BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,365
- 8,097
Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyopewa mamlaka ya ziada mkoani Iringa imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Abuutwalib Seif (34) Mkazi wa Igumbilo, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa kumtupa mtoto wake Khadija Seif (5) mto wa Ruaha. Mtoto alikuwa ni mlemavu wa viungo.
Akisoma kesi hiyo jana Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Said Ally Mkasiwa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akijishughulisha na kazi ya upigaji debe katika kituo Kikuu cha Mabasi cha Igumbilo.
Aidha kwa mujibu wa taarifa za mahakamani hapo, mtuhumiwa alikuwa akiishi na mtoto huyo ghafla akawa haonekani na alipoulizwa na majirani alisema amemrudisha kwa bibi yake.
"Mwili wa mtoto huo ulipopatikana akiwa amekufa Mto Ruaha majirani walimfata na kumwambia mtuhumiwa lakini hakuonesha Jitihada zozote za kwenda kuuchukua ndipo akakamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi," amesema hakimu huyo.
Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 6 wakiwemo majirani waliothibitisha kumtambua mtoto huyo ambaye alikuwa mlemavu wa viungo ndipo mahakama ikamtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa kutenda kosa.
Akitoa malezo yake ya awali mtuhumiwa amekiri kumtupa mtoto huyo Mto Ruaha saa 8 usiku kutokana na hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikimkabili.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Magreth Mahundi aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ambaye ametenda kosa hilo kwa mtoto wake wa kumzaa.
Kwa upande wake wakili aliyemsimamia Mtuhumiwa Cosmas Kishamawe aliiomba Mahakama kumuachilia huru mtuhumiwa kwa sababu ni kosa la kwanza na ana mtoto na wazazi wake ambao wanamtegemea na umri wake bado ni mdogo hivyo ana ndoto nyingi ambazo angependa kuzitimiza.
Hata hivyo mahakama ikamuhukumu kifungo cha kunyongwa mpaka kufa kwa kosa la kumtupa mtoto wake akiwa hai katika Mto Ruaha.
MWANANCHI