Iringa: Afungwa jela miaka mitatu kwa kumchoma mikono mtoto wa kambo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,067
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Edward Uphoro ametoa adhabu kwa mshtakiwa Bruce Karistus aliyekiri kutenda kosa hilo dhidi ya mtoto wake wa kufikia.

Kwa mujibu wa Mashtaka imeelezwa kuwa Oktoba 21, 2022 Karistus alimjeruhi sehemu mbalimbali za mwili mtoto mwenye miaka 7 baada ya kumtuhumu kuiba Tsh. 1000.

Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea, aliomba Mahakama impunguziea adhabu kwa sababu ni kosa lake la kwanza na ana familia inayomtegemea.

========================

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu kifungo cha miaka mitatu Bruce Karistus maarufu kwa jina la Nyaluva (31) kwa kosa la kumchoma na kumsababishia majeraha mtoto Scola Ramadhani mwenye umri miaka saba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 15 katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa katika shauri la jinai namba 64 la mwaka 2022.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Edward Uphoro amesema mshtakiwa huyo amekutwa na hatia kwa kosa la kumchoma mtoto na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mawili wake mtoto wake wa kufikia.

Amesema kuwa Oktoba 21 mwaka huu mshaktiwa akiwa nyumbani kwake alipewa taarifa na mama wa mtoto aitwaye Rebeca kwamba mtoto huyo ameiba Sh1, 000.

"Baada ya kupata taarifa hizi mshtakiwa alimchukua mtoto na kumpeleka jikoni na kuchukua kijinga cha moto na kuanza kumchoma sehemu mbalimbali za mawili wake ikiwemo mapajani pamona na mabegani," amesema Hakimu huyo.

Uphoro ameeleza kuwa baada ya kuona hivyo mama wa mtoto huyo alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya kijiji, ambapo Nyaluva alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Mafinga ambapo alipoulizwa alikiri kutenda kosa hilo.

Amesema kuwa baada ya kukiri kutenda kosa hilo leo Novemba 15 amefikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka lake ambapo alikiri na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela. Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea, aliomba mahakama hiyo impunguziea adhabu kwa sababu ni kosa lake la kwanza na anafamilia ambayo inamtegemea.

MWANANCHI
 
kuzaa mtoto na kumwachia mzazi mmoja, ni kumtakia maisha ambayo si ya nchi hii .
mm hapa nililelewa ki-alshababu! Japo kwa sasa najivunia nilichokipata
 
Sheria sijui zikoje, yaani ukichoma nyumba moto unafungwa jela maisha, ila ukichoma binadamu moto unafungwa miaka mitatu
 
Sheria sijui zikoje, yaani ukichoma nyumba moto unafungwa jela maisha, ila ukichoma binadamu moto unafungwa miaka mitatu
Hii Sheria ya kuchoma nyumba ilikua Ina wa favour Sana wakoloni halafu kwa ujinga wetu tumeirithi.
 
Back
Top Bottom