Iringa: Matukio takribani 404 ya ukatili wa kingono kwa watoto yaripotiwa katika kipindi cha Januari mpaka Novemba mwaka 2019

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
408
1,000
Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha Januari mpaka Novemba 2019 umekuwa na matukio takribani 404 ya vitendo ya ukatili wa kingono kwa watoto ikiwa ni tatizo kubwa linalowakabili watoto katika malezi na makuzi yao nchini.

Hayo yamebainika mkoani Iringa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea vikundi vya malezi kwa watoto katika kijiji cha Kising’a kilichopo Wilaya ya iirnga mkoani Iringa.

Akitoa taarifa hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Saida Mgeni amesema kuwa mkoa wa Iringa unakabiliwa na matatizo mbalimbali na umekuwa ukiongoza katika masuala mabalimbali yasiyofaaa katika jamii ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Serikali ya mkoa wa Iringa imejipanga katika kuhakikisha inapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo kwa kuhakikisha inaratibu utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya vitendo hivyo kwa wanawake na watoto.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali haijalala wala kufumbia macho suala la vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto bali inachukua hatua kali kwa wahusika wa vitendo hivyo wanaobainika.

Dkt. Ndugulile amezitaka Kamati za malezi ya mtoto mkoani Iringa na nchi nzima kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuhakikisha hawawafichi watuhumiwa na hawamalizani kifamilia kesi za ukatil wa kijinsia.

Ameongeza kuwa ni jambo la aibu kwa Tanzania ya viwanda kuwa na vitendo vya kikatili kutokea katika jamii zetu kwani ni kikwazo kikubwa katika kuhakikisha jamii inajiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

“Mkiona wanajamii miongoni mwenu wanataka kumalizana katika kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia toeni taarifa ili tukomehse vitendo hivi visiendelee nchini” alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amewataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanakaa na kuzungumza na watoto wao na sio kuwapiga na kuwapa adhabu zinatazosababisha kupata ukatili wa kisaikilojia ambao ni hatari kwa malezi na makuzi yao na kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao za msingi zilizopo kisheria.

Chanzo: Mtaa kwa Mtaa
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,095
2,000
Ndio watu wanavyombana ivyo na ulinzi wa watoto kwa utaratibu wa kubembelezana.
 

chichiboy1

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
785
1,000
Elimu zaidi inatakiwa si kwa jamii ya Iringa tu, bali maeneo mengi ya nchi yetu..tuungane tuwe na "Sauti Moja"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom