Iringa: Mwanafunzi wa Mwaka wa pili amnyonga mpenziwe wa mwaka wa pili na kutuma ujumbe kwa Wazazi wa Marehemu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
TAARIFA KUTOKA CHUO KIKUU CHA IRINGA

Mwanafunzi.JPG

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa unasikitika kutangaza kifo cha Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza, Mwaka wa Pili Idara ya Uandishi wa Habari PETRONEL P. MWANISAWA kilichotokea siku ya Jumanne, 1/6/2021 hapa mjini Iringa.

Uongozi unawatangazia kuwa kesho Alhamis, 3/6/2021 kutakuwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 8:00 mchana kisha mwili kusafirishwa kwenda Sumbawanga kwa ajili ya mazishi.

Tuungane na Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki katika kuomboleza msiba huu.

Raha Ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie...Apumzike kwa Amani


-----


Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, Petronel Mwanisawa (22) amefariki dunia kwa kunyongwa na mpenzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa, Prudence Patrick (21), ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda Bwire amesema tukio hilo limetokea Juni 1, mwaka huu maeneo ya Kihesa.

Amesema siku ya tukio marehemu hakurudi nyumbani kwao jambo ambalo si kawaida yake, hivyo wazazi wake waliingiwa na hofu na kuanza kumtafuta.

"Marehemu alikuwa anaishi na wazazi wake, na huyu mtuhumiwa yeye alikuwa amepanga. Kwa hiyo siku ya tukio alitoka kwenda chuo, lakini mpaka usiku akawa hajarudi, ndipo wazazi walianza kupata wasiwasi, wakampigia simu rafiki yake lakini hawakufanikiwa," amesema Kamanda Bwire na kuongeza

"Kwa hiyo jana ndo tukampata, na hiyo ni baada ya mtuhumiwa mwenyewe kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa mzazi wa marehemu akisema alikuwa na Petronel na kwamba amefariki. Baada ya hapo hakupatikana tena," alisema.

Amesema baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliripoti kituo cha polisi, ndipo askari walikwenda katika nyumba ya mtuhumiwa na kuukuta mwili wa marehemu.

Bwire amefafanua kuwa, taarifa za awali zinaonyesha binti huyo alinyongwa na mpenzi wake na chanzo ni wivu wa mapenzi.

"Mtuhumiwa tulimkamata njia ya kuelekea Dodoma alipokuwa akijaribu kutoroka na upelelezi wa tukio hilo unaendelea," amesema Kamanda Bwire.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu Cha Iringa Bi Petronel Mwanisawa (21) ameuawa kwa kunyongwa na Mpenzi wake ambaye pia ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuoni hapo

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa Mr Prudence Patrick (22)

Tukio hilo la kusikitisha limetokea maeneo ya Kihesa Iringa na mtuhumiwa alikamatwa njia ya Dodoma akijaribu kutoroka

MCL
 
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Iringa Petronel Mwanisawa ameuawa kwa kunyongwa na Mpenzi wake ambaye pia ni Mwanafunzi mwenzake
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa Prudence Patrick (22)
HAWA vijana wametumwa kufanya mapenzi au kusoma?wazazi kwa kweli tuna kazi kubwa ya kuwalea kwa maadili mema.zile enzi zetu kulikuwa hakuna matukio kama haya.ulikuwa unamaliza chuo hata humjui msichana anafanana na nini lkn siku hizi hawa vijana akili zao zote ni mapenzi.
 
HAWA vijana wametumwa kufanya mapenzi au kusoma?wazazi kwa kweli tuna kazi kubwa ya kuwalea kwa maadili mema.zile enzi zetu kulikuwa hakuna matukio kama haya.ulikuwa unamaliza chuo hata humjui msichana anafanana na nini lkn siku hizi hawa vijana akili zao zote ni mapenzi.
Siku hizi wanapanga chumba mtaani wanaishi kama mke na mume vile..
 
Hili neno, "mapenzi", linakosewa sana matumizi yake. Mapenzi ni kati ya wanandoa tu, nje ya hapo siyo mapenzi bali ni, "zinaa na uasherati".

Jamii yetu inapaswa kubadilika, mfano, kichwa cha habari hii kilipaswa kusomeka hivi; "MWANAFUNZI WA MWAKA WA PILI AMNYONGA MWASHERATI MWENZAKE".
 
Back
Top Bottom