Iringa: Makamu wa Rais, Samia Suluhu azindua Mradi wa Kusimamia Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000

Tuwe pamoja kujuzana kinachojiri.

Ni mradi utakaowezesha kufungua vivutio vya utalii kwa nyanda za juu kusini na kuimarisha zaidi shughuli za kitalii na kuongeza mapato ya nchi yetu

Baada ya kukaribishwa kuhutubia wananchi waliofika katika uzinduzi wa mradi huu, Makamu wa rais Tanzania mama Samia Suluhu Hassani anasema;

=>Awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwa hapa.

Ninafarijika kwa mapokezi mazuri mnayonipa na mnayoendelea kuwapa.

Mradi huu unakusudiwa kutoa ajira za moja kwa moja zinazokisiwa laki 4 na zisizo za moja kwa moja milioni moja.

Katika ziara yangu nimeshudia changamoto ya barabara, serikali ina nia thabiti ya kupanua mtandao wa barabara.

Vivutio vya utalii kanda ya Kusini vinajumuisha maeneo ya kihistoria Kalenga na Isimila, kumbukumbu za vita ya majimaji, Mbozi, ziwa Ngosi mbeya. Natoa rai kwa wizara na idara za serikali kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha ufunguzi wa shughuli za utaalii zinafanikiwa kwa haraka.

Kuendelea kwa shughuli za binadamu kando kando ya mitokumesababisha maji kupungua kandokando ya mito, hivyo kusababisha wanayama kusambaa kwenye makazi ya binadamu, miundombinu duni, ukosefu wa barabara na viwanja vya ndege, gharama kubwa watalii

Serikali inabadilisha historia ya utalii ambayo ilishamiri kanda ya kaskazini pekee. Katika kuendeleza utalii , Serikali imepokea mkopo wa dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya dunia kuendeleza shughuli za utalii kanda ya kusini kwa miaka sita.

Lengo la mradi ni kukuza utalii na kipato cha wananchi kwa kuboresha miundombinu, kujenga uwezo ktk usimamizi wa maliasili na kuwezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija. Mradi utajulikana kwa jina ya RIGRO, utaanza kutekelezwa katika mbuga za Ruaha, Mikumi na Udzungwa.

Ili tuweze kuongeza ufanisi wa mradi huu, lazima maeneo mawili yapewe kipaumbele;
1.Uwanja wa ndege wa Nduli na 2.barabara ya Iringa kwenda Ruaha hifadhini.
Tunaomba benki ya dunia kuangalia ktk awamu ya pili au kipengele kingine ambacho kitaongeza maeneo haya mawili na mradi huu ufanywe kwa ujumla wake.

Sasa tubadilike, tujenge miundombinu ya unyunyiziaji maana umwagiliaji unatumia maji mengi wakati unyunyiziaji unatumia maji kidogo.

Sitavumilia hata kidogo kuendelea kuona tathmini ya mazingira inakuwa kikwazo kwa mradi huu kuendelea.

Tutakapotengeneza ekolojia ya mto wa Ruaha mkuu itatusaidia pia ktk uzalishaji wa umeme. Ninawaomba wananchi mliofika hapa muwe mabalozi wa mradi huu kwa watanzania wengine.

Nawatakia kila la kheri asanteni
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
TBC wanajua kurisha Live mikutano ya kisiasa ya Rais na Makamu wa Rais yenye viashiria vya kiifanyia kampeni CCM

Ila linapokuja suala la kurusha Bunge Live, ndipo vinapokuja visingizio kibao.....

Mara kurusha matanhazo Live ni gharama.....

Mara hizo ni saa za kazi kwa hiyo wananchi hawapaswi waangalie luninga Live, badala yake wanatakiwa kufanya kazi!

Huu ndiyo utendaji kazi wa serikali ya awamu ya 5
 

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
3,916
2,000
Saizi ni muda wa kazi wangerekodi waje warushe usiku tukiwa tumerudi majumbani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom