Iringa mjini yanyang’anyiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iringa mjini yanyang’anyiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 25, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MHASIBU mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Ben Mpete amekuwa mwanachama wa CCM wa saba kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega.

  Mbali na Mbega kutangaza kutetea kiti chake hicho, wana CCM wengine waliotangaza nia ya kumpokonya kiti cha ubunge ni pamoja na Edwin Sambala, Frederick Mwakalebela, Thomac Kimata, Jesca Msambalavangu na Zuberi Mwachula.

  Mpete amesema umefika wakati wa kupokezana kijiti kutoka kwa mbunge wa sasa. Mbega amekuwa mbunge kwa awamu tatu tofauti moja akiwa Mbunge wa viti maalumu.

  “Tunakubaliana kwamba kazi aliyoifanya katika kusukuma gurudumu la maendeleo la jimbo la Iringa ni kubwa lakini muda wake wa kupumzika na mimi nimpokee kazi hiyo ya uwakilishi umewadia,” alisema.

  Kama alivyo Mbega, Mpete mwenye shahada ya juu ya uhasibu aliyoipata Novemba mwaka jana alisema atatumia utashi wake kisiasa, vipaji, akili na elimu aliyonayo kusaidiana na wakazi wa jimbo la Iringa Mjini kuharakisha maendeleo.

  Alisema ajenda yake kubwa endapo atachaguliwa itakuwa ni kuufanya mji wa Iringa kuwa mji wa kitalii, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fursa ya elimu bora inakuwa kwa wakazi wote wa mjini hapa.

  “Tutaanzisha mfuko maalumu wa kusaidia wajane na yatima, na mfuko kwa ajili ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30, na pia tutahakikisha vijana wetu wanapata elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha kujua vyanzo vya mitaji, jinsi ya kuwekeza na kufanya biashara na mbinu za kujiajiri,” alisema.
   
Loading...