Iringa: Dereva Bajaji atupwa Jela maisha kwa kumbaka mwanafunzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
1,191
3,028

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha na fidia ya shilingi milioni 7 dereva wa Bajaji, John Umbo (20) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka 10.

Imeelezwa kuwa siku ya tukio Mei Mosi, 2021 alimrubuni mtoto huyo na kumpeleka kichakani ambapo alimwambia mwathirika achague moja, kuuawa au kubakwa.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Saidi Ally Mkasiwa alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea lakini alibaki kimya.

Mtuhumiwa huyo ambaye amewahi kuwa na kesi kadhaa za ukatili wa kijinsia siku za nyuma na alifikishwa Mahakamani lakini hakuwahi kukutwa na hatiani.

Chanzo: Azam TV
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
14,082
18,325
Mtoto wa miaka 10,hapa nahisi imani za kishirikina zitakuwa zinanahusishwa...
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
5,833
5,468
Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ndio vinara wa maambukizi ya Ukimwi lkn pia vitendo vya ubakaji vimeshamiri huko.

Viongozi wa dini ktk maeneo hayo wanao wajibu wa kueneza neno la Mungu ktk maeneo hayo.
 
allypipi

JF-Expert Member
May 10, 2020
1,776
5,054
Serikali ingezi angalia upya hizi sheria kwasasa kijana wa miaka 20 ni mtoto kabisa yani hata kimawazo.
 
Mkwe21

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,723
1,802
Mtoto wa miaka 10,hapa nahisi imani za kishirikina zitakuwa zinanahusishwa...
Inabidi hizi mahakama nazo ziwe makini, isijekuwa huu ni wivu WA mafanikio ya huyu ndugu mtu amemnenea mabaya na kujiapiza ataona!! Pia wachunguze uhusiano WA mama WA huyo mtoto na huyo kijana!! Inaweza kuwa kesi ya kupika
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
13,750
14,883

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha na fidia ya shilingi milioni 7 dereva wa Bajaji, John Umbo (20) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka 10.

Imeelezwa kuwa siku ya tukio Mei Mosi, 2021 alimrubuni mtoto huyo na kumpeleka kichakani ambapo alimwambia mwathirika achague moja, kuuawa au kubakwa.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Saidi Ally Mkasiwa alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea lakini alibaki kimya.

Mtuhumiwa huyo ambaye amewahi kuwa na kesi kadhaa za ukatili wa kijinsia siku za nyuma na alifikishwa Mahakamani lakini hakuwahi kukutwa na hatiani.

Chanzo: Azam TV
Wangesubiri msimu wa baridi la Iringa uishe ndiyo aanze kutumikia kifungo.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom