IRINGA: Jeshi la polisi lamshikilia Mwalimu kwa kuchapa mwanafunzi na kumsababishia kifo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Jeshi la Polisi linamshikilia mwalimu mmoja wa S/Msingi Ng'ingula kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanafunzi kwa kumchapa viboko.

=======

JESHI la Polisi mkoani Iringa linamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Ng’ingula, Wilaya ya Kilolo, Robson Sanga (59), kwa tuhuma za kumua mwanafunzi wa darasa la tano, Emmanuel Gavile (13) kwa kumchapa fimbo mapajani kwa kuchelewa shuleni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 16, mwaka huu saa 3.00 asubuhi shuleni hapo baada ya mwanafunzi huyo kudaiwa kuchelewa kufika shuleni kwa muda ambao shule imeuweka.

Alisema kutokana na adhabu hiyo, Gavile alilia kwa maumivu makali na kushindwa kujisomea hali iliyowafanya wenzake kumkimbiza katika zahanati ya kijiji hicho ambako hali ilizidi kuwa mbaya.

Baadaye alihamishiwa Kituo cha Afya Usokomi wilayani humo.

“Agosti 26 mwaka huu mwanafunzi huyo alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa akilalamikia maumivu makali katika paja la mguu wa kulia kabla ya kufariki dunia saa 3.00 asubuhi,” alisema Mjengi.

Kamanda alisema uchunguzi wa daktari umeonyesha kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kilisababishwa na kupasuka mfupa wa paja la mguu wa kulia na damu kuviria katika mapafu yake.

Alisema kwa muda wote huo wazazi hawakuweza kuripoti polisi ila baada ya kifo cha mwanafunzi huyo ndipo walipofika kituo cha polisi kutoa taarifa na jeshi hilo limemkamata mwalimu huyo kwa uchunguzi.


Chanzo: Mtanzania
 
Mwalimu au mzazi anayemwadhibu mtoto kwa fimbo kubwa au nyingi kama mnyama hana akili bila kijali umri wa mzazi au mwalimu huyo.
Akili za kitumwa Afrika zinawatesa wengi.
Leo asubuhi nilisikia jirani akimpiga mwanawe kama mfungwa nikamwambia mke wangu kwamba huyo mama hana akili timamu, mtoto ni rafiki yako na si adui yako.
Kama una roho mbaya si bora usizae na mwalimu kama una roho mbaya si bora usiwe mwalimu tu.
 
Sijui kwanini hii adhabu ya kikoloni na kikatili bado inaendelea kuruhusiwa, mbaya zaidi waathiriwa wakubwa ni watoto wadogo wa shule za msingi wasioweza kujilinda wala kujitetea. Watoto wanapata madhara ya muda mrefu kisaikolojia, wengi wanabakia kua waoga waoga maisha yao yote mbele ya mtu mwenye madaraka. Nashukuru mungu mara ya mwisho nilipigwa viboko nikiwa darasa la 6, kutoka hapo ilikua nikiona kuna adhabu ya viboko nilikua nabeba daftari zangu narudi nyumbani. Zogo likiwa kubwa tulikua tunakimbilia kwa afisa elimu pale zimamoto mbeya mjini, kuna mama mmoja alikua mwelewa sana.
 
Ivi hii ndo ile waliyosema wahenga kwamba eti ajali kazini?nauliza tu jamani
 
Itakuwa hakumchapa na fimbo za kawaida itakuwa alitumia fimbo zile za kuchungia ng'ombe maana fimbo za kawaida wahenga tumechezea sana na hakukuwa na madhara kama haya siku hizi.
 
Dyu!! Ualimu ni shughuli!!!

Kuna sehemu sijaelewa, fimbo ya paja na mbavu kuvilia damu. Au mwalimu alichapa mbavu za mtoto.....dah!!!!

R.I.P mwanafunzi.
 
Back
Top Bottom