waliomtuma Na kum train huo utoto wa kujiteka wanarudi kulikonoga

Wazazi wasaidie kutuliza mizuka ya Kisiasa ya Vijana wao watakuja kuishia Kama kina Yerricko Yericko Nyerere Kulima Msusa Na viazi vitamu Mbutu Kigamboni wakati waliokuwa wanawatumia wamesharudi Kwa 'Baba na Mama' Na wameteuliwa Kuwa Mabalozi
 
Huyo dogo alifaa atolewa malinda kabisa.

imesomeka!!
Wewe unakinga Mkuu? Muda wowote hata wewe unaweza kujikuta mbele za hakimu na watu watakutakia kama wewe unavyomtakia mabaya huyu dogo.

Mahakama inaepukwa na watu wanne tu mpaka sasa, sisi wengine wote tunaweza kujikuta mahakamani..

Siku zote kuni ya akiba huicheka kuni inayotekea motoni.
 
Halafu watu waliomtuma Na kum train huo utoto wa kujiteka wanarudi kulikonoga

Wazazi wasaidie kutuliza mizuka ya Kisiasa ya Vijana wao watakuja kuishia Kama kina Yerricko Yericko Nyerere Kulima Msusa Na viazi vitamu Mbutu Kigamboni wakati waliokuwa wanawatumia wamesharudi Kwa 'Baba na Mama' Na wameteuliwa Kuwa Mabalozi
vitu vya hovyo hovyo vinampotezea muda. Fungeni kabisa ili wengine wasifate mkumbo, badala ya kupambania mambo yake linavamia siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
ramba watu tigo upate cheo
 
Back
Top Bottom