Iringa: Mabinti waliokimbia kwao kisa maisha magumu warejeshwa kwenye mstari

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Vijana waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu ambao baadhi yao walikuwa na mzigo mkubwa wa kutunza familia zao na hata mabinti kukimbia vijiji kwenda kufanya kazi za ndani, hivi sasa maisha yao yamekuwa tofauti baada ya kufikishiwa elimu ya ujasiliamali na elimu ya Saikolojia.

Elimu hiyo wameipata katika mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) ambapo Meneja YAM, Zilipa Mgeni alimesema hayo leo Machi 23, 2022 wakati wa mafunzo ya siku 10 Kwa vijana 100 kutoka kata tatu za Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Zilipa alisema kutokana na mwendelezo wa mafunzo hayo yaliyoanza mwaka jana na tathimini ndogo ambayo mradi umefanya kupitia viongozi wa vijiji na kata wanazotoka wameona Kuna mabadiliko makubwa Kwa vijana waliokwisha fikiwa na mradi huo .

Kwani alisema baadhi yao wameepuka tabia za kushinda Vijiweni na hata wale waliokuwa wanategemea kuendesha maisha yao Kwa kwenda mijini kufanya kazi za ndani hivi sasa wametulia Vijijini kufanya shughuli zao wenyewe.

Alisema kuwa Katika mafunzo hayo ya siku 10 yameanza jana katika Ukumbi wa Yatima, Kijiji cha Igoda, Wilaya ya Mufindi kwa kushirikiasha na vijana hao ambao baadhi yao ni wale ambao wamekatisha masomo kwa changamoto mbalimbali kimaisha ikiwa ni pamoja na mabinti waliokatisha kwa mimba za utotoni wameanza kujitambua.

Akizungumzi faida ya mafunzo haya meneja wa mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) Zilipa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana zaidi ya 770 wakiwemo watoto 150 yatima kutoka kata hizo tatu ambazo zote zitaunganishwa na vijiji 16 za mradi huo.

Alisema mradi huo wa YAM ni wa miaka minne kutoka mwaka 2021/2024 umefadhiliwa na serikali ya Filands chini ya taasisi yake ya Diaconess kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation (FCWC).

Mgeni alisema baada ya mafunzo hayo kutolewa kwa walengwa watawezeshwa mitaji ya kuendeshea miradi ambayo watakuwa wamechangua kuifanya kwa kuwaongezea nguvu ya kuiboresha zaidi.

Mkufunzi wa mafunzo hayo mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Dkt Blandina Kivavike amesema kuwa mafunzo hayo maalum ni ya kuwajengea uwezo wa katika nyanja ya ujasiliamali yatawezesha vijana hao kuweza kuondokana na fikra mgando ambazo baadhi yao wamekuwa nazo kuwa ili uwe mjasiliamali ni lazima kuwa na fedha mkononi wakati unaweza kuwa mjasiliamali bila ya kuanza na mtaji wa fedha.

"Maeneo mengi ya vijijini kuna fursa nyingi za kufanya ambazo kimsingi ni moja kati ya mtaji mkubwa kwa mtu ambaye anatamani kuwa mjasiliamali hivyo iwapo wahusika wataondokana na fikra mgando za kutegemea fedha wanaweza kupiga hatua katika maisha," alisema

Kuwa ili vijana hao waweze kuondokana dhana hiyo potofu ni lazima kwanza kujitambua na kujiamini kabla ya kuanza shughuli ya ujasilimali ambayo anahitaji kuifanya na baada ya kuanza ndipo wanaweza kuanza mchakato wa pili wa kuomba mikopo ya kuboresha shughuli husika ya ujasiliamali.

Hata hivyo alisema kupitia ardhi walizonazo vijijini ziwe za familia ama zao binafsi wanaweza kubuni miradi ya kiuchumi ambayo miradi hiyo haihitaji mtaji mkubwa wa fedha zaidi ya kuhitaji nguvu kazi ya mkono.

Alisema mfano ujasiliamali wa ususi kwa mabinti ni ujasiliamali ambao mtu anaweza kuanza kwa ubunifu usio tegemea fedha na baada ya kuanza ndipo wanaweza kuboresha kwa kutafuta eneo litakalohitaji fedha za kuboresha zaidi.

Akizungumza Kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Zulea Mkiwa alisema mafunzo hayo yameendelea kumfanya kuwa tofauti na mwanzo kabla ya mafunzo na Imani yao kuwa mfano mwema Kwa jamii.

Wilaya ya Mufindi ni moja kati ya wilaya tatu za mikoa wa Iringa ambazo zimekuwa na changamoto ya vijana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kupitia serikali na wadau mbali mbali wa maendelea wameendelea kuwawezesha vijana hao ili kuanzisha miradi ya kiuchumi inayowafanya kupiga hatua za kimaendeleo

2b24cd56-8409-4ba9-b9ca-f7875bfdabd7.jpg
Mabinti waliopitia wakati mgumu.


92f4d1ef-5bad-46ea-af4f-fe95975a4313.jpg

Mhadhiri Chuo Kikuu Iringa, Dkt Blandina Kivavike ambae ni Mkufunzi Mafunzo

624c5fb3-bbc4-4e2c-a29b-da7a2d769d4c.jpg

Zulea Mkiwa Mnufaika Mradi wa YAM.





Source: Matukio Daima Blog
 
Back
Top Bottom