Iringa, baraza la madiwani laitishwa kumng'oa Meya, baada ya mahakama kutupa madai yake kwa kukosea vifungu vya pingamizi lake

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Saa chache baada ya Mahakama ya Mkoa kutupa maombi ya kuzuia mchakato kumng’oa meya ya Manspaa ya Iringa, Alex Kimbe, Baraza Maalumu la Madiwani limeitisha kikao kinachoaminika kitahitimisha suala hilo.

Kikao hicho kilichoitishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, kitafanyika leo saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa Manispaa ili kukamilisha majukumu ya mkutano ulioahirishwa Machi 26.

Taarifa ya mkutano huo kwa wananchi iliyosainiwa na ofisa habari wa manispaa, Siima Bingileki inasema kikao hicho kimeitishwa chini ya kanuni ya 9(4) ya kanuni za kudumu za manispaa zilizotolewa mwaka 2015.

Mapema jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Iringa iliyotoa maamuzi ya mapingamizi ya serikali dhidi ya maombi ya Meya Kimbe ikisema alikosea katika kuyawasilisha.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Aden Kanje alisema kutokana na kukosea vifungu, mahakama imeona maombi hayo hayana mashiko

Mahakama hiyo ilipokea maombi ya meya kuzuia mchakato wa kung’olewa Machi 12, 2020 na upande wa Jamhuri uliwasilisha pingamizi Machi 17 na kusikilizwa siku hiyo hiyo.

Hakimu Kanje alisema amesikiliza hoja za pande zote zilizojikita katika mamlaka ya mahakama ya kuzuia mchakato wa kumng’oa meya, na kubaini kuwa “mamlaka ya mahakama yana mipaka kisheria na huwa ni ya mpito ya siku 90 na si ya kudumu, kama alivyokuwa anaomba meya”.

Akizungumza nje ya mahakama, wakili wa meya huyo, Barnabas Nyalusi alisema anasubiri nakala ya uamuzi huo ili ashauriane na mteja wake kuhusu hatua ya kufuata.

“Hakimu hajafuta kesi bali amesema vifungu ambavyo tumetumia katika maombi yetu havikuwa sahihi, kwa hiyo lazima tukasome tena vifungu na kushauriana na mteja wangu,” alisema.

Alisema mteja wake alikuwa anazuia mchakato wa kumtoa meya madarakani, hakuzuia meya kuondolewa kwa kuamini mchakato huo haukufuata sheria.

“Kanuni za kudumu za manispaa zinaeleza wazi ili meya aondolewe ni vitu gani vinatakiwa vifuatwe,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwenye mambo yenye Maslah ya Nchi huwa tunatazama maslahi ya Nchi kabla ya Katiba

Yeye Meya ndio alipaswa kupata theluthi mbili ya wanaomuunga mkono asitumbuliwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambieni arudi tena mahamakani Kwa kile kinachodaiwa kukosewa Kwa vifungu vya pingamizi,ajipange vizuri aende tena, wenzie hawana huruma watamng'oa kweli, mbona rahisi tu
 
In Tanzania, everything is politics, and politics is everything!!
Hapana mkuu. You are giving politics a bad name.
Hii sio siasa, huu ni utoto, upuuzi na upumbavu.
Watu wazima wenye akili timamu badala ya kufanya mambo yao na kuwatumikia wananchi wanahangaika na ujinga huu miezi saba kabla ya uchaguzi!
Sijui watu wamekuaje yaani miaka hii
 
Business as usual

Sent using Jamii Forums mobile app

Yale yale ya Meya Isaya Mwita...!!
Wabunge wote wa CHADEMA wameshanunuliwa na CCM na kilichobakia Sasa Ni KUBADILI MAMEYA KWA LAZIMA KUPITIA MAHAKAMA....!!!
Yaani Ushindi wa CHADEMA kupitia sanduku la KURA mwaka 2015 unaporwa kupitia RUSHWA na MAHAKAMA..!Hakika CCM ya Magufuli imelaaniwa...!
 
Hapana mkuu. You are giving politics a bad name.
Hii sio siasa, huu ni utoto, upuuzi na upumbavu.
Watu wazima wenye akili timamu badala ya kufanya mambo yao na kuwatumikia wananchi wanahangaika na ujinga huu miezi saba kabla ya uchaguzi!
Sijui watu wamekuaje yaani miaka hii

Hakika huu ni UPUUZI na UPUMBAF uliopitiliza unaofanywa na majambazi wa CCM....!
Maficcm wanahangaika na kumng'oa Meya wa Iringa Mjini wakti huu wa janga la CORONA ili kufanikisha huu ujinga!

CCM wanaitumia CORONA kufanikisha Mambo yao ya kishenzi...!!
Tumeona kina Halima Mdee na wenzake juzi wakipelekwa Mahakamani kwa kesi ya kutengeneza"KUVAMIA GEREZA LA SEGEREA"....Hakika ni Ushetwani mtupu!
 
Yale yale ya Meya Isaya Mwita...!!
Wabunge wote wa CHADEMA wameshanunuliwa na CCM na kilichobakia Sasa Ni KUBADILI MAMEYA KWA LAZIMA KUPITIA MAHAKAMA....!!!
Yaani Ushindi wa CHADEMA kupitia sanduku la KURA mwaka 2015 unaporwa kupitia RUSHWA na MAHAKAMA..!Hakika CCM ya Magufuli imelaaniwa...!
Mkuu haya mambo ya ajabu. Watu wetu wengi sana ni maskini kabisa, badala ya kupambana kuwasaidia tunafanya vitu vya namna hii.
Hata kama hatuna ushahidi wa manunuzi ya wanasiasa lakini kweli kabisa yaani hatuna viongozi, wastaafu na wazee wa kukemea hizi vurugu! Ya Dar es Salaam ilikuwa ni aibu zaidi nasikia walimzuia meya kuingia ofisini! Sisi waafrika sijui tukoje yaani, hatujitambui!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom