JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha na fidia ya shilingi milioni 7 dereva wa Bajaji, John Umbo (20) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka 10.
Imeelezwa kuwa siku ya tukio Mei Mosi, 2021 alimrubuni mtoto huyo na kumpeleka kichakani ambapo alimwambia mwathirika achague moja, kuuawa au kubakwa.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Saidi Ally Mkasiwa alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea lakini alibaki kimya.
Mtuhumiwa huyo ambaye amewahi kuwa na kesi kadhaa za ukatili wa kijinsia siku za nyuma na alifikishwa Mahakamani lakini hakuwahi kukutwa na hatiani.
Chanzo: Azam TV