radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.
Mliopo iringa update muwe mnatupa.
UPDATE
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru
====
ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA
Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.
Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.
Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.
Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.
Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.
Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.
Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC
zaidi, soma:

Mahakama kuu yampa tena Ushindi Abdul Nondo dhidi ya serikali, baada ya kudaiwa kujiteka
Jaji wa mahakama kuu Tanzania Mhe.Panterin Kente amemwachia huru Abdul Nondo kwenye hukumu ya rufaa iliyokatwa na jamhuri dhidi ya maamuzi ya mahakama ya hakimu mkazi Iringa yaliyompa ushindi katika kesi ya kudaiwa kujiteka na kutoa taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii. ==== Mahakama...
www.jamiiforums.com