Iringa kwachafuka: FFU watumia mabomu, waandishi wapigwa mawe

tbl

Senior Member
Mar 29, 2011
116
41
WanaJf ni iringa hapa mitaa ya frelimo watu wamejazana sana kwenye nyumba ya mama mmoja wanadai kuna misukule imekutwa amefungia kwenye moja ya chumba katika nyumba yake,inasemekana wananchi walitaka kumpiga mama huyo na hivyo polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya,naona kwa mbali jamani mwembetogwa huku zinapita gari za polisi tu na ving'ora juu aliyepo karibu atujuze tafadhali
 
Mimi nimefanikiwa kukaribia eneo husika. Karibu mji mzima walikuwa hapa. Wananchi wamempiga sana mtuhumiwa na amekimbizwa hospitali, pia wameharibu nyumba yake kwa mawe,wamevunjavunja gari ya polisi. Ilibidi askari watumie mabobu ya machozi na risasi za moto kutawanya watu. Nyumba inalindwa na polisi kwani watu wanataka kuchoma moto, na njia kuelekea eneo husika imefungwa na polisi.
 
Halafu hii ishu mi naisikia nikiwa kazini kama utani vile,pia na sikia huyo Mama mbilinyi alipata kitu kama uchizi,akaanza kupayuka hadharani kwamba kuna watu aliowaweka ndani kama misukule.Kama haitoshi,alidiriki kumwambia mama mmoja kwamba mwanae aliyekufa kwa kugongwa na gari hakufa kweli bali yeye amemchukua msukule na akamwambia yule mama aende akamchukue mwanae nyumbani kwake kwani bado hajamkata hata ulimi.Cha ajabu inasemekana huyu Mama Mbilinyi ni mmiliki wa redio maarufu ya kidini hapa mjini Iringa,OVERCOMERS FM!
 
Askari wa kikosi cha askari wa kutuliza Ghasia (FFU) Iringa watumia mabumu kuwatawanya wananchi waliovamia nyumba ya mtumishi wa Mungu kwa madai kuwakuna misukule.

Wananchi hao wenye hasira kali zaidi ya 200 walitumia mawe kuwashambulia FFU huku wao FFU wakitumia mabomu ya machozi kupambana Huku wanahabari wa vyombo mbali mbali na askari polisi na mchungaji mmoja wakinusurika kuuwawa wakishambuliwa kwa mawe na wengine kuvunjiwa kamera zao na wananchi hao ambao walionyesha kuwachukia askari polisi pamoja na wanahabari ambao waliteuliwa na wananchi wenyewe kuwawakilisha katika kukagua nyumba hiyo bila mafanikio.

Tukio hilo lilitokea eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa na kudumu zaidi ya masaa manne baada ya kuanza majira ya saa 8 mchana na kuendelea hadi saa 12.50 jioni.

Wakielezea juu ya tukio hilo wananchi hao walisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya wananchi wa eneo hilo kuwa katika nyumba hiyo ya mfanyabiashara wa maji kumeonekana misukule 15 ambayo ilionekana ndani ya uzio wa nyumba hiyo.

Kutokana na uvumi huo wananchi kutoka pande mbali mbali za mji wa Iringa walifika katika nyumba hiyo na kuizingira kwa lengo la kutaka kuichoma moto kabla ya askari polisi kufika na kuwaomba wananchi kutofanya hivyo na badala yake kuteuwa wawakilishi ili kuingia ndani ya nyumba hiyo kujikagua misukule hiyo bila mafanikio.

Hata hivyo baada ya askari hao walioambatana na wanahabari zaidi ya sita kutoka vyombo mbali mbali akiwemo mwandishi wa habari hizi kushindwa kuona misukule hao baadhi ya wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi waliamua kuruka ukuta baada ya kuona wananchi wakionyesha jazba zaidi.

Huku baadhi ya waandishi wakiongozwa na katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard ambaye ni mwandishi wa gazeti la Habari leo wakilazimika kujifungia ndani ya nyumba hiyo baada ya wananchi kuanza kuishambulia kwa mawe.
Hali hiyo iliwalazimu askari polisi zaidi ya 10 walikuwepo kuanza kutumia mabumu ya machozi kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiimba kuwa mmekela rushwa wote wanahabari,wachungaji na polisi hivyo lazima mchomwe moto.

Katika tukio hilo mabomu ya machozi zaidi ya 30 yalipigwa hewani huku wananchi wakizidi kuongezeka na kupelekea askari hao kuomba msaada zaidi wa askari wa FFU ambao walifika wakiongozwa na mkuu wa FFU mkoa wa Iringa Mnunka na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao.

Zaidi ya watu 10 walikamatwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na vurugu hizo huku watu wengine zaidi ya 20 wakiwemo wanahabari familia ya mfanyabiashara huyo ,mchungaji aliyefahamika kwa jina la Mang'uliso walijeruhiwa kwa mawe.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla hakuweza kupatikana kuzungumzia madhara yaliyojitokeza katika tukio hilo japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari matatu likiwemo la polisi yakiwa yameharibiwa vibaya kwa mawe.

4712530841850548562-4433966476443058166
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin

mhhh inakuwaje kama tu kachanganyikiwa akasema hivo
kuna watu wameona misukule hiyo?
 
kila mahali ni mabomu kwa kwenda mele halafu eti kiongozi anatarajia angechaguliwa mshindi wa tuzo ya mo ibrahim
 
Hivi hawaogopi hiyo akiba ya mabom itaisha halafu watashindwa kumtishia hata mtoto wa kindergaten??
 
Ni vizuri watanzania wazoee mabomu ili mapunduzi ya kweli yakianza tusiwe waoga tena kama ilivyo hadi sasa
 
Halafu hii ishu mi naisikia nikiwa kazini kama utani vile,pia na sikia huyo Mama mbilinyi alipata kitu kama uchizi,akaanza kupayuka hadharani kwamba kuna watu aliowaweka ndani kama misukule.Kama haitoshi,alidiriki kumwambia mama mmoja kwamba mwanae aliyekufa kwa kugongwa na gari hakufa kweli bali yeye amemchukua msukule na akamwambia yule mama aende akamchukue mwanae nyumbani kwake kwani bado hajamkata hata ulimi.Cha ajabu inasemekana huyu Mama Mbilinyi ni mmiliki wa redio maarufu ya kidini hapa mjini Iringa,OVERCOMERS FM!

No wonder makanisa mengi ya siku hizi ni ya ki-misukule!
 
Mkuu, ni mama Mbilinyi nini mkuu!!!
yule mume wake yule alikuwa anajifanya mchungaji!!!, huku mkewe akisemwa kwamba ni mkali wa mambo yale ya gizani.
walikuwa majirani zangu hao!!! damn!
 
Halafu hii ishu mi naisikia nikiwa kazini kama utani vile,pia na sikia huyo Mama mbilinyi alipata kitu kama uchizi,akaanza kupayuka hadharani kwamba kuna watu aliowaweka ndani kama misukule.Kama haitoshi,alidiriki kumwambia mama mmoja kwamba mwanae aliyekufa kwa kugongwa na gari hakufa kweli bali yeye amemchukua msukule na akamwambia yule mama aende akamchukue mwanae nyumbani kwake kwani bado hajamkata hata ulimi.Cha ajabu inasemekana huyu Mama Mbilinyi ni mmiliki wa redio maarufu ya kidini hapa mjini Iringa,OVERCOMERS FM!
mkuu, wamemtwanga huyo mama au mmewe yule **** **** hivi??
duh!! one time alikuwa jirani yangu huyo!!
 
Wangemtia kiberiti tuu atangulie mbele za haki huwezi weka wenzio kama misukule!
Huyu maana mambo ya giza ameanza kitambo sana na ndiko utajili wake unakotokea uko!
 
Back
Top Bottom