Iringa: Mwanajeshi alewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,009
2,000

Wananchi Iringa wakimtazama askari wa jeshi ambae jina halikuweza kufahamika aliyekuwa amezima kwa ulevi uliopinduki


mjeshi huyo akiwa akiwa amezimaMjeshi huyo akiwa amepata fahamu baada ya kumwagiwa maji
Mjeshi akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita kiasi


..........................................................................................................

KATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa

Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.

Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.

Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .

Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza

" Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare .....sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja

Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana mambi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa .

Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.
 

mbalila

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
814
250
ulevi ni nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,433
2,000
Jkt!!!!!!!!!!!!???????????????


Kulewa sio ishu,ishu ni kutapika na kujikojolea,hahahaaaa kamanda!!!!!.
 

LENGIO

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
1,092
1,250
Mbona nawewe maboso hukumsamehe?ulivyompiga picha na kuweka hapa tayari umemuaribia kazi,wakubwa zake wapo humu watamfutilia.
 

Mangwelele

Senior Member
Jul 22, 2013
111
195
Askari wa JKT (Serviceman) hawezi kuvaa nguo za JW lakini wa JW anaweza kufanya hivyo
nikweli mkuu wale wote wanaovaa bakabaka ni askar wa jwtz lakin jkt wanavaa zile za kijan zenye madoa meuc mm mwenyewe nimepigia depo hapo mafinga kikoc namba 841 kj
 

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
892
500
Jina "maboso" maana yake lojolojo ya ulanzi.na huyu mwanajeshi asije akawa alipiga ulanzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom